Rais wa Klabu ya Rotary Dar es Salaam, Oysterbay, Anne Saels (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya kutangaza nia ya klabu hiyo kuendeleza mashindano hayo kwa mwaka 2018. Chini ya chapa mpya ya ‘The Rotary Goat Races’, mashindano hayo kwa mwaka huu yatafanyika tarehe 23 Juni katika eneo la ‘The Green’ Oysterbay jijini Dar es Salaam. Anayeshuhudia (kulia) ni Mwenyekiti wa Bodi ya mashindano ya mbio za mbuzi za Rotary, Amish Shah.
Mwenyekiti wa Bodi ya mashindano ya mbio za mbuzi za Rotary, Amish Shah (katikati) akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya kutangaza nia ya klabu hiyo kuendeleza mashindano hayo kwa mwaka 2018. Chini ya chapa mpya ya ‘The Rotary Goat Races’ mashindano hayo kwa mwaka huu yatafanyika tarehe 23 Juni katika eneo la ‘The Green’ Oysterbay jijini Dar es Salaam. Pamoja nae kulia ni Rais wa Klabu ya Rotary Dar es Salaam, Oysterbay, Anne Saels na Mkuu wa kamati ya maandalizi, Mathew Helela(kulia).
Mwenyekiti wa Bodi ya mashindano ya mbio za mbuzi za Rotary, Amish Shah akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya kutangaza dhumuni la klabu hiyo kuendeleza mashindano hayo kwa mwaka 2018. Chini ya chapa mpya ya ‘The Rotary Goat Races’ mashindano hayo kwa mwaka huu yatafanyika tarehe 23 Juni katika eneo la ‘The Green’ Oysterbay jijini Dar es Salaam. Kulia Mkuu wa kamati ya maandalizi, Mathew Helela.
Mkuu wa kamati ya maandalizi, Mathew Helela akizungumza jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa hafla ya kutangazwa kurudi kwa mashindano ya mbio za Mbuzi leo jijini Dar es salaam. Pamoja nae, kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya mashindano ya mbio za mbuzi za Rotary, Amish na Rais wa Klabu ya Rotary Dar es Salaam, Oysterbay, Anne Saels.
Mwenyekiti wa Bodi ya mashindano ya mbio za mbuzi za Rotary, Amish akifurahia jambo na Rais wa Klabu ya Rotary Dar es Salaam, Oysterbay, Anne Saels.
Dar es Salaam, 09 Mei 2018. Mashindano maarufu ya hisani ya mbio za mbuzi jijini Dar es salaam yanatarajiwa kuendelea mwaka huu. Baada ya tangazo la mwaka jana la kamati iliyokuwa ikiandaa mashindano hayo kuamua kusitisha michuano hiyo maarufu ya hisani, Klabu ya Rotary ya Dar es Salaam, Oysterbay imeamua kuendelea na uandaaji wa mashindano hayo kuanzia sasa. Waandaji hao wapya wataendelea na utaratibu uleule wa mashindano, huku wakitarajia kuwavutia mashabiki wengi wapya pamoja na wale mashabiki wa siku zote wa mbio hizo.
Katika kipindi cha miaka 17 iliyopita, ‘Dar es salaam Charity Goat Races’ ilikuwa ni moja ya tukio kuu katika kalenda ya matukio ya kila mwaka na moja ya matukio makuu ya hisani hapa jijini. Uamuzi wa kamati ya watangulizi ya uandaaji wa mashindano hayo ya kutoendelea nayo uliwafanya mashabiki wengi kuvunjika moyo.
Baada ya majadiliano ya kina na watangulizi hao, Klabu ya Rotary ya Dar es salaam, Oysterbay iliamua kuendelea na mashindano hayo. Kupitia chapa yake mpya ya “The Rotary Goat Races,” mashindano ya mwaka huu yatafanyika Juni 23, eneo la ‘The Green’ Oysterbay jijini Dar es Salaam, yakitegemea kutumia rasilimali za mwanzo zilizotumiwa katika michuano iliyopita. Tukio hilo litakuwa ni la kiburudani na kifamilia na mapato yake yataelekezwa kwenye miradi ya hisani.
Tofauti na miaka ya nyuma, mapato ya ‘Rotary Goat Races’ hayatapelekwa kwenye mashirika mbalimbali yanayopokea misaada bali yatatumika kwa ajili ya miradi binafsi ya utoaji huduma ya Klabu ya Rotary Dar es salaam, Oysterbay. Miradi hiyo itazingatia hasa masuala mbalimbali ya elimu kwa manufaa ya jamii.
"Kimataifa, Rotary na vilabu vyake wana sifa ya kufanya kazi kwa ufanisi kwa kupitia wanachama wake wa kujitolea, wakielekeza karibia asilimia mia ya fedha zote za miradi kwa walengwa”, alisema raisi wa sasa wa Klabu ya Rotary Dar es salaam, Oysterbay, Anne Saels. “Tunaamini kwamba kupitia miradi ya elimu iliyopangwa tunaweza kuleta tofauti kubwa kwenye maisha ya watu katika jamii na tunafuraha kuwa mashindano ya mbio za mbuzi za Rotary yatakuwa na jukumu muhimu katika kukamilisha hili”.
Mwenyekiti wa bodi ya mashindano ya mbio za mbuzi za Rotary, Amish Shah anaamini kuwa mashindano hayo kwa mwaka huu hayatawaangusha mashabiki. “Kwa motto ya ‘Wakanda Goat Are You’,tukikumbuka muvi iliyofanya vizuri kwa mwaka huu ya ‘Black Panther’, tunatumai kuwavutia mashabiki wapya na wadau wa mbio za mbuzi vilevile”,aliongea mwenyekiti huyo.
Kama ilivyokuwa kwa miaka iliyopita, mashindano ya mbio za mbuzi ya Rotary kwa mwaka 2018 yamefanikiwa kuvutia wadhamini wakuu kama vile Toyota, Swiss International Airlines na Coca Cola. Tunashukuru kwa imani ya wadhamini wetu katika shirika letu na tunaamini kuwa mashindano ya mbio za mbuzi ya Rotary kwa mwaka 2018 yatakuwa ya burudani kwa kila mmoja”.
Klabu ya Rotary ya Dar es Salaam Oysterbay ilianzishwa mwaka 2009 na hadi sasa ina wanachama 70. Ni klabu kubwa zaidi miongoni mwa Klabu za Rotary nane jijini Dar es Salaam na inasaidia jamii katika miradi mbalimbali ikiwemo: Mpango wa Afya ya Jamii ambao huandaa makambi ya matibabu ya mara mbili kwa mwaka kwa vijijini na mijini, mradi wa Vijana Poa wa kusaidia vijana wa chuo kikuu kupata kazi , mbio za Rotary Dar, kusaidia kazi za hospitali ya CCBRT na Rotary Mission Green ambazo ni jitihada za kwenye wilaya za kupanda miti. Zaidi ya hayo, Klabu ya Rotary ya Oysterbay kwa sasa inajenga Rotary Community Corps, mradi ambao umejikita katika kutoa msaada wa moja kwa moja kwa wanufaika katika jamii.
No comments:
Post a Comment