Mbunge
wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Azza Hilal Hamad (CCM)
amekabidhi msaada wa Vifaa tiba vyenye thamani ya shilingi milioni 36.5
kwa ajili ya vituo vya afya na zahanati sita zilizopo katika halmashauri
ya wilaya ya Ushetu,Msalala na Kahama Mji wilayani Kahama mkoani
Shinyanga.
Mheshimiwa
Azza amekabidhi vifaa tiba hivyo leo Jumanne Oktoba 16,2018 kwa Mkuu wa
Wilaya ya Kahama,Anamringi Macha wakati wa Kikao cha Baraza la UWT
wilaya ya Kahama uliofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri ya Mji Kahama.
Vifaa
tiba hivyo ni pamoja na shuka 100,mashine za kupima damu,wingi wa
damu,sukari,joto,mapigo ya moyo na vifaa vya kusaidia kujifungua kwa
akina mama ambavyo kupatikana kwake kumetokana na jitihada za mbunge
huyo kuhakikisha vifo vya mama na mtoto vinapungua mkoani Shinyanga.
Awali akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa tiba hivyo,Mheshimiwa Azza Hilal alisema kupitia Kampeni yake ya ‘Afya Yangu Mtaji Wangu’
na kuwajali akina mama aliamua kutafuta wadau kwa ajili ya kusaidia
kumaliza changamoto ya uhaba wa vifaa tiba katika vituo vya afya na
zahanati.
“Nawashukuru
sana Bahari Pharmacy Ltd na Brett &Beileys kwa kunishika mkono
na kuchangia kupatikana kwa vifaa hivi ambavyo leo navikabidhi ili
vikatumike kwenye zahanati na vituo vya afya kwani hatutaki kuona vifo
vya mama na mtoto”,alieleza Azza.
“Serikali
ya awamu ya tano inayoongozwa na Jemedari,Dkt. John Pombe Magufuli
imedhamiria kuboresha huduma za afya,na tutaendelea kushirikana ili
kuhakikisha wananchi wanakuwa na afya bora ili washikiriki katika
shughuli za uchumi”,aliongeza.
Alivitaja
vituo vya afya vitakavyonufaika na msaada huo kuwa ni
Mwendakulima,Mbika na Lunguya na zanahati ambazo ni Ngogwe,Kisuke na
Bulige.
Akipokea
vifaa tiba,Mkuu wa wilaya ya Kahama Anamringi Macha alimshukuru mbunge
huyo kwa msaada huo na kubainisha kuwa ameunga mkono kwa vitendo ilani
ya CCM na juhudi zinazofanywa na Rais Magufuli katika kuboresha sekta ya
afya.
“Nikupongeze
sana kwani umetumia cheo chako kwa faida ya wote badala ya kujinufaisha
wewe mwenyewe,lakini nikushukuru pia kwa kuendelea kujitoa kwa hali na
mali katika kukitumikia chama na wananchi,umekuwa kiungo mzuri sana”,alisema Macha.
Kwa
Upande wake Mbunge wa Jimbo la Ushetu,Mheshimiwa Elias Kwandikwa ambaye
ni Naibu Waziri wa Ujenzi aliahidi kumuunga mkono mheshimiwa Azza kwa
kutoa msaada wa vifaa tiba katika vituo vitatu vya afya wilayani Kahama.
Mbunge
wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Azza Hilal Hamad (CCM)
akizungumza wakati akikabidhi vifaa tiba vyenye thamani ya shilingi
milioni 36.5 kwa ajili ya zanahati na vituo vya afya wilayani Kahama leo
katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji Kahama.Kushoto ni Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Kahama,Telephora Saria,kulia ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kahama Thomas Myonga. - Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Vifaa tiba vyenye thamani ya shilingi milioni 36.5 kwa ajili ya zanahati na vituo vya afya wilayani Kahama vilivyotolewa na Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Azza Hilal Hamad (CCM) kwa kushirikiana na wadau wake Bahari Pharmacy Ltd na Brett &Beileys.
Kulia ni Mkuu wa wilaya ya Kahama Anamringi Macha(aliyevaa miwani) akiangalia vifaa tiba vilivyotolewa na Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Azza Hilal Hamad.
Kulia ni Mkuu wa wilaya ya Kahama Anamringi Macha akimshukuru Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Azza Hilal Hamad kwa kuleta vifaa tiba wilayani Kahama. Kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Ushetu,Mheshimiwa Elias Kwandikwa ambaye ni Naibu Waziri wa Ujenzi.
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Azza Hilal Hamad akikabidhi vifaa tiba kwa Mkuu wa wilaya ya Kahama,Anamringi Macha.
Mbunge
wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Azza Hilal Hamad akikabidhi
shuka ikiwa ni sehemu ya shuka 100 alizotoa kwa ajili ya vituo vya afya
na zahanati wilayani Kahama.
Wa
pili kulia ni Mkuu wa wilaya ya Kahama Anamringi Macha akiwa
ameshikilia boksi lenye mashine ya kupimia sukari mwilini. Wa kwanza
kulia ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kahama Thomas Myonga.Wa kwanza
kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Ushetu,Mheshimiwa Elias Kwandikwa ambaye ni Naibu Waziri wa Ujenzi akifuatiwa na Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Azza Hilal Hamad akiwa ameshikiliwa vifaa tiba.
Mwakilishi
wa Mganga mkuu wa Halmashauri ya wilaya Ushetu,Dk. Joseph Mugizi
akisoma maandishi katika mashine/kifaa cha kupimia sukari baada ya
kukabidhiwa na Mkuu wa wilaya ya Kahama,Anamringi Macha.
Kushoto ni Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Mji Kahama,Dk. David Lucas akipokea mashine/kifaa cha kupimia wingi wa damu.
Mwakilishi wa Mganga mkuu wa Halmashauri ya wilaya Msalala,Dk. Martine Dotto akipokea kifaa cha kupimia mapigo ya moyo.
Mganga
Mkuu wa Halmashauri ya Mji Kahama,Dk. David Lucas akiwa ameshikilia
kifaa cha vifaa vya kujifungulia kwa akina mama.Katikati ni Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Azza Hilal Hamad akifafanua kuhusu vifaa vya kujifungulia.
Mbunge
wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Azza Hilal Hamad akiwa
katika picha ya pamoja na Wajumbe wa UWT halmashauri ya wilaya ya Ushetu
Mbunge
wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Azza Hilal Hamad akiwa
katika picha ya pamoja na Wajumbe wa UWT halmashauri ya wilaya ya Kahama
Mji.
Mbunge
wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Azza Hilal Hamad akiwa
katika picha ya pamoja na Wajumbe wa UWT halmashauri ya wilaya ya
Msalala.
Mkuu wa wilaya ya Kahama Anamringi Macha akizungumza baada ya kupokea vifaa tiba vilivyotolewa na Mbunge
wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Azza Hilal Hamad.Wa kwanza
kulia ni Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Kahama,Telephora Saria.
Mbunge
wa Jimbo la Ushetu,Mheshimiwa Elias Kwandikwa ambaye ni Naibu Waziri wa
Ujenzi akizungumza wakati Mheshimiwa Azza Hilal akikabidhi vifaa tiba.Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
No comments:
Post a Comment