Thursday, June 21, 2018

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AZINDUA MAJENGO YA TAASISI YA ELIMU YA AFYA MVUMI MKOANI DODOMA

 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa  wa nne kulia akikata utepe kuzindua majengo ya Taasisi ya Elimu ya Afya Mvumi yaliyojengwa kupitia ufadhili wa Mfuko wa Dunia wa kupambana na Ukimwi, Kifua Kikuu na Maralia (Global Fund) uliofanyika leo jijini Dodoma na wanne kutoka kushoto ni Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu. 
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa kulia akipokea cheti cha umalizaji wa ujenzi wa majengo ya Taasisi ya Elimu ya Afya Mvumi kutoka kwa Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati wa uzinduzi wa majengo hayo uliofanyika leo jijini Dodoma.
 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa katikati waliokaa akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa Taasisi ya Elimu ya Afya Mvumi wakati wa uzinduzi wa majengo ya Taasisi hiyo yaliyojengwa kupitia ufadhili wa Mfuko wa Dunia wa kupambana na Ukimwi, Kifua Kikuu na Maralia (Global Fund) uliofanyika leo jijini Dodoma, wa tatu kutoka kushoto ni Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa mwenye suti ya bluu akikagua baadhi ya sehemu za majengo ya Taasisi ya Elimu ya Afya Mvumi baada ya kuzindua majengo hayo yaliyojengwa kupitia ufadhili wa Mfuko wa Dunia wa kupambana na Ukimwi, Kifua Kikuu na Maralia (Global Fund) yaliyozinduliwa leo jijini Dodoma.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa kulia akipata ufafanuzi wa kina kutoka kwa Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati wa uzinduzi wa majengo majengo ya Taasisi ya Elimu ya Afya Mvumi yaliyojengwa kupitia ufadhili wa Mfuko wa Dunia wa kupambana na Ukimwi, Kifua Kikuu na Maralia (Global Fund) uliofanyika leo jijini Dodoma.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa  wa Tatu kulia akizindua majengo ya Taasisi ya Elimu ya Afya Mvumi yaliyojengwa kupitia ufadhili wa Mfuko wa Dunia wa kupambana na Ukimwi, Kifua Kikuu na Maralia (Global Fund) uliofanyika leo jijini Dodoma, wa pili kulia ni Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu.
 aadhi ya viongozi na wananchi  wa Mvumi wilayani Chamwino waliojitokeza kumsikiliza na kushuhudia uzinduzi wa Majengo ya Taasisi ya Elimu ya Afya Mvumi yaliyojengwa kupitia ufadhili wa Mfuko wa Dunia wa kupambana na Ukimwi, Kifua Kikuu na Maralia (Global Fund) uliofanya na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa leo jijini Dodoma.PICHA NA WIZARA YA AFYA. 


SERIKALI ITAENDELEA KUTOA KIPAUMBELE KWA  WATAALAM WA AFYA
NA WAMJW-DODOMA

SERIKALI itaendelea kutoa kipaumbele kwenye sekta ya  afya hususan swala la kuajiri wataalam wa kada mbalimbali za afya nchini kwa kuzingatia maeneo yenye uhaba mkubwa wa watumishi hasa maeneo ya vijijini.

Hayo yamesemwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanza
nia Mhe. Kassim Majaliwa wakati wa kuzindua majengo ya Taasisi ya Elimu ya Afya Mvumi yaliyojengwa kupitia ufadhili wa Mfuko wa Dunia wa kupambana na Ukimwi, Kifua Kikuu na Maralia (Global Fund) uliofanyika leo jijini Dodoma.

Mhe. Majaliwa aliendelea kusema kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itaendelea kuchukua hatua mbalimbali katika kutekeleza Malengo Endelevu ya Milenia hususan lengo nambari tatu linalohusu kuboresha afya za watu pamoja na ustawi wao.

“Miongoni mwa hatua hizo ni kuhakikisha tunashirikiana na wadau wote ili kuongeza idada ya wataalam wa afya nchini kwa kuvijengea uwezo wa kimiundombinu vyuo vya elimu ya afya nchini ili viweze kuongeza udahili na kuzalisha wataalam bora wa afya” alisema Mhe. Majaliwa.

Aidha, Mhe. Majaliwa aliwataka wananchi kuunga mkono juhudi za Serikali za kuongeza idadi ya watumishi wa afya nchini watakaotekeleza majukumu yao kwa uadilifu na weredi mkubwa kwani Taifa bora linajengwa na wananchi wenye afya bora na afya bora kwa wananchi itapatikana iwapo watahudumiwa ipasavyo.

Mbali na hayo Mhe. Majaliwa alisema kuwa nchi bado inakabiliwa na changamoto  ya magonjwa ya Kifua kikuu na Malaria ,hata hivyo Serikali kwa kushirikiana na wadau wa sekta ya afya nchini imeongeza wigo wa upatikanaji wa huduma za ugunduzi wa magonjwa hayo kwa kutumia vipimo vya vina saba (gene -expert).

“Tumefanikiwa kusambaza mashine za “gene expert” 191 kwenye Hospitali zote za Rufaa za Kanda ,Mikoa,Wilaya na baadhi ya vituo vikubwa vya afya ili kuwezeza kupata majibu ya vipimo vya utambuzi wa kifua kikuu ndani ya masaa mawili badala ya kipimo cha hadumini kinachotoa majibu baada ya masaa 24” alisema Mhe. Majaliwa

Aidha , Mhe. Majaliwa amewataka wananchi kujikinga na maambukizi ya Malaria kwa kuzuia mazalia ya mbu kupitia usafi wa mazingira wanayoishi na kutumia vyandarua kwa usahihi ili kuunga mkono juhudi za Serikali katika mapambano dhidi ya ugonjwa huo.

Kwa uapnde Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto mhe. Ummy Mwalimu  ametoa shukrani zake kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuendelea kutoa kipaumbele kikubwa katika masuala ya afya za Watanzania.

“Serikali kupitia Wizara yangu itaendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo kwenye sekta ya afya yenye lengo la kuboresha huduma za afya na  vyuo vya kutolea mafunzo ya kada za afya ili kuimarisha afya za wananchi” alisema waziri Ummy.

Naye Mkurugenzi wa Tume ya Kikristo ya Huduma za jamii Bw. Peter Maduki amesema kuwa mradi wa ukarabati ,upanuzi na ujenzi wa majengo mapya pamoja na vifaa tiba na tahama ulioanza April 2015  katika chuo hicho umegharimu shilingi Bilioni 5.2 ikiwa na malengo ya kuongeza  

No comments: