Sunday, June 17, 2018

SERIKALI YAPIGA VITA AJIRA KWA WATOTO WILAYANI TARIME, YAHIMIZA KUWAPELEKA SHULE

Na Frankius Cleophacee Tarime.

Serikali imepiga vita suala la Ajira kwa watoto wadogo ikiwemo kufanya biashara ndogondogo kwa watoto hao, badala yake wapelekwe shuleni na kuahidi kuwachukulia hatua kali wazazi na walezi watakaokiuka.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Halmashari ya Wilaya ya Tarime Apoo Castro Tindwa kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Tarime Glorious Luoga katika Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika ambapo kiwilaya Wilaya ya Tarime Maadhimisho hayo yuamefanyika kwenye Viwanja vya Shule ya Sekondari Nyamongo katika Kata ya Matongo.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime Apoo Castro Tindwa amepiga vita suala la ajira kwa watoto hususani kufanya biashara ndogo katika Maeneo ya Stendi huku akipiga vita pia suala la Walimu Wa Shule za Sekondari na Msingi kufanya biashara katika Maeneo hayo.

Katika Maadhimisho hayo zimeweza kushiriki Tasisi mbalimbali Likiwemo Shirika la Jukwaa la Utu wa Mtoto CDF Tarime, ATFGM Masanga, Plan International,Muungano wa Jamii Tanzania MUJATA, Acacia North Mara pamoja na Viongozi wa Dini

Kambibi Kamugisha kutoka Shirika la Jukwaa la Utu wa Mtoto na Valerian Mgani kutoka Shirika la ATFGM Masanga wanazidi kupaza sauti zao kwa jamii ili kutokomeza Suala la Ukeketaji kwa Mtoto wa Kike Wilayani Tarime huku wakiomba serikali Kuungana na Mashirika hayo kwa lengo la kupiga Vita suala la Ukeketaji kwa Mtoto wa kike.

Kamugisha amesema kuwa sualala Ukeketaji ndo chanzo kikubwa cha ongezeko la ndoa za Utotoni katika Mkoa wa Mara hivyo Ukeketaji ukitokomezwa Ndoa za Utotoni zitaisha.

Valerian Mgani Kutoka Shirika la ATFGM Masanga ambao ni wadau wa kupiga Ukatili katika Jamii amesema kuwa Mwaka huu Koo nyingi za Kabila la kikurya zinatarajia Kukeketa Mtoto wa kike hivyo ni jukumu la Serikali pamoja na Mashirika hayo kuungana kuendelea kutoa Elimu hiyo.

Vile vile Shirika la Penuary Root Out Alliance Tanzania kwa kushirikiana na Kituo cha Maendeleo ya Kilimo Mogabiri nao wameweza kuadhimisha Siku hiyo katika kijiji cha Magoma kata ya Binagi lengo ni kufikisha Ujumbe kwa jamii kwa lengo la kunusuru Mtoto katika suala zima la Ukatili.

Wegesa Mosama kutoka Shirika la Penuary Root Out Alliance Tanzaniai anazidi kuimiza jamii kuendelea kupiga Vita Mila na Destuli zililizopotwana wakati Huku Afisa Maendeleo ya Jamii Kituo cha Maendeleo ya Kilimo Mogabiri Naomi Marwa akisisitiza suala la Mwanamke kupewa Fursa pamoja na Kufanya Maamuzi katika Jamii.

Licha ya hayo wasichana ambao wameunda Vikundi katika Kijiji cha Magoma kwa lengo la kuendelea kutoa Elimu ya kupiga Vita Ukatili nao wanaopaza Sauti zao huku wakibainisha Changamoto wanazokumbana nazo kuwa bado jamii inakuwa ngumu kupokea elimu hiyo kwa kudai wanaingilia Mila zao.

Philomena Tontora ni Diwani wa Viti Maalumu Kupitia CHADEMA Kata ya Matongo anasema kuwa Nyamongo kuna Wimbi kubwa la watoto wanaotangatanga hivyo Serikali ichukue hatua kali kwa Wazazi na walezi ili kunusuru watoto hao.

“Kauli mbiu katika Maadhimisho hayo ni Kuelekea kwenye Uchumi wa Viwanda mtoto asiachwe Nyumbani”
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime Mkoani Mara Apoo Castro Tindwa akizungumza mbele ye Wananchi (hawapo pichani) wakati wa maadhimisho ya siku ya Mtoto wa Afrika,ndani ya viwanya vya shule ya sekondari Nyamongo wilayani Tarime .
Muwakilishi Kutoka Shirika la ATFGM Masanga,Valerian Mgani ambao wamekuwa wakipiga vita Ukatili katika jamii akiongea na Wananchi kwenye  Maadhimisho hayo.
Muwakilishi Kutoka Shirika la Plan International , Shaban Shaban akizungumza mbele ya Wananchi katika Maadhimisho hayo.
Wanafunzi kutoka Shule za Msingi zinazozunguka Mgodi wa Uchimbaji wa Mawe ya Dhahabu ACACIA North Mara wakiwa katika Maadhimisho hayo ya Siku ya Mtoto wa Afrika,ndani ya viwanya vya shule ya sekondari Nyamongo wilayani Tarime .
Wanafunzi hao wakiwa na Mabinti kutoka Shirika la Jukwaa la Utu wa Mtoto CDF wakionesha igizo lenye ujumbe wa kupinga Ukeketaji kwa Mtoto wa Kike
Wanafunzi wakiwa wamebeba bango lenye ujumbe wa Siku ya Mtoto wa Afrika.
Baadhi ya viongozi wa Serikali wakiwa katika Maadhimisho hayo.

No comments: