Saturday, September 22, 2018

MFALME WA ROOTS ROCK REGGAE WA TANZANIA JAH KIMBUTE AZIKWA JIJINI TANGA LEO

 Jeneza lenye mwili wa Mfalme wa Reggae nchini Marehemu Jah Kimbute ukitelemshwa kwenye nyumba yake ya milele wakati wa mazishi ya mwanamuziki huyo aliyefariki Alhamisi iliyopita nyumbani kwake Msasani jijini Dar es salaam. Mazishi hayo yamefanyika Dunga na kuhudhuriwa na mamia ya waombolezaji
 Jeneza lenye mwili wa Mfalme wa Reggae nchini Marehemu Jah Kimbute ukitelemshwa kwenye nyumba yake ya milele wakati wa mazishi ya mwanamuziki huyo aliyefariki Alhamisi iliyopita nyumbani kwake Msasani jijini Dar es salaam. Mazishi hayo yamefanyika Dunga na kuhudhuriwa na mamia ya waombolezaji
Wazazi wa Jah Kimbute, Mzee Mrinde Samuel Kimbute na Mama Judith Kimbute baada ya kuweka shada la maua kwenye kaburi la mtoto wao wakati wa mazishi ya mwanamuziki huyo aliyefariki Alhamisi iliyopita nyumbani kwake Msasani jijini Dar es salaam.
Ras Kimbute, mtoto mkubwa wa marehemu Jah Kimbute, akiwa na mwanae kaburini
Ibada ya mazishi ikiendelea 
Mdogo wa marehemu Jah Kimbute (shati Jekundu), David Kimbute na watoto wa marehemu
Baba mzazi wa Jah Kimbute, Mzee Mrinde Samuel Kimbute 
Majonzi yametawala mazikoni
 Mjane wa marehemu Jah Kimbute akiweka shada la maua kwenye kaburi wakati wa mazishi ya mwanamuziki huyo aliyefariki Alhamisi iliyopita nyumbani kwake Msasani jijini Dar es salaam. Mazishi hayo yamefanyika Dunga na kuhudhuriwa na mamia ya waombolezaji
Watoto na mjukuu  wa marehemu Jah Kimbute wakiweka shada la maua kwenye kaburi la baba yao wakati wa mazishi ya mwanamuziki huyo aliyefariki Alhamisi iliyopita nyumbani kwake Msasani jijini Dar es salaam. Mazishi hayo yamefanyika Dunga na kuhudhuriwa na mamia ya waombolezaji. Sikiliza moja ya kazi za Jah Kimbute enzi za uhai wake aliyoitoa miaka ya 1980 akiwa mwanamuziki aliyekuwa mstari wa mbele katika kupigania amani na demokrasia.
Mama mzazi wa Jah Kimbute, Mama Judith Kimbute (kilemba cheupe) akiwa na ndugu zake msibani
Mwananmuziki Ras Jhikoman akiwa na mke, watoto na mjukuu wa marehemu Jah Kimbute baada ya mazishi. 
SIKILIZA MOJA YA KAZI ZAKE HAPA CHINI

No comments: