Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza (katikati) akipata maelezo kutoka kwa Mjasiriamali wa sanaa za uchongaji, Ras Jeshi Beku alipotembelea banda la Msanii huyo wakati wa kufunga tamasha la 37 la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo jana Jumamosi Oktoba 27, 2018, Wilayani Bagamoyo, Mkoa wa Pwani.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza (katikati) akipata maelezo kutoka kwa Mjasiriamali wa sanaa za uchongaji, Ras Jeshi Beku alipotembelea banda la Msanii huyo wakati wa kufunga tamasha la 37 la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo jana Jumamosi Oktoba 27, 2018, Wilayani Bagamoyo, Mkoa wa Pwani.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza (kulia), akitazama kikoi kilitengenezwa na Msajiriamali Esther Mwita alipotembelea banda la Msanii huyo wakati wa kufunga tamasha la 37 la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo jana Jumamosi Oktoba 27, 2018, Wilayani Bagamoyo, Mkoa wa Pwani.
Naibu Waziri wa Habari, Utanmaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza akitazama moja shati lilitengtenezwa na Mjasiriamali Monica Matemba alipotembelea banda la Mjasiriamali huyo wakati wa kufunga tamasha la 37 la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo jana Jumamosi Oktoba 27, 2018, Wilayani Bagamoyo, Mkoa wa Pwani.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza akitazama chungu kilitengenezwa na mmoja wa Wajasiariamali alipotembelea banda la Mjasiriamali huyo wakati wa kufunga tamasha la 37 la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo jana Jumamosi Oktoba 27, 2018, Wilayani Bagamoyo, Mkoa wa Pwani.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza akitazama chungu kilitengenezwa na mmoja wa Wajasiariamali alipotembelea banda la Mjasiriamali huyo wakati wa kufunga tamasha la 37 la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo jana Jumamosi Oktoba 27, 2018, Wilayani Bagamoyo, Mkoa wa Pwani.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza akijaribu moja ya vidani vilivyotokana na kazi za wajasiriamali wasanii mara baada ya kutembelea alipotembelea banda la Mjasiriamali wakati wa kufunga tamasha la 37 la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo jana Jumamosi Oktoba 27, 2018, Wilayani Bagamoyo, Mkoa wa Pwani.
Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania, Joyce Fisoo, Mwenyekiti wa Bodi wa Taasisi hiyo Prof. Frowin Paul Nyoni na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano katika Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Geofrey Tengeneza, wakibadilishana mawazo wakati wa kufungwa kwa Tamsha la 37 la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo jana Jumamosi Oktoba 27, 2018, Wilayani Bagamoyo, Mkoa wa Pwani.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza, akisoma moja ya vitabu wakati alipotembelea moja wa mabanda ya wajasiriamali wakati wa kufungwa kwa Tamasha la 37 la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo jana Jumamosi Oktoba 27, 2018, Wilayani Bagamoyo, Mkoa wa Pwani.
Msanii wa sanaa ya uchongaji, Amiri Amasha akitoa ufafanuzi kwa Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza wakati alipotembelea mabanda mbalimbali ya wasanii na wajasiriamali katika kilele cha Tamsha la 37 la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo jana Jumamosi Oktoba 27, 2018, Wilayani Bagamoyo, Mkoa wa Pwani.
Mkuu wa Magofu ya Kaole- Bagamoyo Mkoani Pwani, Siyawezi Hungo (katikati) akitoa ufafanuzi kwa Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza wakati alipotembelea Banda la Taasisi hiyo katika kilele cha Tamasha la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo jana Jumamosi Oktoba 27, 2018, Wilayani Bagamoyo, Mkoa wa Pwani.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kutembelea Banda la Bodi ya Filamu na Michezo ya Kuigiza Nchini wakati wa kilele cha Tamasha la 37 la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo jana Jumamosi Oktoba 27, 2018, Wilayani Bagamoyo, Mkoa wa Pwani. Kulia kwakeni Katibu Mtendaji wa Bodi hiyo, Joyce Fisoo na Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Prof. Frowin Paul Nyoni.
Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania, Joyce Fisoo akitoa ufafanuzi kuhusu matumizi ya vitambulisho rasmi vya Bodi hiyo kwa watayarishaji na waandajii wa filamu mbalimbali nchini kwa Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza wakati alipotembelea banda la Bodi hiyo katika kilele cha Tamasha la 37 la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo jana Oktoba 27, 2018, Wilayani Bagamoyo, Mkoa wa Pwani.
Kikundi cha Ngoma cha Bagamoyo Players kinachoongozwa na Wakufunzi wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBA) wakitoa burudani ya ngoma kwa wageni mbalimbali waliohudhuria kilele cha Tamasha la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo Pwani jana Jumamosi Oktoba 27, 2018, Wilayani Bagamoyo, Mkoa wa Pwani.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza akihutubia wageni mbalimbali waliohudhuria kilele cha Tamasha la 37 la Sanaa nas Utamaduni Bagamoyo jana Jumamosi Oktoba 27, 2018, Wilayani Bagamoyo, Mkoa wa Pwani.
(PICHA NA MAELEZO)
…………………………………
Na Mwandishi Wetu,MAELEZO
Bagamoyo
NAIBU Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza amesema Serikali itaendelea kuwajengea uwezo, umahiri na ubunifu wasanii wa Tanzania kupitia Mradi wa Utambuzi wa Wasanii wa Sanaa za Ufundi (TASIP) ili kukuza soko la tasnia hiyo katika ngazi ya kitaifa na kimataifa.
Akifunga Tamasha la 37 la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo, Wilayani Bagamoyo, Mkoani Pwani jana (Jumamosi Oktoba 27, 2018), Shonza alisema malengo ya Serikali ya Awamu ya Tano ni kuhakikisha kuwa tasnia ya sanaa nchini inapiga hatua kubwa zaidi na kuwafanya wasanii kunufaika na kazi zao.
Aliongeza kwa kuzingatia kuwa Wizara yake inasimamia na kutekeleza sera ya sanaa nchini, Serikali itahakikisha kuwa kuipitia mradi wa TASIP unawafikia na kuwatambua wasanii wote nchini na kuwawezesha kuwa na utambulisho rasmi utawaozesha kupata mitaji na mikopo ya kuendesha shughuli zao.
“Mwaka jana nilizindua mradi huu wa TASIP na mwaka huu tumeanza kushuhudia mafanikio makubwa kupitia program hii, kwa kuwa wapo baadhi ya wasanii waliotambuliwa na kusajiliwa na wameanza kupata mikopo kutoka mabenki hatua inayowezesha kupata kutatua baadhi ya changamoto katika kuendesha shughuli zao” alisema Shonza.
Naibu Waziri Shonza alisema Serikali itaendelea kutoa msukumo kwa wafadhili mbalimbali kuweza kuunga mkono Tamasha la Sanaa na Utamduni Bagamoyo linalofanyika kila mwaka nchini, kwa kuwa Tamasha hilo linawezesha wasanii wa Tanzania wanapata uzoefu wa masuala mbalimbali kutoka kwa wasanii wenzao wa mataifa mbalimbali ya nje na hivyo kuweza kuongeza ubunifu katika kazi zao.
Kwa mujibu wa Shonza alisema kwa kutambua umuhimu wa Tamasha hilo, Serikali itaendelea kuijengea Tasasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBA) kwa ili kuwa na uwezo kuweza kuzalisha wasanii na wakufunzi wenye ubora katika ngazi ya kitaifa na kimataifa kwani Taasisi hiyo imekuwa kiungo muhimu cha uzalishaji wa wasanii katika mataifa mbalimbali ya kigeni.
No comments:
Post a Comment