Tuesday, July 10, 2018

KAMATI YA BUNGE YA MIUNDOMBINU YATEMBELEA SHIRIKA LA POSTA JIJINI DAR ES SALAAM

Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Joseph Ngowi, akizungumza wakati Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Miundombinu, ilipotembelea shirika hilo, kupata taarifa ya utendaji wa shirika, jijini Dar es Salaam leo.
Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Miundombinu, wakiwa pamoja na uongozi wa Shirika la Posta wakati walipotembelea shirika hilo, kupata taarifa ya utendaji wa shirika, jijini Dar es Salaam leo. 
Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania, Hassan Mwang'ombe, akitoa maelezo mafupi kwa Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Miundombinu, walipotembelea shirika hilo, kupata taarifa ya utendaji, jijini Dar es Salaam leo. Katikati ni Mwenyekiti wa kamati hiyo, Moshi Seleman Kakoso na wa nne kushoto ni Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Sekta ya Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Sekta ya Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye, akitoa ufafanuzi kwa Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Miundombinu, walipokuwa katika kikao na uongozi wa Shirika la Posta leo jijini.
Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Miundombinu, wakisikiliza maelezo yaliyokuwa yakitolewa na Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Sekta ya Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye, wakati wajumbe wa kamati hiyo, walipokuwa katika kikao na uongozi wa Shirika la Posta leo jijini. 
Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta Tanzania, Kanali Mstaafu, Dk. Haruni Kondo akitoa ufafanuzi wakati Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Miundombinu walipotembelea Shirika hilo jijini Dar es Salaam leo.
Kaimu Meneja Mkuu Rasiliamali za Shirika, Macrice Mbodo akitoa taarifa ya utendaji wa shirika kwa Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Miundombinu wakati wa ziara hiyo, jijini Dar es Salaam leo.
Meneja Biashara Mtandao wa Shirika la Posta Tanzania, Amina Salum akitoa taarifa ya maduka ya biashara mtandao yaliyoanzishwa na shirika hilo, kwa Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Miundombinu wakati wa ziara hiyo, jijini Dar es Salaam leo. 
Postamasta Mkuu, Hassan Mwang'ombe, akitoa ufafanuzi huku baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo, wakisikiliza kwa makini kuhusu Maduka ya Biashara Mtandao yatakavyofanya shughuli zake na kuwanufaisha wananchi, Serikali pamoja na shirika hilo.
Mwenyekiti wa kamati hiyo, Moshi Seleman Kakoso (kulia), akimtaka mtoa taarifa, Kaimu Meneja Mkuu Rasiliamali za Shirika, Macrice Mbodo, kutoa ufafanuzi zaidi wa taarifa ya jumla ya fedha zinazolipwa kwa wastaafu wa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa mwezi. Katikati  ni Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Sekta ya Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye na kushoto ni Mjumbe wa kamati hiyo, Mussa Azzan Zungu, Mbunge wa Ilala jijini Dar es Salaam. 
Kaimu Meneja Mkuu Rasiliamali za Shirika, Macrice Mbodo akitoa ufafanuzi wa suala hilo, la jumla ya fedha za malipo ya wastaafu wa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa mwezi kwa wajumbe wa Kamati hiyo.
Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Miundombinu, Rukia Kassim, akichangia hoja katika taarifa ya utendaji ya shirika hilo, iliyowasilishwa kwa wajumbe wa kamati hiyo.
Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Miundombinu, Susan Kiwanga, akichangia hoja katika taarifa hiyo, ya utendaji wa shirika hilo. 
Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Miundombinu, Nuru Bafadhil, akichangia hoja katika taarifa ya utendaji ya shirika hilo, iliyowasilishwa kwa wajumbe wa kamati hiyo. 
Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Miundombinu, Pudensiana Kikwembe, akichangia hoja katika taarifa ya utendaji ya shirika hilo, iliyowasilishwa kwa wajumbe wa kamati hiyo. 
Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Miundombinu, Charles Kitwanga (kulia), akichangia hoja katika taarifa hiyo, ya utendaji wa shirika hilo.  
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Sekta ya Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye, akitoa maelezo zaidi kwa Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Miundombinu, kuhusu utekelezaji wa taarifa hiyo. Katikati ni Mwenyekiti wa kamati hiyo, Moshi Seleman Kakoso na kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika, Kanali Mstaafu, Dk. Haruni Kondo.
Mwenyekiti wa kamati hiyo, Moshi Seleman Kakoso, akitoa maelekezo kwa uongozi wa Shirika la Posta wakati akihitimisha mkutano huo. Kushoto ni Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Sekta ya Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye na kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika, Kanali Mstaafu, Dk. Haruni Kondo.
Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Miundombinu, wakiwa katika picha ya pamoja kionesha alama ya dole gumba ikiwa ni ishara ya kuunga mkono kauli mbiu ya Shirika ya 'Lets Go' mara baada ya kumaliza ziara yao kwenye shirika hilo, Makao Makuu ya Shirika la Posta Tanzania.

No comments: