MKUU
wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo akizungumza na wananchi wa
wilaya hiyo waliofanyiwa uchunguzi wa matatizo ya macho wakati wa
zoezi la kufunga kambi ya matibabu ya tiba ya macho
iliyoendeshwa na Taasisi ya isiyokuwa ya kiserikali ya Medewell Health
Centre kwenye kituo cha Afya cha Ubwari wilayani Muheza
Mkurugenzi
wa wa taasisi ya Medewell Munir Meral akizungumza katika ufungaji wa
kambi hiyo kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo
MKUU
wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo katikati akiingia kwenye
Kituo cha Afya Ubwari kufunga kambi ya Macho iliyokuwa ikiendelea
kushoto ni Kaimu Mganga Mkuu wa wilaya ya Muheza Julius Mgeni
MKUU
wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo kushoto akimsikiliza mkazi
wa wilaya ya Muheza akitoa ushuhuda wa kupona macho yake baada ya kupata
matibabu
ZAIDI
ya wagonjwa 300 wamefanyiwa uchunguzi wa matatizo ya macho wilayani
Muheza mkoani Tanga kwenye zoezi lililoendeshwa na wataalamu kutoka
Hospitali ya Medewell iliyopo wilayani ya Kibaha mkoani Pwani huku 121
wakibainika kuwa na tatizo la mtoto wa jicho.
Hayo
yalibainishwa na Kaimu Mganga Mkuu wa wilaya ya Muheza Julius Mgeni
wakati wa zoezi la kufunga kambi ya matibabu ya tiba ya macho
iliyoendeshwa na Taasisi ya isiyokuwa ya kiserikali ya Medewell Health
Centre kwenye kituo cha Afya cha Ubwari wilayani Muheza
Alisema
wataalaamu hao wamekuwa wakiendesha zoezi hilo mara kwa mara ambalo
limekuwa na mafanikio makubwa kwa wagonjwa kupona na kuweza kuona na
hivyo kupunguza idadi ya watu wenye changamoto za namna hiyo.
Alisema
licha ya kufanyiwa uchunguzi lakini wagonjwa 121 walibainika kuwa na
tatizo la mtoto wa jicho ambao waliweza kufanyiwa upasuaji na kupewa
dawa ambazo wanapaswa kuzitumia wakati wa matibabu hayo huku watu 191
wakipatiwa matibabu ya kawaida.
Awali
akizungumza Mkuu wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo alisema
zoezi la uchunguzi na operesheni ambazo zimekuwa zikifanyika vimekuwa na
mafanikio makubwa jambo ambalo limeongeza mwamko wa wananchi kutoka
maeneo mbalimbali ambao wanajitokeza kila wakati.
“Kwa
kweli niwapongeze Medewell kwa kuendesha matibabu haya ya mtoto wa
Jicho nay a kawaida kwani yamekuwa faraja kubwa sana na faida yake
imeweza kuonekana na kuwasaidia watu kuona kuweza kurudi kwenye hali zao
za kawaida”Alisema.
Alisema
hatua hiyo imewawezesha watu kuweza kuona jambo ambalo litawasaidia
wananchi wengi waliokumbwa na tatizo hilo kuweza kufanya shughuli za
uzalishaji mali ikiwemo zile za kujiingizia kipato na hivyo kusaidia
kuinua uchumi wao na jamii zinazowazunguka.
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa wa taasisi ya Medewell Munir Meral alisema
wananchi wamefarijika kwa kiasi kikubwa kutokana na baadhi yao kukata
tamaa kutokana na uwepo wa matatizo hayo ambayo kiuhalisia yana gharama
kukabiliana nayo.
Alisema
mbali ya kutoa msaada wa matatibabu hayo bure lakini pia kwa
kushirikiana na Betacharitable Trust toka Uingereza wamekabidhi kifaa
cha kupima na kuchunhuza matatizo ya macho(slit lamp)yenye thamani ya
zaidi Shilingi Milioni kumi na vifaa vya kupimia miwani (tria set).
Alisema
utolewaji wa vifaa hivyo utarahisisha kituo hicho cha afya kuweza
kuanza kufanya uchunguzi wa matatizo ya macho kupitia wataalamu waliopo
jambo ambalo lilikuwa likishindikana kufanyika kutokana na uhaba wa
vifaa hivyo tiba.
No comments:
Post a Comment