Monday, July 2, 2018

SPRITE BBALL KINGS YAANZA KUTIMUA VUMBI JIJINI DAR

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

Michuano ya Sprite BBall Kings 2018 hatua ya mchujo imemalizika kwa timu 15 kuingia hatua inayofuata  baada ya michezo 25 kupigwa ndani ya Viwanja vya JMK Youth Park Kidongo Chekundu Jijini Dar es Salaam.

 Mechi hizo zilizoanza saa 2 asubuhi ilizikutanisha timu 50 zote zikiwania nafasi ili ziweze kuingia hatua inayofuata ya 16 bora kuungana na mabingwa watetezi wa Mchenga BBall Stars.

Mkurugenzi wa Ufundi wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu Nchini (TBF) Manase Zablon amesema timu hizo zilizofanikiwa kutinga hatua ya 16 bora wameweza kutumia vigezo vya utofauti wa alama za kushinda na kufungwa.

Manase amesema," mechi zilichezwa 25 na washindi 25 walipatikana katika mchezo vigezo vilivyotumika ili kuwapata wakaoenda hatua ya 16 bora tuliangalia utofauti wa vikapu vya kushinda na kufungwa."

Amesema, mechi zilikua na ushindani mkubwa sana na ushindani huo ulipelekea hata zile timu zilizoshiriki mwaka jana zitoke mapema kwakuwa kila timi imejiandaa kuhakikisha wanakuwa mabingwa wapya wa mwaka 2018.

Timu zilizofanikiwa kuingia hatua inayofuata  kuungana na mabingwa watetezi ili kutimiza idadi ya timu 16 ni The Team Kiza, Stylers, St Joseph, Oysterbay, Flying Dribblers, Portrands, Raptors, Ukonga Hitmen, Ukonga Warriors.

Zingine ni Temeke Heroes,Water Institute, Fast Heat, Mbezi Beach KKKT, Air Wings na DMI na ratiba ya hatua ya 16 bora itapangwa mbashara leo kwenye kituo cha EATV saa 3:30 kupitia kipindi cha 5 Sports.

Michuano ya Sprite BBall Kings imeandaliwa na kituo cha Televishen cha EATV na Radio yakidhamiwa na kinywaji cha Sprite wakiwa na lengo la kurejesha heshima ya mpira ya kikapu nchini.

Bingwa wa michuano hiyo atajinyakulia kitita cha Shilling Milioni 10 na kikombe, mshindi wa pili akibeba Milioni 3 na mchezaji bora wa mashindano ( MVP) akibeba milioni 2.
 Mchezaji wa timu ya St Joseph Jermaine Ishengoma akiifungua timu yake dhidi ya Madena Ballers. Ambapo St joseph aliibuka mshindi katika hatua ya mchujo  uliofanyika jumamosi jijini Dar es salaam katika viwanja vya JMK Youth Park kidongo chekundu.
 Mchezaji wa Oysterbay Godfrey Swai akijaribu kumtoka mchezaji wa Ilala East Zone Ally Salum Bakari wakati wa mashindano ya mpira wa kikapu ya sprite bball kings hatua ya mchujo uliofanyika jumamosi jijiji dar es salaam katika viwanja vya JMK Youth Park kidongo chekundu, Ambapo Timu ya Oysterbay iliibuka ushindi wa vikapu 48 kwa 19.
 
 Mchezaji wa timu ya Montifort  akijaribu kumshambulia mpinzani wake wa timu ya Goldent Talent  wakati wa mashindano ya mpira wa kikapu ambapo tmt iliondoka na ushindi.Ambapo Timu ya Montifort  iliibuka ushindi wa vikapu 24 dhidi ya 22 ya Goldent Talents.
Bampa to Bampa......

No comments: