Sunday, October 14, 2018

KAMPUNI YA MZALENDO KUJENGA KIWANDA CHA PIKIPIKI ARUSHA

Na Ahmed Mahmoud Arusha

Kampuni ya kichina ya Kutengeneza vifaa vya pikipiki ililyopo Njiro Jijini Arusha hapa Nchini kimeahidi kuanza kutengeneza Pikipiki ifikapo mwaka 2020.

Akiongea wakati alipotembelewa na Kamati ya siasa ya chama cha Mapinduzi kata ya Themi Mkurugenzi wa kiwanda hicho,Zhang You Chin amesema mapango huo upo mbioni kukamilika kutokana na umuhimu wa mahitaji hapa nchini baada ya kuonesha mafanikio makubwa katika utengenezaji wa vifaa vya pikipiki hususani kofia Ngumu.
Amesema kiwanda hicho tangu kianzishwe mapema mwaka huu,kimeweza kuajiri Wafanyakazi wapatao 60 na wanatarajia kuongeza uzalishaji na kufikia ajira za Wafanyakazi 200 pindi watakapofunga machine za kuunda pikipiki. Tunatengeneza kofia ngumu ambazo hazipasuki hata ikidondoka na tunauza nchi mbalimbali za Afrika zikitoka nchini Tanzania”Amesema
Amesema hadi sasa kiwanda hicho kinazalisha kofia ngumu za pikipiki zipatazo 5000 kwa Siku na vifaa vingine vya pikipiki na baada ya miaka mitatu wanatarajia kutengeneza pikipiki zitakazouzwa jwa bei nafuu na hivyo kupunguza gharama ya kuagiza pikipiki kutoka Nje ya nchi.
Awali mwenyekiti wa ccm kata ya Themi,Thomas Munis amekipongeza kiwanda hicho kwa kuanza kutengeneza kofia ngumu ambazo hazipasuki zitakazosaidia kupunguza vifo kwa ajali za pikipiki

No comments: