Na Rhoda Ezekiel Kigoma
IMEELEZWA zaidi ya tani 160 za matumizi ya nishati ya kuni na mkaa hutumika katika kambi za wakimbizi mkoani Kigoma kwa siku moja, kwa matumizi ya kupikia.
Hivyo hali ina sababisha uharibifu wa mazingira katika maeneo yaliyokaribu na kambi hizo.Hayo yalibainika jana wakati wa kilele cha Maadhimisho ya siku ya mazingira Duniani , yaliyofanyika kimkoa katika Kambi ya Nyarugusu wilayani Kasulu mkoani humo.
Akizungumza Mratibu wa mradi wa utunzaji wa mazingira kambini CEMDO Tanzania Frank Kayegameni akitoa taarifa ya mradi huo amesema kutokana na idadi kubwa ya wakimbizi kambi ya Nyarugusu ambayo imesababisha uhitaji mkubwa wa matumizi ya mazao ya misitu.Amefafanuana wakimbizi huenda kutafuta kuni nje ya kambi kwa kukata miti ambapo kwa siku inakadiriwa mtu mmoja anatumia kiasi cha kuni kilo moja na kambi inakadiriwa kuwa na wakimbizi 152,309 hivyo kusababisha uharibifu mkubwa.
Amesema katika kupambana na hali hiyo Shirika la uhifadhi wa mazingira na utunzaji wa mazingira kambini ( CEMDO) Tanzania, kwa kushirikiana na Shirika la kuhudumia wakimbizi UNHCR wameandaa utaratibu wa upandaji wa miti 1,425,223 katika Vijiji 13 vinavyozunguka Kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu kwa mwaka 2017/2018 , kugawa majiko banifu kwa kaya 9600 za wakimbizi.
Pamoja na majaribio ya ugawaji wa gesi kwa kaya 3180 lengo likiwa ni kupunguza matumizi ya nishati ya mkaa na kuni yanayosababisha uharibifu mkubwa wa mazingira pamoja na kuboresha mazingira kutokana na uharibifu mkubwa wa uoto wa asili unaotokana na ukataji miti ovyo.
Kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagala amesema kauli mbiu ya maadhimisho ya mazingira ni "Mkaa ni gharama; tumia nishati mbadala",Ambapo amesema kauli hiyo inasaidia utunzaji wa misitu na mazingira, lakini kumekuwa na tabia ya baadhi ya wakimbizi kupewa majiko banifu na gesi kwenda kuuza kwa Watanzania ilikujipatia fedha na kuendelea kuharibu mazingira na kuwataka wakimbizi kuacha tabia hiyo na kuendelea kutumia majiko yaliyotolewa na shirika hilo.
Pia Kanali Ndagala amesema amefurahishwa na shughuli zilizotajwa na mashirika hayo ya Kutunza mazingira na kuwaomba kuongeza utaalamu wa kutumia misitu kwa ufugaji wa Nyuki, kwani ufugaji wa nyuki utawaletea kipato na kuongeza uchumi wao kwa ngazi ya kaya na mtu mmoja,Pia, amewashukuru kwa kazi kubwa ya kuelimisha jamii kutambua umuhimu wa kutunza mazingira , kwa mkoa huo jamii imekuwa na tabia ya uharibifu wa mazingira hasa kwa kuchoma moto.
"Kupitia maadhimisho haya nitoe rai kwa wataalam na Viongozi mbalimbali katika halmashauri kusimamia kwa makini kilimo na shughuli za maendeleo, ili jamii ambazo zimekuwa chanzo cha uharibifu wa vyanzo vya maji ziweze kuhifadhi vyanzo vya maji hili halina mjadala sheria zipo wazi wachukuliwe sheria wale wote wanaolima au kufanya shughuli za kijamii hatarishi katika Vyanzo vya maji", Amesem.
Pia suala la uchomaji moto misitu suala hilo wahusika wote pamoja na viongozi walio katika eneo lililochomwa watachukuliwa hatua, lazima tutunze mazingira kwa maendeleo ya Nchi yetu hili ni agizo.Naye Rais wa Wakimbizi Kambi ya Nyarugusu Abilola Angelique amesema wao kama wakimbizi hawana budi kuunga mkono jitihada zinazofanywa na mashirika yanayo wahudumia, kwa kuwa wanapotunza mazingira hata wao wanaendelea kunufaika kwani watatumia ardhi hiyo kulima mazao ya mboga mboga kwa ajili ya kujikimu na watoto wao.
Amewaomba wakimbizi wenzake kuendelea kusimamia utunzaji wa mazingira.

Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagala akipokea Maelezo ya Mazao ya mboga mboga yanayo limwa na wakimbizi Kambi ya Nyarugusu katika mradi wa utunzaji wa Mazingira
Mmoja wa Wakimbizi akimuelezea Mkuu wa Wilaya namna wanavyo yatumia Majiko banifu kuhakikisha hawaharibu mazingira
Mkuu wa Wilaya ya Kakonko kanali Ndagala akioneshwa na Afisa wa Shirika la CEMDO majiko banifu yanayotumia kuni chache kwa lengo la kutokomeza uharibifu wa mazingira.
No comments:
Post a Comment