Sunday, April 22, 2018

MBUNGE MAULID MTULIA AKAGUA ATHARI ZA MAFURIKO KATA ZA MSISIRI A, B, NA KAMBANGWA KINONDONI

ms1
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa , mtaa wa Msisiri A Jumanne Mbena akielezea changamoto za mafuriko ambazo zimesababishwa na baadhi ya wananchi kujenga kwenye Bwawa Tengeneza lililopo eneo la Msisiri A kwa Mbunge wa jimbo la Kinondoni Maulid Mtulia(CCM),akifanya ziara ya kukagua maeneo ambayo yamekumbwa na mafuriko yaliyosababishwa na mvua za masika katika en eo la Kata ya Msisiri A,Msisiri B na Kambangwa
ms2
Mbunge wa jimbo la Kinondoni Maulid Mtulia(CCM),akizungumza wakati alipofanya ziara ya kukagua maeneo am bayo yamekumbwa na mafuriko yaliyosababishwa na mvua za masika katika en eo la Kata ya Msisiri A,Msisiri B na Kambangwa
ms5
Muonekano wa maji yaliyozingira nyumba za wakazi wa Kata za Msisiri A na B na Kambangwa katika jimbo la Kinondoni jijini Dar es salaam.
ms6
Mbunge wa jimbo la Kinondoni Maulid Mtulia(CCM),akipita kwa tabu wakati  alipofanya ziara ya kukagua mae neo ambayo yamekumbwa na mafuriko yaliyosababishwa na mvua za masika katika en eo la Kata ya Msisiri A,Msisiri B na Kambangwa
ms8
Mbunge wa jimbo la Kinondoni Maulid Mtulia(CCM),akiangalia moja ya madimbwi yaliyojaa maji mtaani alipo fanya ziara ya kukagua maeneo ambayo yamekumbwa na mafuriko yaliyosababishwa na mvua za masika katika eneo la Kata ya Msisiri A,Msisiri B na Kambangwa
ms9ms10
Mbunge wa Kinondoni Abdallah Mtulia akimsikiliza Diwani Songoro Mnyonge wakati akitoa maelezo kwake kuhusu mafuriko ambayo yamewakumba wananchi wa maeneo hayo.
ms4
Mratibu wa Kanda ya Mashariki Japhary Chemgege akitoa ufafanuzi kwa Mbunge wa Jimbo la Kinondoni Abdallah Mtulia wakati wa ziara ya kukagua maeneo yaliyokumbwa na mafuriko
......................................................................................

MBUNGE wa Jimbo la Kinondoni jijini Dar es Salaam Maulid Mtulia (CCM), ametembelea maeneo ambayo yamekumbwa na mafuriko ya maji huku akitumia nafasi hiyo kutoa pole kwa wananchi wa jimbo hilo ambao wameathirika kwa namna moja au nyingine na mvua za masika huku akiishauri Halmashauri Manispaa ya Kinondoni kutafuta suluhu ya kudumu ili wananchi wabaki salama.

Pia amesema mbali ya kutoa pole atatumia fedha za Mfuko wa Jimbo kwa ajili ya kukodisha mashine za kunyonya maji pamoja na fedha ya kununua mafuta ili maji ambayo bado yapo kwenye makazi ya wananchi wake yaondolewe huku akitoa katazo la watu wasiendelee kujenga kwenye bwawa la Tengeza wala kutupa taka kwani athari zake ni kubwa kwa wananchi walio wengi.

Mbunge Mtulia amesema hayo jana jimboni kwake Kinondoni baada ya kufanya ziara ya kukagua maeneo ambayo yamekumbwa na mafuriko yaliyosababishwa na mvua za masika katika eneo la Kata ya Msisiri A,Msisiri B na Kambangwa ambapo pia ameshuhudia baadhi ya watu kujenga makazi kwenye bwawa la Tengeneza na matokeo yake maji kukosa pakwenda na hivyo kuharibu makazi ya watu.

Pia ametembelea baadhi ya nyumba za wananchi wa maeneo hayo ambapo zaidi ya asilimia 70 ya makazi ya watu yamekumbwa na mafuriko ambapo akatumia nafasi hiyo kuiomba Halmashauri ya Kinondoni kurekebisha mitaro iliyopo ili maji yapite kwa urahisi huku akitoa ombi la kuchimbwa kwa mitaro mikubwa ambayo itakuwa suluhu ya maji kutokwenda kwenye makazi ya watu kama ilivyo sasa.

Akizungumza zaidi kuhusu mafuriko hayo na athari ambazo wananchi wamezipata Mtulia amesema kwanza anatoa pole kwa wananchi hao lakini kikubwa ambacho anamini kitaisaidia wananchi hao kubaki salama ni kuangalia namna ambayo itasaidia maji hayo kutafutiwa ufumbuzi wa kudumu.
“Nimefanya ziara ya kutembelea maeneo ambayo yamekumbwa na mafuriko, nimeambatana na watalaam mbalimbali wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni na kwa maana ya mjumuiko wao ni sawa nipo kwenye ziara hii na wizara tatu.Kwa kuwa wao ni watalaamu watakuwa na njia nzuri na sahihi ya kuhakikisha unatafutwa ufumbuzi wa maji hayo kuondolewa na wananchi waendelee na maisha yao.

“Pia niombe wale ambao wanajaza taka kwenye bwawa Tengeneza waache mara moja kwani madhara yake ni maji kukosa pakwenda.Pia wale ambao wanaendelea na ujenzi nao waache ili kazi ibaki namna ya kuwasaidia waliopo wawe salama.

“Na ndio dhamira ya ziara yangu ya kwanza kuangalia athari za mvua , kutoa pole na namna ya kushirikisha watalaamu kuangalia namna ya kufanya kwa ajili ya wananchi wetu,”amesisitiza Mtulia.

Akizungumzia hatua ambazo ameamua kuzichukua hivi sasa ili kuwaondolewa wananchi hao adha ya maji ambayo bado yapo kwenye makazi yao, Mtulia amefafanua atatumia fedha za Mfuko wa Jimbo kwa ajili ya kukodisha mashine za kuvuta maji na pia atatoa fedha kwa ajili ya kununuliwa mafuta ili mashine hizo zifanye kazi.

“Kama mbunge nimeguswa na athari ambazo wananchi wamezipata lakini nitatumia fedha za mfuko wa jimbo kuhakikisha maji haya yanaondolewa kwenye makazi ya watu.Kikubwa nimeona hali ilivyo na kilichobaki sisi wanasiasa tukae na watalaam wa manispaa tutafute ufumbuzi wa muda na wa kudumu,”ameongeza Mtulia.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Msisiri A Jumanne Mbena amesema changamoto kubwa ya kujaa maji kwenye makazi ya watu inatokana na baadhi ya wananchi kujenga kwenye bwawa la Tengeneza na kufafanua ipo haja ya mbunge kushiririkiana a halmashauri kuangalia namna ya kuzuia watu wasiendelee kujenga.

Wakati huohuo Diwani Songoro Mnyonge amemwambia Mbunge kuwa ili kutafuta suluhu ya kudumi katika maeneo hayo ni kupatikana kwa mitaro mirefu ya kupitisha maji na wao walishatoa mapendekezo ya kuchimbwa mitaro mitano, hivyo mbunge asaidie katika kufanikisha hilo kwani ndio suluhu ya kudumu kwa wananchi.

“Gharama za uchimbaji wa mifereji hiyo ni kama Sh.milioni 6.5 na ukweli ni kwamba athari za mafuriko hayo ambazo wananchi wamezipata ni zaidi ya fedha hizo.Hivyo tushauri na kutoa ombi kwa mbunge wetu kutusaidia katika hili a tunaimani naye sana kuwa atatusaidiana hatimaye mitaro kuchimbwa,”amesisitiza Mnyonge.

Kwa upande wa Mratibu wa Mazingira Kanda ya Mashariki kutoka Baraza la Mazingira Japhary Chemgege amesema matatizo yanayotokea sasa ya maeneo hayo kujaa maji inatokana na baadhi ya wananchi kujenga makazi kwenye bwawa hilo ambalo kitaalam linafahamika kama tindiga.

Amefafanua maeneo ya matindiga kiasili ni maeneo ambayo yapo kwa ajili ya kuhafidhi maji na hiyo ni asili ya uumbaji wa dunia , hivyo wananchi wanapogeuza maeneo hayo kuwa makazi maana yake changamoto ya maji kujaa katika makazi ya wati itaendelea.

Amesema kisheria hairuhusiwi watu kujenga nyumba katika maeneo ya matindiga na kimsingi wanatakiwa kuondoka ili wengine wabaki salama.

No comments: