Mkurugenzi
wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa, Robert Masunya na naibu mkurugenzi
wa Mradi wa Urasimishaji Ardhi (LTA) unaofanywa chini ya mpango wa Feed
The Future kwa ufadhili wa Shirika la Misaada la Marekani (USAID) Malaki
Msigwa wakimkabidhi hati ya kimila mmoja ya wananchi wa kijiji cha
Mlanda ambaye ni mlemavu
Naibu
mkurugenzi wa Mradi wa Urasimishaji Ardhi (LTA) unaofanywa chini ya
mpango wa Feed The Future kwa ufadhili wa Shirika la Misaada la Marekani
(USAID) Malaki Msigwa akitoa neo kwa wananchi wa kijiji cha Mlanda
wakati wa kutoa hati za kimila
Mkurugenzi
wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa, Robert Masunya na naibu mkurugenzi
wa Mradi wa Urasimishaji Ardhi (LTA) unaofanywa chini ya mpango wa Feed
The Future kwa ufadhili wa Shirika la Misaada la Marekani (USAID) Malaki
Msigwa wakimkabidhi hati ya kimila mmoja ya wananchi wa kijiji cha
Mlanda ambaye alikuwa anawakilisha kundi la wazee
Baadhi
ya wananchi waliojitokeza kushirikia zoezi la utoaji wa hati miliki za
kimila zilizotolewa na Mradi wa Urasimishaji Ardhi (LTA) unaofanywa
chini ya mpango wa Feed The Future kwa ufadhili wa Shirika la Misaada la
Marekani (USAID)
Picha
ya pamoja baina ya viongozi wa Mradi wa Urasimishaji Ardhi (LTA)
unaofanywa chini ya mpango wa Feed The Future kwa ufadhili wa Shirika la
Misaada la Marekani (USAID),viongozi wa halmashauri ya wilaya ya Iringa
pamoja na baadhi ya wananchi walikuwa tayari wamepokea hati za kimila
NA FREDY MGUNDA.IRINGA.
JUMLA
ya wanakijiji 772 kati ya 1890 wa kijiji cha Mlanda kata ya Magulilwa
wilaya ya Iringa mkoani Iringa wamepimiwa maeneo na mashamba yao na
kukukabidhiwa hati miliki za kimila zinazotolewa kupitia Mradi wa
Urasimishaji Ardhi (LTA) unaofanywa chini ya mpango wa Feed The Future
kwa ufadhili wa Shirika la Misaada la Marekani (USAID).
Hati
hizo zilikabidhiwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa,
Robert Masunya wakati wa sherehe fupi za kuwakabidhi hati hizo
zilizofanyika kijijini hapo na kuhudhuriwa na umati mkubwa wa wananchi
na wageni mbalimbali walikuwepo katika tukio hilo.
Akizungumza
na wanakijiji hao baada ya kukabidhi hati hizo Masunya alisema kuwa
hati hizo zitawasaidia kutenga maeneo kwa ajili ya matumizi mbalimbali
kwa kuzingatia uwezo wa ardhi kuhimili idadi hiyo na kasi ya ongezeko la
watu na mifugo kwa miaka mingi ijayo.
Masunya
aliongezea kuwa,hatua hiyo itasaidia kupunguza migogoro ya ardhi kwa
kuimarisha usalama wa miliki za ardhi na kuongeza thamani ambayo
itawawezesha hata kukopesheka katika taasisi za kifedha zikiwemo benki.“Usajili
wa ardhi ni muhimu kwasababu unaongeza ulinzi wa umiliki wa ardhi,
unawezesha uwekezaji, unaongeza thamani ya ardhi na unapunguza migogoro
ya ardhi,” alisema Masunya
Masunya
aliupongeza mpango huo akisema utasaidia kupunguza eneo kubwa la ardhi
ya Halmashauri ya Wilaya ya Iringa ambayo haijapimwa.
Aidha
Masunya aliwaomba Feed The Future wautanue mradi huo angalau ufike
umalize kupima vijiji vyote vya Halmashauri ya Wilaya ya Iringa huku
akivikumbusha vijiji vyote vya wilaya hiyo kuendelea kutoa ushirikiano
kwenye miradi ambayo inasaidia kukuza maendeleo ya nchi.
“Tunataka
katika kipindi ambacho Mradi wa Urasimishaji Ardhi (LTA) unaofanywa
chini ya mpango wa Feed The Future kwa ufadhili wa Shirika la Misaada la
Marekani (USAID) tuhakikishe tunapima ardhi na mipango ya matumizi bora
na ipimwe ili kila mwenye kipande chake cha ardhi awe na hati yake,”
alisema Masunya.
Alisema
kwa kupitia sera hiyo, kutakuwa na usimamizi zaidi wa ulinzi wa ardhi
ya watu masikini ili kupunguza uporaji wa rasilimali hiyo unaofanywa na
matajiri.“Marekebisho
ya sera hiyo ya ardhi yatawezesha pia kufanyika kwa mrekebisho ya
sheria mbalimbali za ardhi ili ziendane na sera na mazingira ya sasa,”
alisema Masunya.
Masunya
aliwataka wanakijiji wa kijiji hicho ambao hawajapimiwa maeneo yao kwa
sababu mbalimbali ikiwemo ubishi na migogoro ya kifamilia kutumia vizuri
muda ambao bado mradi huo upo katika wilaya hiyo na kuhakikisha nao
wananufaika na zoezi hilo.
Wanakijiji
ambao hawajapimiwa maeneo yao wanaweza kuendeleoa kuzalisha migogoro
ambayo haina tija kwa maendeleo yao na kusababisha waendelee kuwa
masikini kwa kuwa hawatakuwa na dhamana ya kwenda kukopa.
Awali
naibu mkurugenzi wa Mradi wa LTA, Malaki Msigwa alisema kuwa kijiji cha
Mlanda kinajumla ya wananchi 1890 na walio nufaika na Mradi wa
Urasimishaji Ardhi (LTA) unaofanywa chini ya mpango wa Feed The Future
kwa ufadhili wa Shirika la Misaada la Marekani (USAID) ni wananchi 772
na kufanikiwa kutoa jumla ya hati miliki za kimila 1777 ambapo wanaume
walikuwa 409 na wanawake 363.
Msigwa
aliwapongeza wataalamu wa mradi huo kwa kuhakikisha wanawasaidia
wananchi wa kijiji cha Mlanda kupima maeneo yao na kupata hati miliki za
kimila ambazo zitakuwa msaada mkubwa kwenye maendeleo ya kiuchumi.
“Baadhi
ya miradi imeibuliwa wakati wa upimaji wa ardhi hivyo ni fursa sasa kwa
wananchi wenyewe kuitumia vizuri ardhi waliyopimiwa na kupewa hati
miliki za kimila na kwa kuwa asilimia fulani kijiji hiki kimepimwa hivyo
wanaweza kuwa kijiji cha mfano kwa kuwapa maendeleo hata wawekezaji
wazuri kwa faida yao” alisema Msigwa
Msigwa
alisema kati ya vijiji hivyo 41 vitakavyotayarishiwa mipango ya
matumizi bora ya ardhi na kila mwenye ardhi kupimiwa na kupewa hati
miliki za kimila, vijiji 36 vipo wilayani Iringa na vitano vipo wilayani
Mbeya.
“Baada
ya kukamilisha zoezi la upimaji mashamba na urasimishaji wa kijiji
chote cha Mlanda, hivi sasa mradi unaendelea na upimaji mashamba katika
vijiji vya mradi ambavyo vipo wilayani Iringa” alisema Msigwa
Naye
diwani wa kata ya Magulilwa Jane Mhangala aliupongeza Mradi wa
Urasimishaji Ardhi (LTA) unaofanywa chini ya mpango wa Feed The Future
kwa ufadhili wa Shirika la Misaada la Marekani (USAID) kwa kuzingatia
jinsia wakati walipokuwa wanaendesha zoezi la upimaji ardhi katika
kijiji hicho.
“Hongera
sana LTA kwa kuwapa elimu wanawake na wanaume na kuhakikisha kuwa
wanapa haki zao sawa bila kuwa na mgogoro wowote tofauti na ilivyokuwa
hapo awali,maana miaka ya nyuma mwanamke alikuwa anabaguliwa kwenye kila
kitu wala alikuwa haruhusiwi hata kumili ardhi” alisema Mhangala.Mhangala
aliongeza kwa kusema kuwa wanakijiji wa kijiji cha Mlanda baada ya
kupata elimu ya kumiliki ardhi kumepunguza sana migogoro ambayo ilikuwa
inaleta chuki kwenye familia.
“Kwa
sasa ardhi ya kijiji hiki imepanda dhamani kwa kiasi kikubwa na tayari
ishapimwa na mmepata hati miliki za kimila ambazo zitawasaidia katika
maendeleo yenu ya kiuchumi” alisema Mhangala
No comments:
Post a Comment