Na Jumbe Ismailly SINGIDA
MCHEZAJI mmoja wa timu ya soka ya Kijiji cha Iyumbu,tarafa ya Sepuka,wilayani Ikungi,Mkoani Singida,Mussa Kikumbu (20) amepoteza maisha na wengine 38 wamejeruhiwa vibaya baada ya gari aina ya kenta walilokuwa wakisafiria kwenda kucheza mchezo wa kirafiki na timu ya Kata ta Mgungira kuacha njia na kupinduka.
Wakiongea kwa nyakati tofauti baadhi ya wachezaji na washabiki waliolazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Singida walisema ajali hiyo ilitokea Okt,07,mwaka huu saa tisa za alasiri wakati wakielekea kwenye mchezo wao wa kirafiki na timu ya kata ya Mgungira.
Mmoja wa majeruhi hao Emanueli Peter alisema waliondoka wakiwa watu 38 kwenye gari hilo na walipoanza safari askari mmoja wa kituo cha polisi Iyumbu alisema yeye hatapanda gari bali angekwenda na usafiri wake wa pikipiki.
Alifafanua majeruhi huyo alaiyelazwa katika wodi namba tatu katika Hospitali hiyo kwamba askari huyo alikuwa nyuma ya garai walilopanda akiendesha huku akionesha kila dalili za kuwa amekunywa kilevi huku dereva naye akiendesha mwendo kasi huku naye akiwa amelwa.
Kwa mujibu wa Peter inasemekana awali askari huyo alikuwa akitaka kumpita dereva wa gari ili aweze kutangulia lakini ilishindikana lakini baada ya muda alianza tena kuomba nafasi ili atangulie na alipopishwa ndipo ghafla alianguka chini.
Aidha majeruhi huyo aliweka bayana pia kwamba baada ya askari huyo kuanguka chini ndipo dereva wa gari walilopanda aliamua kumkwepaa ili asimkanyage na ndipo alipoingia kwenye korongo lililokuwa nje ya barabara na gari hilo kuanguka na kusababisha kifo cha mtu mmoja kati ya watu 39 waliokuwepo kwenye gari hilo.
‘Wakati dereva wa gari aina ya kenta alipokuwa akiendesha alikuwa amelewa na hata askari aliyekuwa anaendesha pikipiki alikuwa pia amelewa “alisisitiza majeruhi huyo wa ajali ya wachezaji wa timu ya mpira.
Naye Fatuma Jishimu alisema walipofika katika kona ya barabara katika Kijiji cha Makungu ndipo alipotokea askari aliyekuwa akilifuata gari nyuma huku akiashiria kuligonga ndipo dereva wa gari aliamua kumpisha ili asije akalipamia na kusababisha watu 38 kuumia.
Kwa upande wake Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa wa Singida,Dk.Ng’hungu Kuzenza alitithibitisha kwamba okt,07,mwaka huu saa nne usiku walipokea majeruhi 12 wa ajali hiyo iliyotokea katika Kijiji cha Iyumbu ambapo kati yao wanawake walikuwa wawili,mtoto wa mmoja wa kike mwenye umri wa miaka miwili na nusu na tisa walikuwa wanaume.
Kwa mujibu wa Mganga Mfawidhi huyo waliolazwa katika Hospitali hiyo ni pamoja na Kidatu Ndika(42),Emanuel Peter (28),Ramadhani Mohamed (22),Hamisi Paulo (18),Mariamu Ramadhani(24) na Paulo Charles(17) wote ni wakazi wa Kijiji cha Iyumbu.
Wengine ni Fatuma Jishimu (19),Joseph Abel(21),Alhaji Mohamed (14),Hussein Rajabu (18),Margreth Sawa (40) na Kishiwa Paulo(21) wote pia ni wakazi wa Kijiji cha Iyumbu.Hata hivyo Dk.Kuzenza aliweka wazi kwamba hali za majeruhi wote ni nzuri na kuzitajata sehemu walizopata amajeraha madogomadogo na kuweza kushonwa,vidonda kichwani,kuumia mikono na mmoja alivunjika mguu na ameshahudumiwa.
Akiongea kwa njia ya simu kutoka Kijiji cha Mgungira,Mganga Mfawidhi wa zahanati ya Kata hiyo,Abdala Salumu Abdala alikiri kupokea majeruhi 21 ambao ni Hussein Mohamed(21).Bush Mohi(24),Benja Chagu(24),Bahati Hamisi(27),Michael Shija(23) na Mlekwa Andea(18) wote ni wakati wa Kijiji cha Iyumbu.
Wengine ni Saidi Ramadhani (22),Kurwa Paulo(26),Robert Masanja(20),Jumanne Paulo(28),Shani Jololo(23),Ghume Mshadala (20),Yasini Hussein (18),Issa Alphonce (28),Magreth Amosi(24),Masaba Tama(33),Denis Maduhu(18),Laurent Limbi(18),Mgeni Lushinge(35),Wilkista Okumu(40) na Joseph Saidi(23) wote ni wakazi wa Kijiji cha Iyumbu.
FATUMA JISHIMU(19) aliyelazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Singida pamoja na mwanaye MAARIAMU RAMADHANI(2) kufuatia ajali ya gari aina ya kenta iliyokuwa imewabeba wachezaji na washabiki Iyumbu FC waliokuwa wakienda kucheza mchezo wa kirafiki na timu ya kata ya Mgungira FC.
PICHA Na.879 Ni MAGRETH SAWA (40) aliyelazwa katika wodi namba tatu hospitali ya Mkoa wa Singida akipatiwa matibabu kufuatia ajali ya gari aina ya kenta kucha njia na kupinduka katika Kijiji cha Iyumbu.(Picha zote Na Jumbe Ismailly)
No comments:
Post a Comment