Saturday, April 14, 2018

MTOTO WA MKULIMA WAZIRI MKUU MSTAAFU PINDA ATAJA MUAROBAINI WA KUZUIA UCHOMAJI MISITU


 Waziri Mkuu mstaafu, Mizengo Pinda, "Mtoto wa Mkulima" akionyesha furaha yake baada ya kuzindua nembo ya "Malkia wa Ssali" kwenye hoteli ya Morena mjini Dodoma leo Aprili 14, 2018.


NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID, DODOMA

WAKATI kuna wimbi la uchomaji misitu ovyo hapa nchini, “Mtoto wa Mkulima, Waziri Mkuu Mstaafu, Mhe. Mizengo Pinda ametoa “dawa” ya kuzuia uharibifu huo wa maliasili na si nyingine bali ni kufuga nyuki.

Waziri Mkuu huyo mstaafu ambaye alipenda kujitambulisha kama mtoto wa mkulima kutokana na mapenzi yake katika Kilimo, alitoa “elimu” hiyo leo Aprili 14, 2018 wakati akizindua nembo ya “Malkia wa Asali Tanzania” kwenye Hoteli ya Morena mjini Dodoma.
“Sisi upande wa Katavi tulichofanya, nilmwambia mkuu wa Mkoa sisi kuchoma choama misitu ni “tradition” (utamaduni) yaani kuchoma ni jambo la kawaida na ukitaka kuzuia hili jaribu kutumia ufugaji wa nyuki kama silaha ya kuzuia uchomaji wa miti.” Alisema na kuendelea.
Kwa hivyo alichofanya maeneo kama Inyonga, tulitenga maeneo na kuweka mabango yetu tukaweka wafugaji wa nyuki na kuwaambia ninyi ndio walinzi wetu na tangu tufanye hivyo kumekuwepo na hali nzuri sana, na uchomaji moto umepungua sana, alisema.
Mheshimiwa Pinda alitoa mfano mwingine jijini Mbeya (Mbeya city), ambako mji umezungukwa na milima mizuri yenye misitu ambayo imekuwa ikiharibiwa na uchomaji moto mara kwa mara.
“Alitokea baba mmoja Askofu Mwalyego siku moja akaja kuniambia baba mimi hii inanikera kama inavyokukera sana wewe, hivi nikijaribu ku-introduce ufugaji wa nyuki hapa itasaidia, nikamwambia try (jaribu), ameweka wafugaji wa nyuki  kuzunguka milima pale Mbeya mjini na mimi nikamwambia I will buy all your honey na juzi nikawa namuuliza zoezi langu linakwendaje, akaniambia nina miaka miwili mitatu sijaona moshi kwenye lile eneo.
Kutokana na uzoefu huo  Mtoto wa Mkulima akatoa hakikisho kuwa “Hii ni silaha moja nzuri kwa sababu mtu akielewa halimpi shida hata kidogo.” Alisema.
Mhe. Pinda pia alisema, ufugaji nyuki pia ni silaha ya kuzuia ujangili wa wanyama na kutolea mfano wa hifadhi ya misitu huko Kigoma na alipokutana na CEO pale masikitiko yake makubwa ilikuwa ni sula la ujangili na ushauri wangu nilimwambia akae na wafugaji nyuki, walau kuzunguka eneo hiulo la misitu.
“Yule bwana alijaribu na nilipomtembelea mara ya pili aliruhusu wafugaji na mfugaji bwana ukimwambia ukimwambia ukiruhusu kuingia hapa mtu ambaye hatumjui tunakufukuza hapa unaondoka na anajua ndoo moja laki moja inamkosa hakubali na kwakweli wamefanya kazi nzuri na amewafanya sasa kama askari wa wanyamapori.” Alifafanua
Akizungumzia faida ya asali, Mhe. Pinda alisema ni chakula kilichobeba virutubisho vyote ambavyo binadamu anahitaji lakini si hivyo tu, asali imekuwa na soko kubwa ulimwenguni na inaweza kuwa chanzo kimoja cha kukuza uchumi kwa wananchi na taifa kwa ujumla.

“Nawaomba sana waheshimiwa wabunge, mimi nilishatoka huko, lakini bwana Camara hapa anachohitaji ni visemeo juu ya umuhimu wa sekta hii, ni sekta ndogo lakini mchango wake unaweza kusaidia sana katika uchumi.
Aidha Mheshimiwa Pinda alisema, nchi yetu imejaliwa kuwa na eneo kubwa sana la misitu kuliko nchi nyingi na kusikitishwa wakati alipokwenda Addis-Ababa Ethiopia ambapo aliposoma jarida, aliona eti Ethiopia ndio namba moja kwa uzalishaji asali barani Afrika, nikamwambia Camara hivi Ethiopia ina uoto gani wa asili wa kuizidi Tanzania?
Alisema, mahitaji ya asali Tanzania  ni zaidi ya tani 140,000 na anaamini ni zaidi lakini Tanzania inatoa asali kidogo sana, na Ethiopia wanazalisha tani 40,000 wakati yeye (Pinda) Tanzania inazalisha tani 24,000 tu.
Nembo hiyo iliyozinduliwa ni ya kampuni ya Nyuki Safari ambayo iko chini ya Mtanzania Kaizirege David Camara na Mmarekani Mary Winzer Canning na lengo lake ni kuboresha bidhaa hiyo ya asli ili kuvutia soko.

Mhe. Pinda akiangalia Mvinyo (wine), uliotengenezwa na kampuni ya Nyuki safari ikiwa na nembo mpya ya Malkia wa Asali.
Mhe. Pinda akiungana na Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhe. Kuandikwa, (wapili kulia), Mbunge wa Urambo, Mhe. Margareth Sitta, (wakwanza kushoto), Mwanzilishi mwenza na Afisa Mkuu Mbunifu wa kampuni ya kuzalisha asali ya Nyuki Safari, Mary Winzer Canning, (wanne kushoto), na Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki, Profesa Silayo na mrembo aliyebeba nembo hiyo. 

 Mhe. Pinda na wageni wengine wakishiriki kwenye uzinduzi wa nembo hiyo.


 Mhe. Pinda wakati akitoa hotuba yake.
 Mhe. Pinda katika picha ya pamoja na Waanzilishi wenza wa kampuni ya Nyuki Safari, Bw.Kaizirege David Camara, (kushoto), na Bi. Mary Winzer David Canning.
 Bw. Kaizirege akizungumza.
 Mhe. Pinda, (katikati), Mama Sitta ba Bi. Mary


 Mkurugenzi wa Wilaya ya Chamwino, Bw.Paschal Masatu, akitoa hotuba yake
Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki, Profesa Silayo, akizungumza.

No comments: