Kaimu
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Moshi,
Mhe. Kippi Warioba, Naibu Meya wa Manispaa ya Mji wa Moshi, Mhe. Jombo
Koyi, (watatu kushoto), na Mbunge wa Viti Maalum (Vyuo Vikuu), Mhe.
Esther Mmasi. (wane kushoto), wakiwa wamebeba miche ya miti na baadhi ya
wafanyakazi wa TANESCO Mkoa wa Kilimanjaro wakiongozwa na Meneja wao
Mhandisi Mahawa Mkaka (wasita kushoto), wakati wa zoezi la upandaji miti
Mkoani humo leo Oktoba 14, 2018
NA
SAMIA CHANDE, KILIMANJARO
SHIRIKA
la Umeme Tanzania (TANESCO) limeungana na Watanzania katika kuadhimisha
kumbukumbu ya miaka 19 ya kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Julius
Kambarage Nyerere kwa kupanda miti elfu kumi (10,000) mkoani
Kilimanjaro.
Sambamba
na upandaji huo wa miti, TANESCO pia imetoa elimu ya uhifadhi wa
mazingira ikiwa ni pamoja na kutunza miundombinu ya Shirika hilo ambayo
imekuwa ikiathiriwa mara kwa mara na Miti inayopandwa jirani na
miundombinu ya umeme.
Kampeni hiyo ya upandaji miti ilizinduliwa rasmi leo Oktoba 14, 2018.na Kaimu
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Kippi Warioba ambaye pia ni Mkuu wa
Wilaya ya Moshi katika shule ya Msingi Muungano katika Manispaa ya Mji
wa Moshi.
Akizungumza
katika uzinduzi wa kampeni hiyo ya kupanda miti, Mhe.Warioba
aliipongeza TANESCO kwa jitihada zake za dhati za kuungana na wananchi
wa Mkoa wa Kilimanjaro katika kutunza mazingira kwa kupanda miti katika
wilaya za Moshi, Rombo, Same, Mwanga, Hai na Siha lakini pia kuelimisha
wananchi umuhimu wa kutunza mazingira kwa kupanda miti.
Aidha
Kaimu Mkuu huyo wa Mkoa, aliitaka TANESCO kuendelea kutoa elimu ya
upandaji miti ili wananchi waelewe maeneo sahihi ya kupanda miti bila
kuathiri miundombinu ya umeme.
“Ni
wajibu wa kila mwananchi kujenga utamaduni wa kutunza mazingira, kwa
kupanda miti hususan ya matunda, kwani utafaidi kivutli, matunda na
wakati huo huo unakuwa umetunza mazingira.” Aliasa Mhe. Kipi Warioba.
Kwa
upande wake Menja wa TANESCO Mkoa wa Kilimanjaro. Mhandisi Mahawa Mkaka
akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO Dkt. Tito
Mwinuka alisema kuwa zoezi hilo linalengo la kuelimisha wananchi maeneo
sahihi ya kupanda miti ambayo hayaingiliani na miundombinu ya umeme ili
kuepusha madhara mbalimbali kama vile ajali za umeme na upotevu wa
umeme pia na uhifadhi wa mazingira.
Mhandisi
Mkaka alisema TANESCO ina misongo mbalimbali ya umeme hivyo wananchi
wanapaswa kuzingatia sheria inayotaka shughuli za
kijamii ikiwemo upandaji wa miti zifanyike umbali wa mita mbili na nusu
kutoka kwenye miundombinu ya umeme hii itapunguzi tatizo la kukatika kwa
umeme mara kwa mara.
Zoezi
hil la upandaji miti lilifanywa na wafanyakazi wa TANESCO Mkoani
Kilimanjaro na kuhudhuriwa na Mbunge wa viti maalum Bi. Ester Mmasi anae
wakilisha Vyuo Vikuu na Naibu Meya Manispa ya Moshi Mhe. Jomba Koyi.
TANESSCO
inategemea kutekeleza zoezi hili la upandaji miti nchi zima ili
kuhakikisha jamii inapata elimu ya jinsi ya upandaji miti na pia
utunzaji wa miundombinu ya umeme, alisema Mhandisi Mkaka kwa niaba ya
Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO Dkt. Tito Mwinuka.
Kaimu
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Moshi,
Mhe. Kippi Warioba, akifanya maandalizi ya kupanda mti leo Oktoba 14,
2018
Meneja
wa TANESCO Mkoani Kilimanjaro Mhandisi Mahawa Mkaka akimkabidhi zawadi
ya mche wa Matunda Kaimu Mkuu wa Mkoa Kippi Warioba
Wafanyakazi wa TANESCO Mkoa wa Kilimanjaro, wakipanda miti leo Oktoba 14, 2018.
Mbunge wa Viti Maalum (Vyuo Vikuu), Mhe. Esther Mmasi, akimwagilia mti alioupanda.
Meneja wa TANESCO Mkoa wa Kilimanjaro, Mhandisi Mahawa Mkaka, akizungumza wakati wa tukio hilo.
Wafanyakazi wa TANESCO Mkoa wa Kilimanjaro, wakipanda miti leo Oktoba 14, 2018.
Mbunge wa Viti Maalum (Vyuo Vikuu), Mhe. Esther Mmasi, akimwagilia mti alioupanda.
Meneja wa TANESCO Mkoa wa Kilimanjaro, Mhandisi Mahawa Mkaka, akizungumza wakati wa tukio hilo.
No comments:
Post a Comment