Saturday, August 4, 2018

DKT. SHEIN ATEMBELA OFISI ZA KIWANDA CHA MAFUTA YA NAZI NCHINI INDONESIA

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akisalimiana na Meneja Mauzo wa Kiwanda cha mafuta ya Nazi cha Samani Island Virgin Coconut Oil Manufacture kiliopo Jimbaran Bali Nchini Indonesia wakati alipotembelea Ofisi hizo jana akiwa katika ziara ya mualiko wa Makamo wa Rais wa Indonesia Mhe.Mohamed Jusuf Kalla
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) na Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Malaysia pia akiiwakilisha Tanzania Nchini Indinesia Mhe.Dkt.Ramadhan Kitwana Dau, (kulia) na Meneja Mauzo wa Kiwanda cha mafuta ya Nazi cha Samani Island Virgin Coconut Oil Manufacture kiliopo Jimbaran Bali Nchini Indonesia Nd,Iwayan Sundarma wakiangalia burudani baada ya mapokezi katika ofisi za kiwanda hicho 
 Meneja Mauzo wa Kiwanda cha mafuta ya Nazi cha Samani Island Virgin Coconut Oil Manufacture kiliopo Jimbaran Bali Nchini Indonesia Nd,Iwayan Sundarma  (kushoto) akitoa maelezo kwa  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) pamoja na ujumbe wake walipotembela  jana Ofisi za Kiwanda hicho kiliopo  Jimbaran Bali Nchini Indonesia
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein pamoja na Ujumbe wake (hawapo pichani)  jana walipotembelea Kiwandani hapo waliweza kuona bidhaa mbali mbali zinazotokana na nazi ambazo hutengenezwa kwa kupitia  Kiwanda cha mafuta ya Nazi cha Samani Island Virgin Coconut Oil Manufacture kiliopo Jimbaran Bali Nchini Indonesia 
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akiwa na ujumbe wake (kushoto) wakizungumza na Uongozi wa Kiwanda cha mafuta ya Nazi cha Samani Island Virgin Coconut Oil Manufacture katika Ofisi ziliopo Jimbaran Bali Nchini Indonesia  walipotembelea jana  katika ziara ya mualiko wa Makamo wa Rais wa Indonesia Mhe.Mohamed Jusuf Kalla. [Picha na Ikulu.] 

No comments: