Na Frankius Cleophace, Tarime
NCHI za Kenya na Tanzania zimeshauriwa kuendelea kushirikiana vema katika kupinga na kulaani vitendo vya ukeketaji kwa mtoto wa kike huku zikitakiwa kumthamini na kumpa kipaumbele katika elimu.
Ushauri huo umetolewa leo na Mwenyekiti wa Wazee wa Mila kutoka nchini Kenya Zacharia Ghati wakati wa mkutano wa hadhara ulioandaliwa na wazee wa Mila Kijiji cha Pemba kwa kushirikiana na Shirika la ATFGM Masanga ambao wanapiga vita ukeketaji.Zacharia amesema kuna koo ambazo zinapatikana Tarime kwa upande wa Tanzania pia zinapatikana nchini Kenya, hivyo wote wanatamaduni moja.
" kama ni suala la ukeketaji wengine wanaenda Kenya ili kutimiza azma yao na wengine kutoka Kenya na kuja Tanzana, hivyo sasa kuna haja kubwa ya kushirikiana baina ya nchi zote mbili ili kukomesha ukeketeji,"amesema.
Kwa upande wa Mzee wa Mila kutoka Koo ya Bukenye Elias Maganya anasema wao kama wazee wa mila tayari wamepaza sauti zao na kudai kuwa mwaka huu hapatakuwa na ukeketaji kwa mtoto wa kike.
"Na suala la kupaka unga tutapaka watoto kuanzia miaka 15 si watoto wadogo na lengo ni kutimiza mila na ili suala litamalizika polepole kama zamani tulikuwa tunatoboa masikio."Wajaruo wanangoa Meno lakini Vyote kwa sasa vimeisha na suala la Ukeketaji litaisha lenyewe,"amesema Elias.
Kwa Upande wake Mratibu wa Afya na Ustwai wa Jamii Wilaya ya Tarime Abel Gichaine amesema kusisitiza mikataba ambayo nchi ilisaini kwa lengo la Kulinda haki za binadamu ili zisikiukwe.Hivyo suala la ukeketaji linapotendeka linakikua sheria hizo ikiwemo Sheria ya Mtoto ya Mwaka 2009 huku Mkurugenzi wa Shirika la ATFGM Masana Stella Mgaya amehimiza amehimiza umuhimu wa kumjua ili jamii iondokane na ukeketaji.
Ametumia fursa hiyo kuwataka mabinti kipindi cha tohara inapoanza waende Kituo cha kuhifadhi mabinti hao Masanga ili kupatiwa elimu ikiwemo elimu ya makuzi, kupinga ndoa na mimba za utotoni.
Zacharia Ghati Mzee wa Mila kutoka Nchini Kenya akitoa Elimu kwa Wananchi wa kata ya Pemba .
Wazee wa Mila Muungano wa Koo12 Kabila la Wakurya na Wazee wa Mila kutoaka Nchini Kenya wakiwa katika Mkutano huo wa kutoa Elimu ya Kupinga Ukeketaji kwa Mtoto wa Kike.
Wangubo Mtongori Mzee wa Mila kutoka Koo ya Bukira Tanzania na Kenya akitoa Elimu kwa Wananchi wa kata ya Pemba.
Wanaanchi wa Kijiji cha Pemba kata ya Pemba wakiwasikiliza Wazee wa Mila Muungano wa Koo12 kipindi wakitoa Elimu Hiyo ya kupinga Ukeketaji kwa Mtoto wa Kike.
Abel Gichaine ambaye ni Mratibu wa Huduma ya Afya na Ustawi wa Jamii Wilaya ya Tarime akitoa Elimu kwa Wananchi hao na kutaja madhara yanayompata Mwanamke aliyekeketwa wakati wa kijifungua na kufafanua sheria ya Mtoto ya Mwaka 2009.
No comments:
Post a Comment