Friday, May 4, 2018

WAZIRI MAHIGA NA WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA UJERUMANI WAKUTANA KWA MAZUNGUMZO RASMI

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga (kulia) akiwa ameongozana na mgeni wake Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani, Mhe. Heiko Maas alipowasili kwenye Kituo cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) kwa ajili ya kufanya mazungumzo rasmi ya ushirikiano kati ya Tanzania na Ujerumani. Mhe. Waziri Maas yupo nchini kwa ziara ya kikazi ya siku mbili kuanzia tarehe 03 hadi 04 Mei, 2018 
Mhe. Waziri Mahiga akimkaribisha rasmi nchini Mhe. Waziri Maas 
Mhe. Waziri Maas akisaini Kitabu cha Wageni alipowasili JNICC huku Waziri Mahiga akishuhudia 
Mhe. Waziri Mahiga akiongoza ujumbe wa Tanzania kwenye mazungumzo rasmi kati ya Tanzania na Ujerumani. Kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Zanzibar, Mhe. Issa Haji Gavu, kushoto kwa Mhe. Mahiga ni Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Bw. Geoffrey Mwambe akifuatiwa na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Jestas Nyamanga. 
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani, Mhe. Heiko Maas akiongoza ujumbe wa Ujerumani kwenye mazungumzo kati ya nchi hiyo na Tanzania. Kulia kwake ni Balozi wa Ujerumani nchini, Mhe. Detlef Waechter 
Mazunguzmo rasmi kati ya Mhe. Waziri Mahiga na Mhe. Waziri Maas yakiendelea 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga (kulia kwa pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani, Mhe. Heiko Maas wakimsikiliza Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Mindi Kasiga alipokuwa akitoa utaratibu kuhusu mkutano kati ya Mawaziri hao na Waandishi wa Habari (Joint Press Conference) uliofanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) kuhusu madhumuni ya ziara ya Waziri Maas nchini 
Mhe. Waziri Mahiga kwa pamoja na Mhe. Waziri Maas wakizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu mazungumzo kati yao ambayo yalijikita katika kuimarisha ushirikiano wa kihistoria uliopo pamoja na kuboresha maeneo mbalimbali ya ushirikiano ikiwa ni pamoja na uwekezaji, biashara, kupambana na rushwa na biashara haramu ya madawa ya kulevya na usafirishaji binadamu pamoja na kupambana na ujangili wa wanyamapori. 
Sehemu ya Waandishi wa Habari na Viongozi kutoka Serikalini wakifuatilia mkutano kati yao na Mhe. Waziri Mahiga na Mhe. Waziri Maas ambao hawapo pichani. 
Mhe. Waziri Maas pia alipata fursa ya kutembelea Shule ya Sekondari ya Majaribio ya Chnag'ombe ambayo ni miongoni mwa shule chache nchini zinazofundisha Lugha ya Kijerumani. Pichani akiwa na wanafunzi wanaojifunza lugha hiyo shuleni hapo 
Mmoja wa wanafunzi shuleni hapo akimzawadia Mhe. Maas picha ya kuchora ya Hifandhi ya Mlima Kilimanjaro 
Mhe. Maas akiwa na mmoja wa walimu (mwenye kitambulisho) wanaofundisha Lugha ya Kijerumani katika Shule ya Sekondari ya Majaribio ya Chang'ombe 

No comments: