





sehemu ya vitu ambavyo vilikabidhiwa
Wafanyakazi
wa Bandari ya Tanga wametoa msaada wa vitu mbalimbali vyenye thamani y
ash.milioni 1.5kwa kituo cha wazee wasiojiweza kilichopo eneo la
Mwanzange Jijini Tanga
Msaada
wa vitu hivyo ni vyakula mbalimbali ambavyo vitatumika kwa ajili ya
kusheherekea sikukuu ya Eid El Fitri ambapo halfa ya makabidhiano
ilifanyika juzi kwenye kambi hiyo.
Akizungumza
mara baada ya kukabidhi msaada huo,Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi
Bandari ya Tanga Hassan Senkole alisema waliona ni busara kupunguza
sehemu ya mapato yao katika mwezi mtukufu wa ramadhani kuwasaidia wazee
hao.
Alisema
waliamua kutoa msaada huo ili kuwa sehemu ya jamii iliyowasaidia wazee
hao katika sikukuu ya Eid EL Fitri ili nao waweze kusheherekea sikukuu
hiyo bila kuwepo kwa vikwazo vya aina yoyote ile.
No comments:
Post a Comment