Fursa ya kwanza ya uandaaji wa mashindano maarufu ya mbio za mbuzi imekua ya mafanikio kwa Klabu ya Rotary ya Oysterbay. Tukio hilo lenye burudani ya aina yake lilikwenda kwa Motto wa ‘Wakanda Goat are You’, na kuvuatia watu zaidi ya 4,500 waliokusanyika katika eneo la The Green, Oysterbay kwa ajili ya kushuhudia mashindano hayo.
Matukio muhimu yaliyofuata baada ya mbio hizo ni mchezo wa bahati nasibu ambao uliwezeshwa na wafadhili wa hapa nyumbani pamoja na gwaride la kuonyesha mavazi, ambapo watu mbalimbali walipata fursa ya kuonyesha mavazi yao aina ya Wakanda kwa kurejelea mafanikio ambayo muvi ya Marvel ya ‘Black Panther’ imeyapata kwa mwaka huu.
Ni mwaka wa kumi na nane mfululizo wa mashindano hayo lakini kwa mwaka wa kwanza chini ya Rotary Goat Races, tukio hili maarufu la kifamilia lilivutia maelfu ya watu siku ya tarehe 23 Juni. Tukio hilo likifanyika katika eneo la ‘The Green’ chini ya motto wa ‘Wakanda Goat are You”, wahudhuriaji walifurahia aina saba za mbio, vyakula vya aina mbalimbali vya hapa nyumbani, zawadi kubwa mbalimbali za bahati nasibu, michezo ya kuweka dau na gwaride la ushindani la mavazi ya Wakanda.
Mashindano hayo yalianza kwa mbuzi kusimama kwenye mstari wa mwanzo wa mashindano, huku watazamaji wakivuta pumzi kuona mbuzi wanavyopigania ushindi wa kuwa namba moja.
KAtika raundi ya kwanza Mbuzi aliyeibuka kidedea ni namba 8 ambapo zawadi yake ilidhaminiwa na Kampuni ya vinywaji ya CocaCola, Raundi ya pili mbuzi namba 7 aliibuka mshindi na zawadi yake kudhaminiwa na East Africa TV/Radio huku raundi ya tatu mbuzi namba tisa akikiibuka mshindi na zawadi yake kudhaminiwa na Kampuni ya Aggreko.
Wamiliki wa mbuzi hao walisherehekea ushindi huo kwa staili ya kipekee na watu ambao waliweka dau kwa mbuzi hao kushinda walipokea fedha zao za dau hilo. Katikati ya mbio hizo, michezo ya bahati nasibu kwa washindi wa zawadi kubwa pia ilifanyika na washiriki kadhaa kushinda. Watoto pamoja na watu wazima walipendezesha gwaride la mavazi na kujishindia zawadi kabambe kwa mavazi hayo. Ni wazi watoto walifanya vizuri zaidi kwenye kipengele hiki.
Viongozi wa mashindano ya mbio za mbuzi, Abdulrahman Hussein na Mathew Hellela walifurahishwa na mwitikio mkubwa wa watu.“Ni mara yetu ya kwanza kuandaa mashindano haya ya mbio za mbuzi na tunafuraha kuwa tukio hili limekuwa la kufana sana kwa kila mhudhuriaji na pia kwa watu kutuamini katika kuwapa kitu kikubwa na cha tofauti kwa mwaka huu”, alisema Abdulrahman Hussein.
"Pia inaonyesha kuwa timu yetu ya kujitolea, ambayo ilitumia mwezi mzima kuandaa tukio hili, ilikuwa kwenye njia sahihi na nguvu zao leo zimelipa kwa kuwapa wakati mzuri wahudhuriaji wote”, aliongeza Hussein.Kwa upande wake Mathew Hellela aliwashukuru wafadhili wote kwa imani na misaada yao.
"Tulikuwa wapya katika kuandaa tukio la namna hii na tunashukuru sana kwa imani ambayo wafadhili wametupatia sisi watu wa Klabu ya Rotary katika kufanya jambo lililo sahihi. Mwaka huu ulikuwa mwanzo mzuri na tunatarajia kubeba mafanikio haya kwa miaka ijayo ya mashindano ya mbio za mbuzi za Rotary ".
Anne Saels, Rais wa Klabu ya Rotary, Oysterbay alisema kuwa anajivunia sana timu yake na anasubiria kwa hamu kutekeleza miradi ya elimu ambayo Klabu yake itaifanyia kazi hivi karibuni, kwa kutumia mapato ya mbio hizo. Miradi hiyo itazingatia hasa masuala mbalimbali ya elimu kwa manufaa ya jamii.
Mashindano ya mbio za mbuzi kwa mwaka huu yamefadhiliwa na Resolution Insurance, SWISS, Toyota, Coca Cola, East Africa TV/Radio, Aggreko, SBL, Mastercard, Le Grand Casino na Red ‘n White. Michango ya ukarimu pia imetoka kwa JC Decaux, PM Group, Almar Containers TZ, SBS, Abstrat, The Slipway Hotel na Pizza Hut pamoja na Advertising Dar, ALAF-Safal Group, Britam Insurance, Selcom Paytech, VClick Professional Photography, WS Insight, Green Waste Pro na CAPS Limited.
Michezo ya bahati nasibu ilipewa nguvu na SWISS, SBL, The Sea Cliff Hotel, The Slipway Hote, Zen Spa, Engen, Coastal Airlines na 305 Karafuu Restaurant. Michango mingine ilitoka Kwa kampuni za:-Jumia, Advertising Dar, Splendid Cleaners, TAN Management – Insurance broker, Merrywater, Vet Care, Dar Signs, Karafuu Restaurant, Prime Advertising, Reader Rabbits, World Link.
Klabu ya Rotary ya Dar es Salaam Oysterbay ilianzishwa mwaka 2009 na hadi sasa ina wanachama 70. Ni klabu kubwa zaidi miongoni mwa Klabu nane za Rotary jijini Dar es Salaam na inasaidia jamii katika miradi mbalimbali ikiwemo: Mpango wa Afya ya Jamii ambao huandaa makambi ya matibabu ya mara mbili kwa mwaka kwa vijijini na mijini, mradi wa Vijana Poa wa kusaidia vijana wa chuo kikuu kupata kazi mbio za Rotary Dar, kusaidia kazi za hospitali ya CCBRT na Rotary Mission Green ambazo ni jitihada za wilaya za kupanda miti.
Zaidi ya hayo, Klabu ya Rotary ya Oysterbay kwa sasa inajenga Rotary Community Corps, mradi ambao umejikita katika kutoa msaada wa moja kwa moja kwa wanufaika katika jamii. Mapato yote ya mbio za Mbuzi za Rotary yatatumika kwenye miradi ya elimu ya Klabu ya Rotary ya Dar es Salaam Oyster Bay, kama mpango wa ufadhili wa elimu ambao unawasaidia wanafunzi wa Chuo Kikuu nchini Tanzania, nipe fagio na Shule ya Msingi Msasani.
Washiriki wa mashindano ya mbio za mbuzi wakiwa wamewabeba mbuzi wao tayari kushiriki mbio hizo wakati wa hafla ya mashindano hayo maarafu ambayo yaliyofanyika katika eneo la The Green, Oysterbay jijini Dar es Salaam wikiendi hii. Kwa mwaka huu mashindano hayo ya kufana yaliandaliwa na Klabu ya Rotary Dar es salaam, Oysterbay ambapo yalivutia zaidi ya watu 4,500 huku yakiwa chini ya Motto wa ‘Wakanda Goat Are You’? yakirejerelea mafanikio ambayo muvi ya Marvel ya ‘Black Panther’ imeyapata kwa mwaka huu.
Washiriki wa mashindano ya mbio za mbuzi wakiwakimbiza mbuzi wao wakati wa hafla ya mashindano hayo maarafu ambayo yaliyofanyika katika eneo la The Green, Oysterbay jijini Dar es Salaam wikiendi hii. Kwa mwaka huu mashindano hayo ya kufana yaliandaliwa na Klabu ya Rotary Dar es salaam, Oysterbay ambapo yalivutia zaidi ya watu 4,500 huku yakiwa chini ya Motto wa ‘Wakanda Goat Are You’? yakirejerelea mafanikio ambayo muvi ya Marvel ya ‘Black Panther’ imeyapata kwa mwaka huu.
Anne Saels, Rais wa Klabu ya Rotary Dar es salaam, Oysterbay akizungumza na waandishi wa habari wakati wa hafla ya mashindano ya mbio za mbuzi yaliyofanyika katika eneo la The Green, Oysterbay jijini Dar es Salaam wikiendi hii. Kwa mwaka huu mashindano hayo ya kufana yaliandaliwa na Klabu ya Rotary Dar es salaam, Oysterbay ambapo yalivutia zaidi ya watu 4,500 huku yakiwa chini ya Motto wa ‘Wakanda Goat Are You’? yakirejerelea mafanikio ambayo muvi ya Marvel ya ‘Black Panther’ imeyapata kwa mwaka huu.
Anne Saels, Rais wa Klabu ya Rotary Dar es salaam, Oysterbay akizungumza na waandishi wa habari wakati wa hafla ya mashindano ya mbio za mbuzi yaliyofanyika katika eneo la The Green, Oysterbay jijini Dar es Salaam wikiendi hii. Kwa mwaka huu mashindano hayo ya kufana yaliandaliwa na Klabu ya Rotary Dar es salaam, Oysterbay ambapo yalivutia zaidi ya watu 4,500 huku yakiwa chini ya Motto wa ‘Wakanda Goat Are You’? yakirejerelea mafanikio ambayo muvi ya Marvel ya ‘Black Panther’ imeyapata kwa mwaka huu.
Anne Saels, Rais wa Klabu ya Rotary Dar es salaam, Oysterbay akizungumza na waandishi wa habari wakati wa hafla ya mashindano ya mbio za mbuzi yaliyofanyika katika eneo la The Green, Oysterbay jijini Dar es Salaam wikiendi hii. Kwa mwaka huu mashindano hayo ya kufana yaliandaliwa na Klabu ya Rotary Dar es salaam, Oysterbay ambapo yalivutia zaidi ya watu 4,500 huku yakiwa chini ya Motto wa ‘Wakanda Goat Are You’? yakirejerelea mafanikio ambayo muvi ya Marvel ya ‘Black Panther’ imeyapata kwa mwaka huu.
No comments:
Post a Comment