Cassius O. Mdami ni miaka miwili sasa tangu umetuacha familia yako; mke wako Rose Mdami; na watoto wako Martina, Grace, Gideon, Gonsalver na Gibson.

Mungu anajua maumivu yote na machungu tuliyopitia familia yako na tunayoendelea kuyapitia kwa kutokuwepo kwako. Machozi yanatudondoka na hakuna wa kuyafuta; ila tumaini tunalo ya kwamba iko siku moja tutaonana nawe katika makao ya Baba Mbinguni.
Mungu endelea kutufariji kama maneno yako yasemavyo katika kitabu cha Kumbukumbu la Torati 31:8 “ Naye Bwana ndiye atakayekutangulia, atakuwa pamoja nawe, hatakupungukia wala kukuacha; usiogope wala usifadhaike ”
Pumzika kwa Amani Baba G4
No comments:
Post a Comment