Wednesday, May 9, 2018

TAPSEA KUFANYA MKUTANO MKUU ZANZIBAR

Na Ali Issa, Maelezo Zanzibar  
Makatibu Mahsusi wa Taasisi za Serikali na Watu Binafsi Wametakiwa Kufanya Kazi zao Kwa Kufuata Sheria na maadili ya kazi hiyo kama zinavyo waelekeza ili kuleta ufanisi katika kazi.

Hayo yamesemwa Katika Hoteli Ya Mansoon Shangani na Mwenyekiti wa chama cha Makatibu Mahsusi Tanzania (TAPSEA) Zuhura Songambele Maganga wakati alipokuwa akizungumza na wandishi wa habari kuhusu mkutano Mkuu wa sita wa Chama hicho utakao fanyika chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar kampasi ya Tunguu.

Amesema kumekuwa na malalamiko juu ya makatibu mahsusi kufanyakazi kinyume na maadili ya kazi zao hivyo mkutano huo mkuu utaoaza  kesho utaelekeza majukumu ya makatibu mahsusi wanavyotakiwa kutekeleza kazi kwa kufuata maadili ya kazi zao na mamlaka anayoifanyia kazi.

Aidha alisema kuwa makatibu hao wataelekezwa kufanya wajubu wao kwa kuthamini utaifa wao kwa malengo ya kuweka mbele maslahi ya nchi katika utoaji huduma bora kwa jamii.

“lengo la chama chetu mwaka huu ni kukuza taaluma, kudumisha uwajibikaji na kuinuwa hadhi ya taaluma ya katibu muhsusi kitaifa kimataifa,na kusaidia kudumisha utoaji huduma bora katika jamii” alisisitiza mwenyikiti TAPSEA.

Mwenyekiti huyo amesema tangu kuazishwa chama hicho cha makatibu mahsusi kumekuwa na maendeleo yaliyopatikana ikiwa ni pamoja na kuwaunganisha makatibu mahsusi wa Tanzania kupitia mikutano yao kwa kuwapa taaluma na kubadilishana uzowefu.

Faida nyengine amesema wamefanikiwa kushawishi na kukubaliwa kuazishwa shahada ya uhazili katika chuo cha utumishi wa umma Tanzania bara baada ya maombi ya muda mrefu.

Aidha amesema wamefanikiwa kununua kiwanja kwa ajili ya kujenga ofisi ya TAPSEA Makao makuu ya serikali Dodoma na kushughulikia malalamiko yanayo pelekwa wanachama na kuyapatia ufumbuzi

Nae mwakilishi wa Chama cha Makatibu mahsusi upande wa Zanzibar Zainabu Ibrahimu aliwataka wafanyakazi wa kada hiyo kujiunga na chama chao kwani kunafaida kubwa wakati wa utumishi wao baada ya kkustaafu kwa kupata ruzuku za utumishi wake iwapo atakuwa mwanachama hai.  
 Mwenyekiti wa chama cha Makatibu Mahsusi Tanzania  (TPSEA) Zuhura Songambele Maganga  akizungumza na waandishi wa habari katika Hoteli ya Mazsons Shangani kuhusu kufanyika mkutano wa sita wa Chama hicho unaoanza tarehe 10.5.2018 katika Ukumbi wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar Kempasi ya Tunguu.
Mwakilishi wa Chama cha Makatibu Mahsusi Tanzania upande wa Zanzibar, Zainab Ibrahim  akieleza kuimarika kwa  chama hicho kwa upande wa Zanzibar katika mkutano  wa waandishi wa habari uliofanyika Hoteli ya Mazsons Shangani.

No comments: