Monday, November 19, 2018

JENISTA MHAGAMA ATOA VYETI KWA WAHITIMU WA PROGRAMU YA MWANAMKE WA WAKATI UJAO (FEMALE FUTURE PROGRAMME)

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii .


CHAMA cha Waajiri Tanzania (ATE) wamefanya mkutano mkuu wa kwanza wa wanawake katika uongozi kwa mwaka 2018 uliombatanisha mahafali ya pili ya programu ya mwanamke wa wakati ujao (Female Future Programme). 

ATE wamefanya mkutano huo wakishirikiana na Shirikisho la vyama vya waajiri nchini Norway (NHO) wenye lengo la kuwajengea uwezo wanawake kwa ajili ya kushika nafasi za juu za uongozi na kuwapa uwezo wa kuingia kwenye bodi mbalimbali na kushiriki katika maamuzi.

Akifungua Mkutano huo, Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira ma Wwtu wenye Ulemavu Jenista Mhagama amesema mkutano huu mkubwa wa mwaka wa uongozi kwa wanawake unaenda samamba kabisa na juhudi za nchi yetu katika kuhakikisha idadi ya wanwake kwenye nafasi zao za juu za uongozi inazidi kuongezeka pia wanawake kuwa na idadi kubwa ya uwakilishi katika bodi za wakurugenzi za makampuni mbalimbali. 

"Serikali ya awamu ya tano imeendelea kusimamia na kuhakikisha kunakuwa na uwiano mzuri wa viongozi wanawake ndani ya serikali na jumuiya mbalimbali , makampuni ya kibiashara nchni na katika kufanikisha hili serikali imeanzisha mpango mkakati wa kitaifa kwa ajii ya maendeleo ya usawa wa kijinsia ambapo upo kwenye dira ya maendeleo ya Taifa 2025"amesema Jenista. 

Jenista amesema, programu hiyo ni fursa kwa wanawake wa wakati nujao na mafunzo hayo wakiyatumia vizuri yatawasaidia kuendesha maisha katika nyanja mbalimbali, kazini, nyumbani, kwenye jamii na kwa kizazi kijacho. 

Amesema, kwa mwaka 2017 idadi ya wanawake katika bodi mbalimbali za taasisi za serikali iliongezeka na kufikia 117 kutoka 114 kwa mwaka 2014 ikilinganishwa na wanaume ambapo walipungua toka 526 mwaka 2014 hadi 352 mwaka 2017, aidha katika miaka hiyo idadi ya wanawake majaji imeongezeka na kufikia 39 kati ya majaji 95, wakati mwaka 2012 majaji wanawake walikuwa 34 kati ya 97.

“Programu hii kwangu ni fursa kwenu na mafunzo haya mkiyatumia vizuri yatawasaidia kuendesha maisha katika Nyanja mbali mbali: kazini, nyumbani, kwenye jamii na kwa kizazi chetu kijacho” aliongeza Waziri Jenista. 

"Nawapongeza Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) kwa mafanikio haya makubwa ya kutoa mfunzo kwa Wanawake 25 kutoka makampuni 16 katika Awamu hii ya pili ya Programu hii ya Mwanamke wa Wakati Ujao kwani imekuwa ni sehemu ya kuongeza Wanawake wengi zaidi katika nafasi za uongozi na uwakilishi katika Bodi za Wakurugenzi katika Taasisi mbalimbali," 

Naye Mkurugenzi wa ATE, Dkt. Aggrey Mlimuka alisema kuwa katika Awamu ya Pili ya Programu ya Mwanamke wa Wakati ujao ATE wameweza kutoa mafunzo kwa Wanawake 25 kutoka kampuni na Taasisi 16.

“Tumetoa mafunzo haya kwa kushirikiana na Chuo cha Mafunzo ya Uongozi Afrika Mashariki na Kusini (ESAMI) na katika awamu hii ya Pili ya mafunzo jumla ya wanawake 25 kutoka katika makampuni na Taasisi 16 ambayo yamefadhili mafunzo haya yaliyokuwa na sehemu kuu tatu ambazo ni Uongozi, Ufanisi katika Bodi na Ufanisi katika utekelezaji wa majukumu mahali pa Kazi” 

Hivyo basi napenda kutoa wito kwa makampuni, Taasisi, Mashirika ya Kiserikali na Binafsi kuendelea kuunga mkono programu kwa kuleta wafanyakazi wengi zaidi ili waweze kupatiwa mafunzi haya kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.

Dkt. Mlimuka aliongeza kuwa Programu ya Mwanamke wa Wakati Ujao imelenga hasa kujenga uwezo Wanawake katika kuongoza kwenye Nafasi za juu na kuleta matokeo makubwa katika kampuni na taasisi zao pasipo kuathiri majukumu yao Binafsi. 

“Programu ya Mwanamke wa Wakati ujao ina Malengo Makuu matatu ambayo ni Kupata Wanawake wengi Zaidi kwenye nafasi za juu za uongozi, kwenye hatua za kufanya maamuzi na pia kwenye Bodi Mbalimbali za Wakurugenzi, Pili ni kuwahamasisha na kuwapa changamoto viongozi wanawake kufanya kazi kwa juhudi na malengo makubwa ili kuhakikisha wanapata matokeo chanya kwenye makampuni na taasisi zao wanazoziongoza na Tatu ni Kutengeneza Jukwaa kubwa la Wanawake kwa ngazi zote kuka pamoja na kubadilishana uzoefu kuhusiana na uongozi” Alifafanua Dr. Mlimuka. 

Akitoa salamu zake Mwenyekiti wa ATE Bi. Jayne Nyimbo alisema kuwa Mkutano huu Mkuu wa Uongozi kwa Wanawake uliobeba kauli mbiu ya wenye kauli mbiu isemayo “Uongozi wenye Ufanisi kwa Mazingira yanayobadilika Kibiashara” ni moja ya mkakati wa Programu ya Mwanamke wa wakati ujao wa kuhakikisha inawaleta pamoja wanawake na kuwawezesha kukua kiuongozi. 

“ATE tukiwa ndio wawakilishi wa waajiri wote nchini furaha yetu ni kuona wanachama wetu ambao ni taasisi na makampuni mbalimbali wanakuwa na Viongozi wanawake wenye uwezo mkubwa lengo likiwa kuongeza uzalishaji wa taasisi zao na taifa kwa ujumla” Alisema Jayne Nyimbo. 
Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira ma Wwtu wenye Ulemavu Jenista Mhagama akizunguzma wakati wa 

mkutano mkuu wa kwanza wa wanawake katika uongozi kwa mwaka 2018 uliombatanisha mahafali ya pili ya programu ya mwanamke wa wakati ujao (Female Future Programme).
Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waajiri Nchini (ATE) Dkt Aggrey Mlimuka akizzungumza na waandishi wa habari wakati wa 

 mkutano mkuu wa kwanza wa wanawake katika uongozi kwa mwaka 2018 uliombatanisha mahafali ya pili ya programu ya mwanamke wa wakati ujao (Female Future Programme).

Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira ma Wwtu wenye Ulemavu Jenista Mhagama akitoa cheti kwa moja ya wahitimu Arafa wakati mkutano mkuu wa kwanza wa wanawake katika uongozi kwa mwaka 2018 uliombatanisha mahafali ya pili ya programu ya mwanamke wa wakati ujao (Female Future Programme).


Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira ma Wwtu wenye Ulemavu Jenista Mhagama akitoa cheti kwa moja ya wahitimu Bahati Minja wakati mkutano mkuu wa kwanza wa wanawake katika uongozi kwa mwaka 2018 uliombatanisha mahafali ya pili ya programu ya mwanamke wa wakati ujao (Female Future Programme).

Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira ma Wwtu wenye Ulemavu Jenista Mhagama akitoa cheti kwa moja ya wahitimu Sophia Said Mwema wakati wa mkutano mkuu wa kwanza wa wanawake katika uongozi kwa mwaka 2018 uliombatanisha mahafali ya pili ya programu ya mwanamke wa wakati ujao (Female Future Programme)

Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira ma Wwtu wenye Ulemavu Jenista Mhagama akiwa katika picha ya pamoja na Sekretarieti ya Chama cha Waajiri Nchini (ATE)  mkutano mkuu wa kwanza wa wanawake katika uongozi kwa mwaka 2018 uliombatanisha mahafali ya pili ya programu ya mwanamke wa wakati ujao (Female Future Programme).


Wadau wakiwa wanaendelea na mkutano mkuu wa kwanza wa wanawake katika uongozi kwa mwaka 2018 uliombatanisha mahafali ya pili ya programu ya mwanamke wa wakati ujao (Female Future Programme)

No comments: