Na Woinde Shizza,Arusha
WADAU mbalimbali wa zao la alizeti wameanza jitihada za kujadili mikakati ya kuhakikisha wanainua zao hilo hasa kwa kuzingatia mafuta ya alizeti ni bora kwa afya ya binadamu.
Wanasema kuwa alizeti ni moja kati ya mazao yanayostahimili ukame na kumpa mkulima faida kubwa kutokana na ukwel kwamba mbali ya alizeti kutoa mafuta pia hitoa malighafi nyingine ka
Wakizungunza leo wadau hao wanasema zao hilo pia hutumika katika kukamua mafuta ya kula pamoja na kutengeneza chakula cha mifugo ikiwemo mashudu yanayotumiwa na ng`ombe na kuku ili kunenepesha mifugo pamoja na sabuni.
Hivyo kutokana na umuhimu wa zao hilo pamoja na kuwa na faida nyingi bado jalijapewa kipaumbele stahiki ili Taifa lipate mafuta ya kutosha na kupunguza uingizwaji wa mafuta kutoka nje ya nchi.Wamesema wameanza juhudi za kuhamasisha kilimo cha zao hilo ambalo ni muhimu katika kuchochea uchumi wa viwanda kwani wako wasindikaji wadogo na wakubwa wa mafuta ya alizeti ambao wananunua alizeti kutoka kwa wakulima.
Mkurugenzi wa Taasisi hiyo isiyokua ya kiserikali ya Gola Foundation Salaiwe Elisha Maghembe amesema ili kuhasisha kilimo cha zao hilo wameanzisha shamba la mfano la ekari 30.Ambapo wanalima alizeti kama njia mojawapo ya kuwafundisha wakulima na kukuza uchumi wa taasisi hiyo.
Maghembe amesema tayari wametenga kiasi She. milioni 60 kwa ajili ya kutoa mashine za kusindika mafuta ya alizeti kwa vikundi vya wakulima walioko katika Mikoa ya Mwanza na Kagera .Elisha anasema zao la alizeti linaweza kutumika kuchochea uchumi wa viwanda kwa kuwa na vikundi vya wakulima wanaolima na kusindika zao hilo kwa maana ya kuongeza thamani na kuuza mafuta pamoja na chakula cha mifugo.
Pia licha ya kuhamasisha kilimo cha alizeti wanahasisha ufugaji kuku kwani mabaki ya alizeti baada ya kukamuliwa mafuta hutumika kama chakula bora cha kuku hivyo wakulima hao wakifuga kuku wanaweza kupata kipato cha ziada na kuondokana na umasikini.“Pia tumejikita katika kutoa mafunzo ya kilimo bora cha alizeti kinachofanywa kwa kanuni na taratibu pamoja na utengenezwaji wa kalenda ya zao hilo muhimu,”amesema Elisha
Anaeleza kuwa taasisi hiyo ina mpango wa miaka 10 wa kuwekeza kwenye kilimo cha alizeti pamoja na kutoa mashine rahisi za kukamua alizeti kuwawezesha wakulima kuongeza thamani zao hilo.Amefafanua kwa sasa Gola inashirikiana na Shirika la Kagera Edible Oil katika kuwafikia wakulima wa alizeti mkoani Kagera ambapo wameanzisha Ofisi ya pamoja ili kuwahudumia wakulima kwa karibu ikiwemo mafunzo na vitendea kazi.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Kagera Edible Oil Kibambi Ibrahim anasema zao la alizeti linastawi katika maeoneo yote na linastahimili ukame.Pia halitumii viuatilifu vyenye sumu kali ambavyo ni hatari kwa afya ya mlaji pia kumgharimu mkulima fedha nyingi.Anaeleza kwa Mkoa wa Kagera wamejipanga kuhamasisha wadau kujenga kiwanda cha sabuni ambacho kitatumia malighafi zinazotokana na alizeti kwani mkoa huo bado hauna kiwanda cha sabuni.
Ameongeza tayari wameweka mikakati ya kuhakikisha zao hilo linalimwa kwa wingi na kuongezewa thamani ili yapatikane mafuta ya kutosha ya kuuza ndani na nje ya nchi ikiwemo nchi za Kenya,Uganda,Rwanda na Burundi."Juhudi za kuwaweka wakulima pamoja katika makundi na kuwapatia elimu kuhusu kilimo bora cha alizeti zinaendelea lengo ni kukuza kilimo cha alizeti katika mkoa huo,"amesisitiza.
Imeelezwa ushirikiano baina ya Gola Foundation na Kagera Edible Oil unatarajia kuzaa matunda kwa kuunganisha nguvu kwa pamoja na kuwafikia wakulima na kutatua changamoto zao ikiwemo za kielimu na teknolijia ya usindikaji.Huku wakiwaomba wadua wengine wajitokeze ili kuunga mkono juhudi hizo.
“Tumepanga kuwa na mkutano wa wadau wa alizeti Juni 25 ili kujadili kwa pamoja namna ya kulipeleka mbele zao la alizeti wadau watakutana Bukoba mjini vikundi vyote vya wakulima wa alizeti pamoja na vyama vya ushirika,” anafafanua Kibambi.Anasisitiza zao la alizeti ni mkombozi kwa wakulima kwani mazao mengine yamekua yakiporomoka bei kama kahawa lakini zao la alizeti huwa haliporomoki bei kirahisi na linaweza kuvunwa kwa mwaka mara 3 tofauti na mazao mengine ambayo huvunwa kwa mwaka mara moja.
Kagera Edible oil inatoa mafunzo kwa wakulima 3000 wa alizeti katika Mkoa wa Kagera na kwa mwaka huu mavuno yanatarajia kufikia tani 60 kipindi cha nyuma ilikua na makunsanyo ya tani 4. Pia wanatarajia kuwa na kiwanda cha kukamua mafuta ya alizeti ambacho kitakua chachu ya kilimo cha alizeti kwani wakulima watakua karibu na soko la mazao yao.
Tayari Gola Foundation na Kagera Edible Oil ina mkataba wa kufanya kazi kwa pamoja na kushirikiana katika masuala ya uwekezaji katika mkoa wa Kagera.
No comments:
Post a Comment