Tuesday, October 9, 2018

PROF.MBARAWA : SERIKALI IMEJIPANGA KUMALIZA SHIDA YA MAJI 2020

Serikali imejipanga kuhakikisha miradi ya maji hapa nchini inatekelezwa kwa kasi kubwa kwa majiji unafikia asilimia 95 ambapo miji ya wilaya asilimia 90 na vijijini kwa asilimia 85 ifikapo mwaka 2020 ambapo kwa jiji la Arusha inatekeleza mradi mkubwa wa maji utakaozalisha lita million 200 kwa siku kwa gharama ya billion 520.

Aidha Serikali imepanga kutekeleza Mradi mkubwa wa maji hapa nchini utakogharimu kiasi cha Trilion 1.1 sawa na dola za kimarekani million 500 kwa watanzania wamesubiria maji hivyo watakaopata nafasi ya kusimamia mradi huu kuutekeza kwa ufanisi na kwa wakati.

Akizungumza wakati wa ziara ya kutembelea visima vya maji katika kijiji cha Levolosi kata ya Kimnyaki wilaya ya Arusha dc na kutiliana saini Waziri wa maji na umwagiliaji Prof.Makame Mbarawa amesema kuwa serikali itaendelea kuhakikisha miradi hiyo inaondoa adhaa ya maji kwa watanzania

Amesema kuwa jiji la Arusha kwa sasa linazalisha maji lita million 45 kwa siku wakati mahitaji yanayotosheleza kwa siku ni lita million 94 ndio maana serikali ikaliona hilo na ikaandaa mradi mkubwa uakapo kamilika utazalisha lita million 200 kwa siku ambao utaondoa tatizo la maji kwa jiji la Arusha na kuwa historia.

“Jiji la Arusha kwa sasa kuna upungufu mkubwa wa maji ambapo serikali inakuja na mradi huu mkubwa kwa kuchimba visima 56 tunajenga mfumo wa kusafisha maji na mfumo wa kusambaza maji na mfumo wa kusafisha maji taka na wakandarasi wapo kazini”alisema Prof.Mbarawa.

Kwa Upande wake Mkurugenzi wa Mamlaka ya maji (AUWSA) Mhandisi Lucy Koya Alisema kuwa Wakandarasi wanaendelea na kazi ikiwamo utandazaji wa mabomba ya maji taka na kuondoa uvujaji wa maji machafu barabarani kwa kuondoa mabomba ya zamani na kutandika mapya makubwa kutoka na mahitaji ya sasa.

Amesema kuwa mamlaka hiyo imeongezewa eneo la kata 8 za wilaya ya Arusha dc na tunaishukuru serikali yetu kwa kuona changamoto ya upungufu wa maji na kutuletea mradi huu mkubwa wa billion takribani 520 mkopo nafuu kutoka benki ya maendeleo ya Afrika.

Nae Mwenyekiti wa Bodi ya Auwsa Dkt.Richard Masika alisema kuwa bodi yao imejipanga kuhakikisha miradi hiyo inajengwa kwa ufanisi na kwa viwango ndio maana wamepeleka watumishi wa sekta ya utawala kwenye mafunzo ya kusimamia miradi mikubwa kuweza kujifunza ili teknojia hii ibaki nchini na kuboresha weledi ili kupitia mafunzo hayo kujua thamani ya mradi na kuondoa gharama.

Amesema kuwa mafunzo hayo yatasaidia kuongeza na kusimamia mradi huu kwa ufanisi na weledi na hatutarajii mradi huu ukashindwa kusimamiwa kwa muda uliopangwa na chini ya ubora ila najua utasimamiwa kwa kuangalia ubora na thamani ya mradi na kujengwa kwa muda uliopangwa .

No comments: