Saturday, April 28, 2018

UBALOZI WA KUWAIT NCHINI WAKABIDHI VIFAA KUSAIDA WENYE MAHITAJI KWA HUMANITY ACTIONS FOR CHILDREN FOUNDATION


Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

UBALOZI wa Kuwait nchini Tanzania umekabidhi vifaa mbalimbali viwakimo vya watu wenye ulemavu wa ngozi kwa Taasisi ya Humanity Actions for Children Foundation ambayo imekuwa ikijihusisha kutoa huduma kwa watoto wenye mahitaji maalumu.

Baadhi ya vifaa hivyo ni viti maalumu vya kusaidia wenye ulemavu ‘wheelchair’ 15, magongo 20, kofia za kujikinga na jua 40 na fimbo maalumu 30 kwa ajili ya watu  wasioona.

Akizungumza wakati wa tukio hilo la taasisi hiyo kukabidhiwa vifaa hivyo, Katibu wa kwanza wa Ubalozi wa Kuwait nchini Mohammad Alamiri, amefafanua msaada huo umetokana na mapenzi mema ya ubalozi huo kwa watu wenye ulemavu nchini Tanzania na kuahidi kuendelea kutoa kwa wenye uhitaji.

"Kwa kipindi cha miaka mitatu, Kuwait imekuwa na utaratibu wa kuzisaidia taasisi mbalimbali zilizopo katika mfumo wake, kwa kuzipatia misaada mbalimbali kwa ajili ya kupunguza changamoto zinazowapata watu wenye ulemavu na mahitaji maalumu waliopo nchini,"amesema.

Ameongeza ubalozi wao umekuwa na utaratibu huo unaolenga kuhakikisha watu wenye mahitaji maalumu, wakiwemo walemavu wa ngozi(Albino) watu wasioona na wengineo wenye matatizo ya kutembea wanafaidika na misaada ambapo tayari Sh.bilioni 1.1 
zimetumika katika mpango huo.

Amezitaka taasisi zote ambazo zinapata misaada kwa ajili ya kuwasaidia wenye mahitaji kuhakikisha wanafikisha kwa walengwa na kueleza makubaliano ya ubalozi huo na taasisi wanazozipatia misaada hiyo moja ni baada ya kujiridhisha wana moyo wa kusaidia jamii kama ambavyo wanaridhishwa na taasisi hiyo.

Wakati huohuo Katibu Mkuu wa Chama cha Albino Tanzania Mohammed Chanzi, ametumia nafasi hiyo kuzikumbusha taasisi kuhakikisha wanafikisa misaada kwa walegwa badala ya kupokea na kubaki nayo.

Amesema kupokea msaada ni jambo moja lakini kuufikisha unakokwenda ni jambo la pili na hivyo ametoa rai kwa taasisi na mashiriki pindi yanapopewa misaada basi iwe inafika na kupongeza taasisi hiyo kwa uaminifu wao ambao umesababisha Ubalozi wa Kuwait kuwa karibu nao na kusaidia jamii ya Watanzania.

Amesema kwa kufanya hivyo anaamini kutaendelea kuwavutia wadau mbalimbali, zikiwemo balozi zingine kujitokeza na kutoa misaada hiyo na hivyo kuwanufahisha walengwa kulingana na mahitaji yao.

Naye Mkurugenzi Mwazilishi wa taasisi ya kuhudumia watoto wenye shida mbalimbali cha Humanity Actions for Children Foundation Rahma Abdallah pamoja na kuushukuru ubalozi wa Kuwait kwa misaada hiyo, amesema tayari ofisi yake imeweka utaratibu wa kuigawa misaada hiyo kwa walengwa wakati wowote kuanzia wiki ijayo.

Amesema kuanzishwa kwa taasisi hiyo, zaidi kulilenga kuhakikisha mtoto na watu  wenye matatizo mbalimbali wakiwemo walemavu  wanapata huduma mbalimbali kulingana na mahitaji yao.

Mwenyekiti wa Humanity Actions for Children Foundation Rashid Mchujuiko  amelezea kufurahishwa na msaada huo wa Ubalozi wa Kuwait ambapo naye amesisitiza lazima vifaa hivyo vifike kwa walengwa na itakuwa ni tukio la wazi ili umma ujue.
 Katibu wa Kwanza wa Ubalozi wa Kuwait nchini Tanzania Mohammad Alamiri akikabidhi kiti  maalum cha walemavu kwa Taasisi ya Humanity Actions for Children Foundation leo jijini Dar es Salaam .Kulia kwake ni Mkurugenzi Mwanzilishi wa taasisi hiyo Ramha Abdallah.
 Katibu wa Kwanza wa Ubalozi wa Kuwait nchini Tanzania Mohammad Alamiri akikabidhi 
kofia kwa ajili ya kuzuia mwanga wa jua kwa Mkurugenzi Mwanzilishi wa taasisi hiyo Ramha Abdallah (kulia) leo jijini Dar es Salaam.
 Katibu wa Kwanza wa Ubalozi wa Kuwait nchini Tanzania Mohammad Alamiri akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa taasisi hiyo.Watatu kulia ni Katibu Mkuu wa Chama cha albino nchini Mohammed Chanzi.
 Katibu Mkuu wa Chama cha Albino Tanzania Mohammed Chanzi (aliyesimama) akizungumza kabla ya Ubalozi wa Kuiwat nchini Tanzania kutoa msaada wa vifaa kwa ajil ya watu wenye mahitaji maalum kwa Taasisi ya Humanity Actions for Children Foundation leo jijini Dar es Salaam.
Katibu wa Kwanza wa Ubalozi wa Kuwait nchini Tanzania Mohammad Alamiri(katikati) akisaini kitabu cha wageni baaada ya kuwasili  katika Taasisi ya Humanity Actions for Children Foundation kabla ya kukabidhi vifaa kwa taasisi hiyo leo jijini Dar es Salaam.Wakwanza kulia Katibu Mkuu Chama cha Albino Mohammed Chanzi na kushoto Mkurugenzi Mwazilishi wa taasisi Rahma Abdallah.

No comments: