Monday, July 2, 2018

WALIOKUWA NGARIBA TARIME WAPEWA MAFUNZO YA UJASIRIAMALI.

Na Frankius Cleophace Tarime.

Waliokuwa Ngariba Wilayani Tarime Mkoani Mara wamepatiwa Mafunzo ya Ujasiriamali kwa lengo la kujikwamua Kiuchumi ili wasirudie tena suala Ukeketaji kwa Mtoto wa ni baada ya kupatiwa Elimu juu ya Madhara ya Ukeketaji kwa Mtoto wa Kike.

Ngariba hao wamedai kuwa kipindi cha Ukeketaji hupata pesa Nyingi zinazotokana na Ukeketaji jambo ambalo uwangumu kuacha kitendo hicho licha ya Mashirika mbalimbali likiwemo Shirika la AFGM Masanga kuendelea kutoa Elimu juu ya Madhara ya Ukeketaji ili Jmii iweze kubadilika.

Kwa kuliona hilo Shirika la ATFGM Masanga ambao ni wadau wa Kupinga Ukatili katika Jamii wameamua kutoa Mafunzo ya Ujasiriamali kwa Waliokuwa Ngariba lakini kwa sasa wameachana na Kitendo hicho baada ya kupewa Elimu ili waweze kufanya kazi zinazotambulika na Serikali kwa lengo la kujipatia kipato na siyo kutegemea tena Ukeketaji.

Mafunzo hayo ya Ujasirimali pia yamewashirikisha Mabinti lengo ni kuwajengea Uwezo ili kuendelea kutoa Elimu hiyo katika Jamii inayowazunguka huku walikuwa Ngariba hao wakipatiwa Mafunzo ili kuendeleza Biashara zao na kuondokana na mawazo ya kurudia kukeketa tena.

Wamedai kuwa katika Kukeketaji wamekuwa wakipata zaidi ya Mill Nane mpaka Tisa Ukeketaji unamalizika huku Binti Mmoja akikeketwa kuanzia Elfu Kumi na zaidi.“Sisi kipindi cha Ukeketaji tulikuwa tunapata Pesa Nyingi lakini kwa sasa wazee wamekataa hatutakeketa tena hivyo tunaomba Serikali itupatie Mitaji baada ya Mafunzo haya tuliyoyapata” alisema Mmoja wa Walikuwa Ngariba.

Akifunga mafunzo hayo katibu wa afya wilaya ya Tarime Neema Alphonce amewataka Waliokuwa Ngariba pamoja na Mabinti hao kuendelea kuwa mabarozi wazuri katika Jamii inayowazunguka huku wakitumia Vizuri Vikundi vilivyoundwa na kupewa Elimu ya Ujasiriamali.

Naye mwezeshaji wa mafunzo hayo Stella Tungalaza amezidi kusisitiza kuzingatia vyema kile Walichofundishwa darasani kwa lengo la kujikomboa na kuongeza Uchumi

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shirika la ATFGM Masanga Sister Stella Mgaya ambao ni wadau wa kuipiga Vita Ukatili wa Kijinsia Wilayani Tarime Mkoani Mara anazidi kusisitiza Wazee wa Mila kusimia Vyema Kauli ya kuwa Mwaka huu hapatakuwa na Ukeketaji na Kuomba Serikali kuendelea Kushirikiana Vyema na Mashirika hayo ili kuchukua hatua kali kwa wale watakaokiuka na Kukeketa Mtoto wa Kike.

“Wazee walishatoa Kauli kuwa hakuna Ukeketaji lakini Wakurya wanatabia ya Kujaribu hivyo wanaweza Kujaribu kukeketa na Serikali isipofuatilia wanaongeza kasi ya kukeketa sasa tushirikiane zaidi japo tunashirikiana Vizuri” alisema Stella Mgaya.

Mgeni rasmi ambaye ni Katibu wa Afya Wilaya ya Tarime Neema Alphonce akikabidhi cheti cha Mafunzo ya Ujasiriamali kwa mmoja wa waliokuwa ngariiba baadaya kupata Elimu hiyo.
Picha ya pamoja na Mgeni rasmi na Washiriki baada ya kupata Mafunzo hayo.
Stella Tingalaza ambaye ni Mwezeshaji wa Mafunzo hayo yaliyoandaliwa na Shirika la ATFGM Masanga akiendelea kutoa Elimu kwa washiriki hao wakiwemo Mabinti kutoka Maeneo tofauti.
Mkurugenzi wa Shirika la ATFGM Masanga Sister Stella Mgaya akiongea na Washiriki wa Mafunzo hayo na kusisitiza suala kuendelea kuelimisha jamii katika Maeeo wanayotoka.
Washiriki wakiendelea na Mafunzo hayo.
Mkurugenzi wa Shirika la ATFGM Masanga Sister Stella Mgaya akipongeza Mmoja wa washiriki wa Mafunzo hayo.

No comments: