Friday, October 26, 2018

MBIO ZA NAMTUMBO SELOUS MARATHON ZAZINDULIWA JIJINI DAR,KUFANYIKA NOVEMBA 10, 2018

Kwa mara nyingine tena zile mbio ambazo zimekuwa zikisubiriwa kwa hamu na shauku kubwa na wakazi wa mkoa wa Ruvuma na vitongoji vyake hususan wilaya ya Namtumbo maarufu kama Namtumbo Selous Marathon zimewadia ambapo tarehe rasmi ya kufanyika kwa mbio hizo imetangazwa kuwa tarehe10 Novemba2018. 

Akizungumza na waandishi wa habari katika hafla ya uzinduzi wa mbio hizo jijini Dar EsSalaam, Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo Mh. Sophia Kizigo amesema kuwa mbio hizo zilizoanza rasmi mwaka jana chini ya udhamini wa kampuni ya madini ya Uranium one na kampuni ya Nyuklia ya Rosatom ya Urusi zinalenga kukusanya kuchangisha fedha na vifaa vya ujenzi kwa ajili ya ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Namtumbo ambapo ujenzi wa baadhi ya majengo umekwisha anza tangu mwaka jana na kwamba unatarajiwa kuendelea tena mwaka huu. 

Nina kila sababu ya kuwashukuru sana wadhamini wa mbio hizi wenzetu Uranium One na Rosatom kwa jinsi ambavyo wamekuwa wakijitolea kuhakikisha kuwa mbio hizi sio zinafanyika lakini pia malengo yake kufanikiwa kwa kiasi kikubwa sana pia tunawashukuru wadau mbalimbali wakiwemo chama cha riadha, wafanyakazi na uongozi wote wa hospitali ya wilaya ya Namtumbo na wananchi wa Namtumbo kwa ujumla kwa michango mbalimbali. 

Naomba pia ni shukuru makampuni na wale wote waliokwisha kuchangia ujenzi wa hospitali hii ya Namtumbo. Makampuni hayo ni MMI, FB Attorney, Namis Corporate, Tanesco, BOT, ITV/Radio One, Halotel, Tulia Trust, wabunge wa mkoa wa Ruvuma, Ma DC na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma. 

Kwa upande wake kampuni Uranium One na mwakilishi wa Rosato amesema kuwa mbio hizo pamoja kulenga kuboresha miundombinu ya afya katika wilaya ya Namtumbo, mbio hizo pia zinaleta umoja na mshikamano mzuri baina ya serikali sekta binafsi na wananchi kwa ujumla huku ikihamasisha afya kwa njia ya mazoezi. 

Nao waratibu wa mbio hizo wamewataka watanzania wanaopenda michezo wajitokeze kwa wingi kushiriki katika mbio hizo za KM 21, KM 10, KM 5, na KM 2.5 ambapo walitaja njia nzuri ya kujisajili kuwa ni kutuma ujumbe kwenda runselous2018@gmail.com ambapo kuanzia miaka 16 na kuendelea watashiriki KM 21 na KM 10 lakini KM5 na 2.5 zitawahusu wazee na watoto 

Mbio hizo zinatarajiwa kudhuriawa na wakimbiaji kutoka mataifa mbalimbali kama Marekani, Japan na Urusi ambako wafanya kazi wa kampuni ya Uranium nao watakuja kushiriki mbio hizo. 

Kujisajili: kupitia ofisi ya mganga mkuu wa wilaya ya Namtumbo na barua pepe runselous2018@gmail.com

Mahala: Mbio zote zitaanzia na kuishia Hospitali ya Wilaya ya Namtumbo 
Muda: Mbio zitaanza saa 12 asubuhi 


“PAMOJA TUNAWEZA” 


Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo Mh. Sophia Mfaume Kizigo (katikati) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa Namtumbo Selous Marathon zitakazofanyika Namtumbo,Mkoani Ruvuma Novemba 10 mwaka huu.Kulia ni mwakili kutoka Mantra(Uranium One) Tanzania Mrs Khadija Pallangyo, na kushoto ni katibu wa afya wilaya ya Namtumbo.
Mwakilishi kutoka Chama cha Riadha Tanzania RT Iddi Muhunzi (kushoto) akiongea na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa Namtumbo Selous Marathon zitakazofanyika Namtumbo mkoani  Ruvuma Novemba 10 mwaka huu. Katikati ni Mkuu wa wilaya ya Namtumbo na kulia ni mwakili kutoka Mantra(Uranium One) Tanzania Mrs Khadija Pallangyo.
Mwakilishi kutoka Chama cha Riadha Tanzania RT Ombeni Zavala akiongea na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa Namtumbo Selous Marathon zitakazofanyika Namtumbo mkoani  Ruvuma Novemba 10 mwaka huu.

No comments: