Sunday, July 8, 2018

TIMU NANE ZATINGA ROBO FAINALI SPRITE BBALL KINGS

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.


MICHEZO minne ya hatua ya 16 bora ya Michuano ya Sprite BBall Kings 2018 imefanyika katika viwili tofauti na timu nane kufanikiwa kuingia hatua  ya robo fainali.


Mechi hizo zimepigwa Jumamosi na Jumapili huku michezo minne ya awali ikipigwa katika Viwanja vya Airwing huku mingine ikipigwa Viwanja vya Bandari Kurasini Jijini Dar ed Salaam.

Katika mchezo wa kwanza, timu ya DMI ilifanikiwa kuondoka na ushindi wa vikapu 113 dhidi ya 64 vya Fast Heat na Mechi ya pili ilikua ni kati ya Flying Dribbellrs dhidi ya Ukonga Hitmen ambapo Flying Dribbllers walifanikiwa kuondoka na ushindi wa vikapun 87 dhidi ya 63.

Mchezo wa tatu ulikua baina ya Airwing na St Joseph ambapo Ushindi wa vikapu 98 vya St Joseph dhidi ya 78 vya Airwing uliwapeleka hatua ya robo fainali.Mchezo wa nne ulikua ni baina ya Portland wakichuana na Mbezi Beach KKKT, na Portland kuondoka na ushindi mkubwa wa Vikapu 126 dhidi ya 54.

Mechi zingine nne zimechezwa kwenye Viwanja vya Bandari Kurasini jana zikiwakutanisha Mchenga BBall Stars dhidi ya Oysterbay, Mchenga kufanikiwa kuingia robo kwa vikapu 117 dhidi ya vikapu 56. Mchezo wa pili kati ya Stylers alikua anapambana na Temeke Heroes, na Temeke kufanikiwa kuondoka na ushindi wa vikapu 76 dhidi ya vikapu 58 vya stylers.

Mechi nyingine ya tatu iliwapeleka Team Kiza robo fainali kwa vikapu 66 dhidi ya 56 vya Ukonga Warriors huku mchezo wa mwisho ulikua ni baina ya Raptors akichuana na Water Institute na Vikapu 77 vikawapa ushindi Water Institute dhidi ya 68.

Mkurugenzi wa Ufundi wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu (TBF) Manase Zabron amesema kuwa timu zimejiandaa sana na aliyejiandaa vizuri ndio ataondoka na ubingwa wa 2018. Amesema kwa mwaka huu kutakua na ushindani mkubwa sana.

Michuano ya Sprite BBall Kings 2018 yanayodhamiwa na kinywaji cha Sprite  yameanza mwishoni mwa wiki kwa hatua ya mchujo kufanyika, timu 8 kufanikiwa kuvuka kuingia robo fainali na zinaenda kukutana siku ya Jumamosi baada ya droo kuchezeshwa kesho mubashara kupitia kituo cha EATV na EA Radio.

Mshindi wa kwanza atafanikiwa kuondoka na kitita cha Milioni 10 pamoja na Kombe, Mshindi wa pili milioni 3 na mchezaji bora wa mashindano akitwaa milioni 2 
Mchezaji wa Portlands Dennis Babu (jezi nyeupe) akipambana na mchezaji wa Mbezi Beacj KKKT wakati wa mchezo wao wa hatua ya 16 bora uliomalizika kwa Portland kuondoka na ushindi wa Vikapu 126 dhidi ya 54 ya Michuano ya Sprite BBall Kings.
Mchezaji wa Ukonga Warriors Richo Rover akijaribu kumkwepa Baraka Mopere wa Flying Dribbllers wakati wa mchezo wao wa hatua ya 16 ya Michuano ya Sprite BBall Kings baina yao uliomalizika kwa Flying Dribbllers kuondoka na ushindi wa Vikapu 87 kwa 63.

No comments: