Tuesday, June 26, 2018

WANANCHI WAIPIGIA MAGOTI SERIKALI KUTAFUTA UFUMBUZI WA MGOGORO ULIODUMU KWA MIAKA 37 TARIME

Na Frankius Cleophace, Tarime

WANANCHI wa Kijiji cha Kebweye katika Kata ya Nyakonga wamewatupia lawama wananchi wa Kijiji cha Kyoruba kata ya Pemba kwa madai kuwa wamevamia eneo lililodaiwa kuwa na mgogoro takribani miaka 37 na kufyeka mazao yao.

Mbali ya kuvamia eneo hilo wamedai kuwa wamekuwa wakijenga nyumba usiku na mchana jambo ambalo limewafanya wananchi wa Kebweye kutoa ombi kwa Serikali kuingilia kati.

Wakizungumza jana kwenye mkutano wa kufanya maendeleo SAIGA wananchi hao wamedai mgogoro wa eneo hilo linalogombaniwa kati ya Kijiji cha Kebweye na Kyoruba ulianza tangu mwaka 1981 ambapo viongozi wa Serikali wamekuwa wakienda pale lakini uamuzi wanayotoa wananchi hao hawaridhiki.

Diwani wa Kata ya Nyakonga Riziki Mwita amesema suala la kufyekwa kwa mazao na kuanza ujenzi litasababisha familia nyingi kutaabika kwa kukosa chakula, hivyo Serikali ya wilaya iweze kuingilia mapema na kutatua changamoto hiyo.

"Mkuu wa Wilaya ya Tarime Luoga alifika eneo hili na kuamua wananchi wote pande mbili walitumie kwa ajili ya kilimo lakini sasa tunashangaa wenzetu wamevamia eneo hilo usiku na kufyeka mazao nakujenga kwa ajili ya Makazi,"amesema Diwani.Mwenyekiti wa Kijiji cha Kebweye Marwa Mniko amesema mgogoro huo umedumu kwa muda mrefu na wametoa taarifa katika mamlaka mbalimbali lakini hata baadhi ya viongozi wanapindisha ukweli na matokeo yake wananchi wanateseka.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Tarime Gloriuos Luoga akizungumzia mgogoro huo amefafanua kuwa uanzishwaji wa kijiji linasimamiwa na Rais kwa mujibu wa sheria.Amesema kwa sasa ameagiza Mkurugenzi kufuatilia suala la GN zote katika ofisi za ardhi ili kila sehemu yenye mgogoro wa mipaka wilayani Tarime waweze kusoma GN hizo ili kuondoa migogoro hiyo

Pia amewatupia lawama viongozi wa kuchaguliwa wakiwemo wenyeviti wa vijiji na madiwani kwa madai ndio chanzo kikubwa cha migogoro hiyo na wamekuwa wakiichochea."Huu mgogoro wa Kyoruba na Kebweye nimeenda zaidi ya mara tatu Mwenyekiti wa Kijiji cha Kebweye amaeandika barua lakini tatizo hawa viongozi kipindi cha kampeni wanadanganya wananchi,"amesema.

Pia amesema viongozi hao wa kuchaguliwa wamekuwa wakiuchochea mgogoro huo ili waendelee kuongoza jambo ambalo ni hatari kwani kubadili GN zinazowekwa kipindi kijiji kinaanzishwa haiwezekani.Hivyo amewataka wananchi kutowasikiliza wanasiasa pale wanapokuwa na tatizo wafike mara moja ofisini kwake kwa lengo la kupata ufumbuzi mara moja.

Wananchi na wakazi wa Kijiji cha Kebweye Kata ya Nyakonga wakiongea na Vyombo vya habari katika Mkutano wa hadhara uliofanyika kijiji hapo kwa lengo la kuzungumzia kilio chao cha Mgogoro ambao umedumu takribani Miaka 37 kuanzia Mwaka 1981.

Wananchi na wakazi wa Kijiji cha Kebweye Kata ya Nyakonga wakiongea na Vyombo vya habari katika Mkutano wa hadhara uliofanyika kijiji hapo kwa lengo la kuzungumzia kilio chao cha Mgogoro ambao umedumu takribani Miaka 37 kuanzia Mwaka 1981.

Wananchi na wakazi wa Kijiji cha Kebweye Kata ya Nyakonga wakiongea na Vyombo vya habari katika Mkutano wa hadhara uliofanyika kijiji hapo kwa lengo la kuzungumzia kilio chao cha Mgogoro ambao umedumu takribani Miaka 37 kuanzia Mwaka 1981.

Viongozi wa Serikali ya Kijiji akiwemo Diwani wa kata ya Nyakonga Riziki Mwita wakiwa katika kikao hicho.

Wananchi wa kijiji cha Kebweye kata ya Nyakonga Wilayani Tarime Mkoani Mara wakiwa katika Mkutano huo.

Mkuu wa Wilaya ya Tarime Glorious Luoga akielezea jitihada za Serikali kutatua Mgogoro huo baina ya Wananchi wa kijiji cha Kebweye na Kyoruba ambapo Mkuu wa Wilaya amesema Mgogoro huo unachangiwa kuchochewa na Viongozi wa Kisiasa.

Ni Maeneo yanayodaiwa kuvamiwa na Wananchi wa Kijiji cha Kyoruba na kufyeka Mashamba kisha kujenga Majengo yao Usiku na kuanzisha Makazi kwa madai ni Maeneo yao.

Ni Maeneo yanayodaiwa kuvamiwa na Wananchi wa Kijiji cha Kyoruba na kufyeka Mashamba kisha kujenga Majengo yao Usiku na kuanzisha Makazi kwa madai ni Maeneo yao.

Viongozi wa Serikali za Vijiji na baadhi ya Waananchi wakiangalia baadhi ya Nyaraka zinazozungumzia Mgogoro huo.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Kebweye Marwa Mniko akiongea na wananchi hao katika Mkutano huo kabla ya kutoa Malalamiko yao.

No comments: