Wednesday, May 2, 2018

Wito kwa jamii kuondokana na mila potofu,Jamii yaaswa kupeana elimu

Naibu Mkurugenzi wa Kampuni ya Simu Halotel Bwana Trieu Thanh Binh na baadhi ya wafanyakazi wa kampuni hiyo wakikabidhi msaada wa mahitaji mbalimbali ya Kijamii kwa baadhi wa wauguzi leo wakati wafanyakazi wa kampuni hiyo walipowatembelea watoto walioko katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) na kuwapelekea mahitaji hayo.
Naibu Mkurugenzi wa Kampuni ya Simu Halotel Bwana Trieu Thanh Binh akikabidhi msaada wa mahitaji mbalimbali ya kijamii yenye kwa baadhi wa wauguzi leo wakati wafanyakazi wa kampuni hiyo walipowatembelea watoto walioko katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) na kuwapelekea mahitaji 
Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Simu Halotel Stella Pius akikabidhi moja ya msaada wa mahitaji mbalimbali ya kijamii kwa mmoja wa wazazi wakati wafanyakazi wa kampuni hiyo walipowatembelea watoto walioko katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI)na kuwapelekea mahitaji hayo.

Kuwepo kwa mila potofu katika jamii ya watanzania ni moja na ya jambo ambalo limekuwa ni kikwazo katika juhudi mbalimbali zinazofanywa na serikali pamoja na taasisi mbalimbali za kijamii katika kupunguza au kutokomeza kabisa matatizo ya kiafya ambayo huwapata watoto wachanga wanaozaliwa na walio na umri chini ya miaka mitano.

Watoto wengi katika rika hilo huwa katika athari ya kuzaliwa au kupata magonjwa ambayo ni kuwa na vichwa maji, pamoja na mgongo wazi, ikiwa ni magonjwa ambayo huweza kuepukwa endapo tu jamii nzima ya watanzania wataweza kupatiwa elimu sahihi ya namna ya kuepuka au kuzuia magonjwa hayo na endapo kutabainika watoto wenye matatizo hayo jamii isiweze kuwaficha kutokana na imani potofu.

Hayo yamebainishwa na Daktari bingwa wa magonjwa ya upasuaji katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) Bwana Laurent Lemeri Mchome, wakati akiongea na waandishi wa habari baada ya wafanyakazi wa kampuni ya simu ya Halotel walipowatembelea watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi pamoja na wazazi/walezi wao waliolazwa katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) kwa ajili ya kuwapa mahitaji mbalimbali ya kijamii kama sehemu ya msaada wao kama wafanyakazi. 

“Akiongea baada ya kukabidhiwa msaada huo, kwa niaba ya madaktari na wauguzi wodini hapo Dr Laurent Mchome amesema kila mwaka Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) tumekuwa tukitoa matibabu kwa wagonjwa zaidi ya 350 nchi nzima kupitia kampeni ya watoto wenye vichwa maji na mgongo wazi. Pia tumekuwa tukiweka kambi ya kutibu watoto kila mkoa kwa kila kanda nchini na changamoto kubwa ni kwamba jamii kubwa ya watanzania hawana elimu ya kutosha kuhusu magoinjwa haya kuwa yanatiwa na watoto hupona kabisa”.

“Naomba nitoe wito kwa jamii hasa kwa wale ambao wanafahamu kuhusu ugonjwa wa vichwa maji na mgongo wazi wanapoona jamii ambayo ina watoto wenye matatizo haya wasiogope bali wawape ushauri kuwaleta hospitali kwasababau matibau yanafanyika na watoto wanapona kabisa” Aliongeza Dr Mchome. 

Akizungumza wakati wa kukabidhi mahitaji hayo Naibu Mkurugenzi wa Kampuni ya Halotel. Bwana Trieu Thanh Binh amesema kuwa katika kuhakikisha tunasaidia sekta hii ya afya nchini, tumeona ni vyema kuja kuwatembelea watoto hawa na kujumuika nao siku hii ya leo kwa kuwapa misaada hii ya kijamii ambayo ambapo nimwendelezo wa kampeni ya kusaidia jamii yenye uhitaji, ili waweze kuimarika katika afya yao wanapoendelea kupata matibabu wodini hapa. Hii ni pamoja ya kuonesha upendo kwao na kutambua thamani yao katika jamii ya watanzania.

“Tunatambua changamoto mbalimbali ambazo ziko katika kuwapa matibabu watoto wenye matatizo ya vichwa vikubwa na mgongo wazi wawapo wodini wakisubiri wakisubiri kupata matibabu upasuaji hivyo nitoe wito kwa taasisi zingine mbalimbali, makampuni na watu binafsi kuweza kujitolea na kuwasaidia mahitaji mbaliambali ikiwa ni katika kujali na kutambua thamani ya afya yao aliongeza bwana Binh.”

Kwa upande wa Uongozi wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa (MOI) , Afisa Uhusiano Bwana Patrick Mvungi alisema “ Tumefarijika sana kwa kupokea msaada huu kutoka Kampuni ya simu ya Halotel na wafanyakazi wake, tunawashukuru sana kwa kuthamini afya za watoto hawa lakini pia kwa kuunga mkono jitihada za kuisaidia sekta ya afya nchini. Hii ni hatua mpya na kubwa kwetu sisi katika kuimarisha ushirikiano wetu na Halotel kwa kiwango cha juu hasa katika kuboresha sekta ya afya kwa ujumla”.

Licha ya kampuni ya simu ya Halotel kupiga hatua kubwa katika kusambaza huduma za mawasiliano na kutoa huduma zenye ubora wa hali ya juu nchini nzima, kampuni hii imekuwa ikijihusisha na kutoa misaada mbalimbali kwa jamii ya watanzania. Hii ni katika kuonesha jinsi inavyothamini na kujali jamii ya watanzania kwa nyanja mbalimbali, ikiwemo kuboresha sekta ya afya na elimu kama moja ya kipaumbele cha kampuni ya hii kwa maendeleo ya watanzania na nchi kwa ujumla.

No comments: