![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjiiEtAiJx_eETv1bJ5AwLmoLKnPj9hkkT9_n6wps6KGr0pcvO08cHUVPnWRQnmso4a1mzb3Z9V1BRUCc5d6rp0r6JeAQum3aWPqTjSdUXFRQUs6eLhAwUaXAjlTaslFi0s7H_dvp2R9VgL/s640/E86A5313.jpg)
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgJJcj_b7xqKKn1e_YFSUdvLWP3ArDub8pH-72lismNk7A7RaJA8FJzmYFqbsM1NE-onA_m8QjH_saow5P9tQ_qzTtHBA01PlwXDsJO0giad9BNqjzWVZX71eooemUGVawSfCRm8K0IWgkT/s640/E86A5248.jpg)
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjXwYvMdkHW0JFC-TqWNY_GFYyh7i6ne2tujkxF16i8cCE42xlD5lrpOY0lE7bGSPf_RwpVkv3kG5ZEQrKMHHsHyJ2eIKVi5nLrT-PzgeN3bPRtty5ULbEoDMnaafMZ9If3v3suWTdi27vf/s640/E86A5287.jpg)
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjqFgtO0JcusqBIja8glh94ylmwdcw5s2_pZcgjDngtQ1SCWZvf7V-lJL5CxgiHA7-Rad1rY6umaOq2TRaWJXvlnRgygTvCJ3nCAi1ScckZmI1jpWhAz1PbZoB4-h_LjvmzzAnAxb6i6psp/s640/E86A5255.jpg)
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiLroxsAgEUP2ou8hVIneIvQFgJ9EkCrjZu37mxTI5KMHdyP7UTcpwujsXrylQ4aJPJgvc7vjhFg1zv43ycaFjbSEnCA8N3PDv6BGHgrmCXTT9Qjpdcu7CDDAQQtJO8PAgnb5knia7reXbv/s640/E86A5281.jpg)
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgS7rAKsbOksFX2TY3uolhP6lmOTVb9yeECUbz6zHz7shDukScsuxpSUU_EvKCA5zXwViZ94TRx9GLNFf298geqJZCMpWy6Qs_zTHCfyQFHwi5tVSo84RjdaM_EK3OPOqZx1qezh9WS71Ki/s640/E86A5267.jpg)
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgg89R5Mmcj8npBgMz4cU0JqhlpBc5vkd43KvwT0ivhMF8D3azwa0mGY8UJDrVsaXyZAyeCTRvE7k6zpWIDPWLJmAYRdtxnwHjP3s8B5j2NuiZv-czfGV0FapuAk9pi0JQGlegCWwV4B11I/s640/E86A5361.jpg)
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEglCvWqHoUR2BIpCNf0AOI5m4w57SJKUk0z9irgG96iFCNZvzbmjeRhwEMrS95R_2_OfdcQ-wy2P2WEFXEBLzwW3gTDWZ1-vyJedI1IJNketEmPTz5N3YTmzt6AyxqewGA1bgU3RITrhL6k/s640/E86A5343.jpg)
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhRxLHx0lnvlBhroelOszLoxCRpyIG2dTQ6hweY80goUtxaB7GQQkz4gyY1sN56qv5cfimWS1jFj_VpJUVhB2HXEwqtxwML5VLy-TFLBcsPHlHPh5S6v1fJ4TBqdi0Fs706bAVnUM3l7Hxi/s640/E86A5406.jpg)
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhElCXInVzFAQ38BNca-meZdcLYasOST_s-OmYW5vc9VPRy-k5Vnl0Y7EtefaB7Xo-MG8JKwc4_ljUMkG4H_lemU2oFv9aNXqnODXWVFbfi-IpYWQdaY34Qm2smV0ARUThjwjbrCaRGO8M7/s640/E86A5384.jpg)
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjn5s0TIa_1-8N3dcyrxKegUEiml4yNt159ReJs_op2v4vol_TRzgrrEO-FTC5PbJniNxNAPqRbEkybI_-Olgoi0QFsCPTI3u6aaikCpn6klOY8vYm-2dKesVpL2tSeYYq4lTbwBJR2-bU3/s640/E86A5415.jpg)
ZAIDI ya Sh Bilioni 20 zimekusanywa kutoka kwa mashirika 40 yasiyo ya kiserikali pamoja na taasisi mbalimbali za serikali kwa ajili ya kusaidia katika kampeni za kupambana dhidi ya Virusi vya Ukimwi na Ukimwi ambapo tayari Mamilioni ya watanzania wamekwisha nufaika nazo.
Fedha hizo zimekusanywa kampuni ya Kuchimba dhahabu ya Geita (GGM) kupitia changamoto ya kupanda Mlima Kilimanjaro, ijulikanayo kama “Kili Challenge” tangu mwaka 2001 ilipoanzishwa ,mwaka huu ukiwa mwaka wa 17 ikishirikisha washiriki 70 watakao shiriki kupanda Mlima huku wengine wakizunguka mlima huo kwa kutumia Baiskeli .
Akizungumza wakati wa Hafla ya kuwaaga washiriki wa Programu ya Kili Challenge 20018 iliyofanyika katika lango la kupanda Mlima Kilimanjaro la Machame ,Makamu wa Rais wa GGM, Simon Shayo amesema Progaramu hiyo imepanua wigo wa kusaidia Taasisi zinazojikita kuhudumia wachimbaji wadogo wadogo pamoja na maeneo ya wavuvi ambako tafiti zinaonyesha wako kwenye mazingira hatarishi ya kuambukizwa VVU.
“Kila siku na kila mwaka ,tukio hili la hisani linaendelea kuwa na matokeo makubwa kwa jamii inayotuzunguka ,ninayo furaha leo kutagaza kwamba kupitia Kili Challenge tumeweza kuchangisha zaidi ya Bilioni 20 .”alisema Shayo.
Alisema fedha hizo zimekusanywa kutoka katika Mashirika 40 yasiyo ya kiserikali (N.G.O,S) pamoja na taasisi mbalimbali za serikali kupitia Tume ya taifa ya kudhibiti Ukimwi (TACAIDS) ambapo watanzania zaidi ya Milioni moja wamenufaika nayo.
Shayo alisema mbali na tukio hilo ,KAmpuni ya GGM imeendelea kuwekeza katika miradi ya kijamii ikiwemo ya Elimu,Afya,Maji na miundombinu ya barabara katika mkoa wa Geita na kwamba imetenga kiasi cha Sh Bil 9.2 kwa ajili ya huduma za jamii nah ii ni baada ya kuingia makubaliano na Wilaya ya Geita pamoja na Halmashauri yake.
Mgeni rasmi katika tukio hilo ,Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi,Vijana na Ajira ,Anthony Mavunde amesema Serikali ya Tanzania inajivunia jitihada hizi ambazo zinaonekana kuwa endelevu katika utafutaji wa raslimali za udhibiti wa UKIMWI nchini.
“Kama nilivyosema TACAIDS imekuwa ikishirikiana kwa karibu na GGM kuhakikisha jambo hili linatekelezwa kwa tafsiri ya kuoanisha Changamoto za mapambano dhidi ya UKIMWI na ugumu wa upandaji wa Mlima Kilimanjaro kupitia njia ngumu ya Machame na uzungukaji wa Mlima Kilimanjaro kwa baiskeli.”alisema Mavunde.
Hadi sasa zaidi ya Watu 700 kutoka duniani kote wameshiriki katika changamoto hiyo ya kihistoria ya upandaji Mlima kupitia programu ya “Kili Challenge” na kukusanya fedha ambazo zimesaidia maeneo mbalimbali yakiwemo makundi ya Wajane, Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI, Watoto yatima, Vijana, pamoja na Taasisi zinazotoa huduma muhimu za UKIMWI.
Aidha, Fedha hizi zimetumika kuboresha huduma za Hospitali mbalimbali nchini zikiwemo za Mkoa wa Geita na Kibong’oto Mkoani hapa na ujenzi wa Vituo vinne (4) vya maarifa kwenye njia kuu za usafirishaji.
No comments:
Post a Comment