Waziri
wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage, akimkabidhi Tuzo
ya Mshindi wa pili wawakilishi wa Kampuni ya PLASCO Ltd, kutoka
(kushoto) Unguu Sulay, Edith James na Alimiya Osman, wakati wa hafla ya
Tuzo za 13 za Rais za Viwandani, (PMAYA) iliyofanyika kwenye Hoteli ya
Serena jijini Dar es Salaam, leo mchana. Picha zote na Muhidin Sufiani
(MAFOTO)
Waziri
wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage, (wa pili kulia)
akisikiliza maelezo kutoka kwa Mshirika wa Taasisi ya Kaizen Tanzania,
James Alva, wakati alipotembelea mabanda ya maonyesho katika hafla ya
utoaji Tuzo za 13 za Rais za Viwandani, (PMAYA) iliyofanyika kwenye
Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Waziri
wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage, akimkabidhi Tuzo ya
Mshindi wa jumla Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia Tanzania TBL
Group, Roberto Jarrin, wakati wa hafla ya Tuzo za 13 za Rais za
Viwandani, (PMAYA) iliyofanyika kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es
Salaam.
WAZIRI
wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage, akimkabidhi Tuzo ya
Mshindi wa kwanza katika Makampuni matatu makubwa (TOP 3) Meneja wa
Kampuni ya Bia ya Serengeti, Helene Weesie, wakati wa hafla ya Tuzo za
13 za Rais za Viwandani, (PMAYA) iliyofanyika kwenye Hoteli ya Serena
jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB,
Charles Kimei.
Waziri
wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage, akimkabidhi
Tuzo Meneja Rasilimali watu wa Kampuni ya Alaf Tanzania, Daphne
Kakonge, wakati wa hafla ya utoaji tuzo za Rais za Viwandani.
Afisa Masoko wa Kampuni ya Alaf Tanzania, Theresia Mmasy, akipokea cheti cha shukrani wakati wa hafla hiyo.
Waziri
wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage, akimkabidhi Cheti
cha kutambua mchango wa udhamini mwakilishi wa Kampuni ya IPP, Paul
Urio, wakati wa hafla ya Tuzo za 13 za Rais za Viwandani, (PMAYA)
iliyofanyika kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam
Waziri
wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage, akimkabidhi Cheti
cha kutambua mchango wa udhamini Mwenyekiti wa Kampuni ya Montage,
Nestory Mapunda, wakati wa hafla ya utoaji Tuzo za 13 za Rais za
Viwandani, (PMAYA) iliyofanyika kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es
Salaam
Na Muhidin Sufiani, Dar
WAZIRI
wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage amesema kuwa azma ya
kukua kwa uchumi unategemea sekta ya viwanda na hakuna budi kuhakikisha
wanatimiza vigezo vya uchumi ili ukue kwa asilimia 12 kwa mwaka, pato la
taifa lisipungue chini ya asilimia 15 na ajira kuongeza kwa asilimia 40
ya ajira zote.
Mwijage
amesema hayo wakati wautoaji tuzo za Rais za Viwandani (PMAYA) kwa
mwaka 2017 zilizofanyika leo Jijini Dar es salaam na kuwataka Shirikisho
la Viwanda (CTI) kuwa wabunifu na kuzitangaza bidhaa zao ili kuweza
kuingiza mapato ya asilimia 25 ya fedha za kigeni.
Akizungumza
wakati wa utoaji tuzo hizo, Mwijage amesema kuwa serikali ya awamu ya
tano toka iingie madarakani imeweza kuendelea kuboresha mazingira ya
kufanya biashara na kuwezesha kuvutia wawekezaji wa ndani na nje ya
nchi.
"Mpaka
sasa toka Desemba 2015 tayari tumewahamasisha wawekezaji wa ndani na wa
kujenga viwanda vipya 3,306 na tunawapongeza wawekezaji wa ndani nannje
kwa kuchagua kuwekeza Tanzania na kuunga mkono serikali yetu ya kukuza
uchumi wa viwanda kufikia 2025, " amesema Mwijage.
"
Natambua kuwa baadhi yenu mna madai mbalimbali ya kurejeshewa malipo
yenu yakiwemo ya ushuru wa forodha ya 15% ya ziafa kwenye uaguzaji wa
sukari kwa ajili ya matumizi ya viwanda na malipo ya marejesho ya
ongezeko la thamani,"
Mwijage
amesema zipo changamoto zinazotokana na wenye viwanda wenyewe ikiwemo
udhaifu wa kutafuta masoko ya ndani na nje ya nchi ya Tanzania
unasababisha bidhaa za ndani kutokufahamika vizuti miongoni mwa
watanzania na watuamiaji wa nje.
Mwijage
amesema kupitia baraza la Taifa la Uwekezaji Wananchi Kiuchumi (NEEC)
itahakikisha watanzania wote wanashiriki katika ujenzi wa uchumi.
Serikali kupitia baraza la uwezeshaji lina miradi ya kimkakati ya
kusaidia viwanda vyetu na watanzania kwa ujumla kupata fursa mbalimbali
zilizopo.
Kwa
upande wa Mwenyekiti wa CTI Dkt. Samwel Nyantahe ameishukuru serikali
kwa kuweka mijadala ya kuwasaidia watanzania wafanyabiashara hasa wenye
viwanda na baada ya serikali ya awamu ya tano kuja na sera ya ujenzi wa
viwanda watanzania wengi wamejitokeza kuanzisha viwanda mbalimbali kwa
azma ya kuunga mkono juhudi za Rais wa awamu ya tano ya kujenga uchumi
wa viwanda.
Aidha
ameeleza kuwa katika maadhimisho ya miaka 13 katika utoaji wa tuzo
mwaka 2016 mheshimiwa Rais alipendekeza kuhusisha sekta zote na wasio
wanachama wahusishwe na tuzo ya matumizi bora nishati viwandani
ilianzishwa.
Mashindano
hayo yataleta ushindani mkubwa katika sekta ya viwanda hali
itakayopelekea kukuwa kwa uchumi na kuongeza pato la taifa.
Katika
tuzo za mwaka 2017 kampuni ya bia ya Tanzania Breweries (TBL) iliweza
kupata ushindi wa jumla katika viwanda vyote vinavyozalisha bidhaa
mbalimbali wakifuatiwa na Zenufa na mshindi wa tatu ni Plasco Ltd
KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA
Waziri
wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage, akimkabidhi Tuzo,
CEO wa Kampuni ya Jambo Plastics Ltd, Rupa Suchack.
Waziri
wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage, akimkabidhi cheti
Mshirika wa Taasisi ya Kaizen Tanzania, James Alva na msidizi wake
Beatrice Kithinji, wakati wa hafla hiyo.
Wasnii wa Kikundi cha Sanaa cha Safi Theatre wakitoa burudani
No comments:
Post a Comment