Thursday, October 4, 2018

NDOA ZA UTOTONI ZAENDELEA KUWA KIKWAZO CHA MTOTO WA KIKE KUFIKIA MALENGO

Na Chalila Kibuda, Golobu ya Ja Jamii
NDOA  za utotoni zimeendelea kuwa kikwazo kwa maendeleo ya mtoto wa kike ambapo takiwmu za hali ya watu na afya nchini kwa mwaka 2015/2016 zinaonyesha asilimia 36 ya wanawake umri wa  miaka 25-49 wamepata watoto kabla ya kufikisha umri wa miaka 18.
Hayo aliyasema  Mchumi na Mratibu wa Mpango kazi wa Kitaifa wa kutokomeza Vitendo vya Ukatili dhidi ya Wanawake na watoto kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Seto Ojwando katika mdahalo wa Wadau uliofanyika katika Chuo cha Ustawi Jamii jijini Dar es Salaam.
Amesema tafiti za afya na uzazi na viashiria vya malaria  TDHS 2015/2016  zinaonyesha kuwa mwanamke mmoja kati ya 10 wenye umri wa miaka 15 hadi 49 wamekeketwa  huku mikoa ambayo inaongoza katika ukeketaji huo ni Manyara  asilimia 58, Dodoma asilimia 47, Arusha 41, Mara asilimia 32 pamoja na Singida asilimia 41.
Ojwando amesema katika tafiti hiyo ya TDHS ya 2015, 2016 Mikoa  inayoongoza kwa mimba za utotoni ni Katavi asilimia 45,Tabora asilimia 43, Dodoma asilimia 39, Mara asilimia 37 pamoja na Singida asilimia 34.
Amesema kuwa nia ya kukuatana na wadau pamoja na wasomi katika Chuo cha ustawi wa jamii ni sehemu ya utekelezaji wa mapango kazi wa Taifa wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto  na mpango wa vietndo vya ukatili dhidi ya watoto ulianza 2017  ikiwa ni lengo kupunguza vitendo vya aina zote ukatili dhidi ya mwanamke na watoto kwa asilimia 50 ifikapo mwaka 2022.
Nae Kaimu Mkuu wa Taasisi ya Ustawi wa Jamii Dkt.Zena Mabeyo amesema kuwa kama wazalishaji wa wataalam wanawajibu kutoa rasilimali watu  itakayotumika kwa ajili ya kustawisha jamii katika kuondokana na mimba za utotoni, ukeketaji pamoja na vitendo vya aina yeyote vya ukatili.
Amesema kuwa serikali imekuwa mstari wa mbele wa kupigania masilahi ya watoto wa kike hivyo jamii inahitaji kuchukua hatua katika kuwalinda watoto wa kike kufikia malengo yao.
Mtoa mada katika mdahalo huo Mhadhili wa Chuo cha Ustawi wa Jamii Leah Omary  amesema kuwa watoto wa kike wanahitaji kupewa ulinzi pamoja na wazazi kukaa na familia zao.
Maazimio ya mdahalo huo yatapelewa katika kilele cha maashimisho ya siku ya kimataifa ta ya mtoto wa kike yatakyofanyika Oktoba 11 jijini Dar es Salaam.  
 Kaimu Mkuu wa Chuo cha Ustawi wa Jamii Dkt. Zena Mabeyo akifungua madahalo wa kitaifa wa kutokomeza ukeketaji ,Mimba na Ndoa za Utotoni uliofanyika katika Chuo hicho jijini Dar es Salaam.
 Mhadhili wa Chuo cha Ustawi wa Jamii, Leah Omary akitoa mada katika madahalo wa kitaifa wa kutokomeza ukeketaji ,Mimba na Ndoa za Utotoni uliofanyika katika Chuo hicho jijini Dar es Salaam.
 Mchumi na Mratibu wa Mpango kazi wa Kitaifa wa kutokomeza Vitendo vya Ukatili dhidi ya Wanawake na watoto kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Seto Ojwando akizungumza katika mdahalo wa kuhusiana na seriakli kuchukua hatua mimba za utotoni, ndoa z utotoni pamoja na ukeketaji
 Mhadhili wa Chuo cha Ustawi wa Jamii, Zachayo Shigongo akitoa maada kusiana na malezi ya watoto katika madahalo wa kitaifa wa kutokomeza ukeketaji ,Mimba na Ndoa za Utotoni uliofanyika katika Chuo hicho jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya wadau katika mdahalo huo wa kujadili na kutokomeza ukeketaji ,Mimba na Ndoa za Utotoni uliofanyika katika Chuo hicho jijini Dar es Salaam.

No comments: