Baadhi ya Viongozi wa Serikali na
Wajumbe wa Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa wa Simiyu wakikagua shamba la
pamba la mnufaika wa Mpango wa Kunusuru kaya Maskini(TASAF), Bibi .
Rebecca Masunga (mwenye kitambaa cheupe kichwani) wa Mtaa wa Nyakabindi
wilayani Bariadi wakati wa Ziara ya Kamati hiyo ya kukagua utekelezaji
wa Ilani ya CCM wilayani humo.
Baadhi ya Viongozi wa Serikali na
Wajumbe wa Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa wa Simiyu wakiangalia mifugo ya
mnufaika wa Mpango wa Kunusuru kaya Maskini(TASAF), Bibi . Rebecca
Masunga wa Mtaa wa Nyakabindi wilayani Bariadi wakati wa Ziara ya Kamati
hiyo ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM wilayani humo.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Enock Yakobo akimpongeza mnufaika wa Mpango wa Kunusuru kaya
Maskini(TASAF), Bibi . Rebecca Masunga wa Mtaa wa Nyakabindi wilayani
Bariadi kwa kununua jembe la kukokotwa na ng’ombe (plau) kwa ajili ya
kulimia, wakati wa Ziara ya Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa wa Simiyu
kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM wilayani humo.
Baadhi ya Viongozi wa Serikali na
Wajumbe wa Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa wa Simiyu walipotembelea na
kuona nyumba ya mnufaika wa Mpango wa Kunusuru kaya Maskini(TASAF), Bibi
. Stella Masamaki wa Mtaa wa Old Maswa wilayani Bariadi, wakati wa
Ziara ya Kamati hiyo ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM wilayani
humo.
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi,
Mhe.Festo Kiswaga akitoa maelezo ya awali juu wanafaika wa TASAF III
wilayani humo wakati wa Ziara ya Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa wa Simiyu
kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM wilayani humo.
Mkuu wa Wilaya ya Itilima,
Mhe.Benson Kilangi akitoa maelezo ya awali juu mradi wa Maji
ulioibuliwa na wanafaika wa TASAF III katika Kijiji cha Nkoma wilayani
humo wakati wa Ziara ya Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa wa Simiyu kukagua
utekelezaji wa Ilani ya CCM wilayani humo.
Mkuu wa Wilaya ya Meatu,
Mhe.Dkt.Joseph Chilongani (kulia) akiwaongoza Wajumbe wa Kamati ya Siasa
ya Mkoa wa Simiyu na baadhi ya viongozi wa Serikali kuelekea kwenye
ukaguzi wa Jengo la Wodi ya Wazazi katika Hospitali ya Wilaya ya Meatu,
wakati wa ziara ya viongozi hao ya kukagua Ilani ya CCM wilayani humo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri
ya Wilaya ya Meatu, Ndg..Fabian Manoza akitoa maelezo kwa Wajumbe wa
Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Simiyu na baadhi ya viongozi wa Serikali
kuhusu Jengo la Wodi ya Wazazi linalojengwa katika Hospitali ya Wilaya
ya Meatu, wakati wa ziara ya viongozi hao ya kukagua utekelezaji wa
Ilani ya CCM wilayani humo.
Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Mhe.Dkt.
Seif Shekalaghe akitoa maelezo kwa Wajumbe wa Kamati ya Siasa ya Mkoa wa
Simiyu na baadhi ya viongozi wa Serikali kuhusu Jengo la Zahanati ya
Kijiji cha Mwandete inayojengwa kwa ushirikiano wa Serikali na wananchi,
wakati wa ziara ya viongozi hao ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM
wilayani humo.
…………………..
Na Stella Kalinga, Simiyu
Mfuko wa Maendeleo ya Jamii
(TASAF) Awamu ya tatu umeendelea kunufaisha wananchi wakiwemo wakazi wa
kijiji cha Nkoma wilaya ya Itilima na Nyakabindi wilaya
ya Bariadi mkoaniSimiyu.
Mmoja wa wanufaika wa Mpango
huo, Bibi. Rebecca Masunga kutoka Mtaa wa Nyakabindi wilayani Bariadi,
amesema TASAF imemsaidia kutoka katika umaskini sasa anapata kipato
kinachomwezesha kujikimu, kwa kuwa amelima ekari tatu za pamba, ekari
moja ya mahindi, ana ng’ombe 14 na mbuzi wanne na amenunua plau kwa
ajili ya kulimia.
“Nilikuwa maskini wa kutupwa ,
nilipoingia TASAF na kuanza kupokea zile elfu 36 nilikopa fedha nikalima
nyanya ekari moja nikauza, nilipata shilingi laki sita nikanunua
ng’ombe watatu wakakua; baadaye nikawauza nikapata milioni moja na laki
tano nilinunua ng’ombe 14 ndiyo hao mnaowaona tunawachunga sasa”
alisema Rebecca Masunga
“Tuna kikundi chetu ambacho
tunaweka fedha zetu baadaye tunagawana, tukisha gawana tunaenda
kuzalisha, tunalima nyanya, kabeji, pamba halafu tunauza; mpango wangu
wa baadaye niwe na mtaji mkubwa na nijenge nyumba bora ” alisisitiza
Bibi.Masunga.
Nae Bibi. Stella Masamaki mkazi wa
Old Maswa wilayani amesema kupitia mpango wa Kunusuru kaya maskini
aliweza kukodi mashamba nakulima pamba, baada ya kuuza pamba akajenga
nyumba bora ya vyumba vitatu na akatoka kwenye nyumba ya udongo.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Enock Yakobo amewapongeza wanufaika wa TASAF ambao wamezitumia
fedha hizo kwa manufaa na akawashauri kuanzisha miradi midogo midogo na
kuwatumia wataalamu wa kilimo pamoja na mifugo kuwasaidia katika
uendelezaji wa miradi yao ya kilimo na mifugo.
Katika hatua nyingine Mratibu wa
TASAF Wilaya Itilima Bw. John Rajabu amesema wanufaika wa Mpango wa
Kunusuru kaya Maskini wameibua mradi wa maji ambao pia utawanufaisha na
wananchi wengine, ambapo mpaka kukamilika kwake utatumia takribani
milioni 15.
Wakati huo huo Wajumbe wa Kamati
ya Siasa ya CCM Mkoa wa Simiyu wamefanya ziara katika Wilaya ya Meatu,
Itilima na Maswa na kukagua miradi ya Maji, Afya na Elimu nakuwataka
viongozi na watendaji katika maeneo husika kutimiza wajibu wao na
kuhakikisha kuwa miradi yote inatekelezwa kwa viwango na kwa wakati ili
wananchi waweze kupata huduma wanazostahili.
Sanjali na hilo wajumbe hao
wamewataka viongozi kutambua fedha zinazochangwa na wananchi na
kusimamia vizuri kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya
maendeleo, ili zitumike kama ilivyokusudiwa.
No comments:
Post a Comment