Wednesday, October 10, 2018

SERIKALI YAPIGA MARUFUKU KWA MADAKTARI KUWAANDIKIA WAGONJWA DAWA KWA MAJINA YA KIBIASHARA


Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile akitoa hotuba yake ya ufunguzi wa Kongamano la Wadau wa Mnyororo wa Ugavi wa Dawa- Tanzania (Tanzania Health Supply Chain Summit 2018) linalofanyika kwa siku mbili jijini Dar es Salaam. Picha na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.Mwenyekiti wa Kongamano la Wadau wa Mnyororo wa Ugavi wa Dawa- Tanzania (Tanzania Health Supply Chain Summit 2018) Bw. Mavere Tukai akizungumza machache wakati akitoa neno la utangulizi katika Ufunguzi wa Kongamano la Wadau wa Mnyororo wa Ugavi wa Dawa -Tanzania linalofanyika kwa siku mbili jijini Dar es Salaam. 
Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI, Dkt. Zainabu Chaula akitoa shukrani zake za pekee kwa waandaaji wa Kongamano la Wadau wa Mnyororo wa Ugavi wa Dawa- Tanzania (Tanzania Health Supply Chain Summit 2018) linalofanyika kwa siku mbili jijini Dar es Salaam. Kulia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile na Mwenyekiti wa Kongamano la Wadau wa Mnyororo wa Ugavi wa Dawa- Tanzania (Tanzania Health Supply Chain Summit 2018) Bw. Mavere Tukai. 


Washiriki wa Kongamano la Wadau wa Mnyororo wa Ugavi wa Dawa- Tanzania (Tanzania Health Supply Chain Summit 2018) 
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile (katikati) akizungumza na wanahabari mara baada ya kufungua Kongamano la Wadau wa Mnyororo wa Ugavi wa Dawa- Tanzania (Tanzania Health Supply Chain Summit 2018) linalofanyika kwa siku mbili jijini Dar es Salaam. 
Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD) Bwana Laurean Bwanakunu (kulia) akielezea jinsi mfumo wao wa utoaji wa Dawa. 
 
Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG. 
 
Serikali imepiga marufuku kwa madaktari kuwaandikia wagonjwa dawa kwa majina ya kibiashara badala yake watumie majina ya asili (Generic name). Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile wakati akifungua mkutano wa Kongamano la Wadau wa Mnyororo wa Ugavi wa Dawa- Tanzania (Tanzania Health Supply Chain Summit 2018) linalofanyika kwa siku mbili jijini Dar es Salaam. 
 
Dkt. Ndugulile amesema imefika wakati serikali imebidi kutoa tamko hilo kwasababu Madaktari wengi wamekuwa wakikiuka miongozo wa utoaji matibabu uliotolewa na wizara ya afya. "Katika mfumo wa utoaji wa huduma za afya, tunamtaka daktari aandike kwa jina la asili ili mfamasia akatafsiri aina ile ya dawa tulizonazo kwenye akiba yetu za dawa tulizonazo, ubora wa dawa za Tanzania ni za kiwango cha juu kabisa, tuwaambie wa Tanzania waache zile dhana potofu akisikia zile zinazotoka," amesema. 
 
Amesema kinachotokea kwasasa katika hospitali nyingi unakuta madawa ni mengi ila hayatumiki wanaishia kwenda kununua nje wakati angeandika kwa jina halisi angepatiwa. Amewataka wafamasia na waganga wafawidhi wa hospitali zote nchini kuhakikisha wanatoa orodha ya dawa zote walizonazo kila mwanzo wa wiki ili kuwawezesha watoa dawa kufahamu dawa walizonazo ili kuondoa adha kwa wananchi kuandikiwa dawa ambazo hazipo.
 
 Nae Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI, Dkt. Zainabu Chaula amesema kuwa ni vyema madaktari wakazingatia maagizo yale yote ambayo yamekuwa wakitolewa na viongozi.  Kwa upande wa Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD) Bwana Laurean Bwanakunu amesema kuwa wao wamejipanga na wanaakiba ya kutosha ya dawa hivyo ni vyema wahusika kufuata utaratibu ili wanunue na wapelekewe kwa wakati muafaka. 
 
Kongamano la Wadau wa Mnyororo wa Ugavi wa Dawa- Tanzania (Tanzania Health Supply Chain Summit 2018) linawakutanisha wadau wote wa masuala ya afya kutoka nchi nzima.

No comments: