SHIRIKISHO
la Riadha Tanzania (RT), limempongeza Mkurugenzi wa MultiChoice
Tanzania, Maharage Chande kwa kuteuliwa kuwa Mkurugenzi mpya wa
MultiChoice Kanda ya Afrika Mashariki na Magharibi.
Mei 20 mwaka huu, Kampuni ya
MultiChoice Africa Limited, ilithibitisha uteuzi wa Wakurugenzi wawili,
ambako Mtanzania Maharage Chande ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa
MultiChoice Tanzania, anakuwa Mkurugenzi mpya wa Kanda ya Afrika
Mashariki na Magharibi.
Uteuzi
huo uliotangazwa na Ofisa Mtendaji Mkuu wa MultiChoice Africa, Brand de
Villiers, unabainisha kuwa Maharage anachukua nafasi ya Stephen Isaboke
aliyekuwa Mkurugenzi wa Kanda ya Afrika Mashariki ambaye sasa anakuwa
Mkuu wa Mamlaka (Group Executive Head of Regulatory). Uteuzi ambao
unaanza Juni Mosi mwaka huu.
Ofisa
Mtendaji Mkuu wa MultiChoice Africa, Brand de Villiers, amesema uteuzi
wa Maharage umezingatia uwezo na upeo wake mkubwa aliyouonyesha katika
kipindi alipoiongoza MultiChoice Tanzania tangu alipojiunga nayo Juni
2016.
Rais
wa RT, Anthony Mtaka, amesema familia ya Riadha Tanzania imepokea kwa
furaha uteuzi huo wa Maharage, hasa ukizingatia katika uongozi wake,
MultiChoice Tanzania kupitia DStv, imekuwa mshirika mkubwa katika
kuchangia maendeleo ya mchezo wa Riadha hapa nchini.
“Sisi
kama Riadha Tanzania, tumepokea kwa faraja kubwa kupanda kwa cheo kwa
Mtanzania mwenzetu Maharage Chande, hakika tutamkumbuka kwa mengi katika
kusapoti maendeleo ya Riadha hapa nchini….Tunamtakia kila la heri
katika majukumu yake mapya na bila shaka mapenzi yake katika mchezo wa
Riadha atayaendeleza,” alisema Mtaka ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa
Simiyu.
Mtaka,
alibainisha baadhi ya mchango wa MultiChoice Tanzania chini ya Maharage
katika Riadha Tanzania, ni kutayarisha timu na wachezaji wa Riadha
katika mashindano mbalimbali.
“Ni
uthubutu wa Mkurugenzi Mtendaji Maharage Chande aliamua kumdhamini
Mwanariadha Alphonce Felix Simbu baada ya mashindano ya Olimpiki Rio de
Jeneiro Brazil alipoibuka namba 5 na hatimaye kuja akiwa namba 3 katika
mashindano makubwa ya Dunia huko London 2017.
“Maharage
akiwa Mtendaji Mkuu wa MultiChoice Tanzania, ameendelea kuunga mkono
Timu ya Riadha Tanzania ambapo mwaka huu kampuni yake ilitoa fedha za
maandalizi kwa ajili ya mashindano ya Jumuiya ya Madola,” alisema Mtaka
na kuongeza.
Na
hivi majuzi Maharage amempa udhamini mchezaji mwingine wa Riadha ili
aweze kufanya maandalizi ya mashindano ya Dunia yatakayofanyika nchini
Qatar 2019.
“Ukiacha
hilo, MultiChoice Tanzania pia ilikuwa bega kwa bega na RT katika
kuimarisha ushirikiano wa wanafamilia ya Riadha na Wadau wake wakiwamo
waandaaji wa matukio mbalimbali ya mchezo wa Riadha,” alisema Mtaka na
kuongeza.
Sisi
kama Riadha Tanzania tunampongeza na kumtakia heri katika majukumu yake
tukiamini heshima ya nchi yetu Tanzania katika kampuni hii kubwa
duniani itaendelea kuaminika na kuheshimika, na zaidi sisi kama familia
ya Riadha tunaahidi kuendelea kuwa mabalozi wazuri wa MultiChoice
Tanzania.
No comments:
Post a Comment