Sunday, April 22, 2018

KAIMU MURUGENZI MKUU NIDA AFANYA ZIARA SHINYANGA KUKAGUA MAENDELEO YA ZOEZI LA USAJILI NA UTAMBUZI WA WATU


Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Ndg. Albert Msovela akifungua kikao cha Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa. Kushoto ni Ndg. Andrew W. Massawe Kaimu Mkurugenzi Mkuu NIDA.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu NIDA akizungumza na wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na usalama ya mkoa wa Shinyanga. Kulia ni Katibu Tawala Mkoa Ndg Albert Msovela na kushoto ni Ndg. Alphonce Malibiche Mkurugenzi Uzalishaji Vitambulisho; na wa mwisho ni Ndg. Rose Joseph Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano.

Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Shinyanga wakisikiliza kwa makini taarifa kuhusu maendeleo ya zoezi la Usajili vitambulisho vya Taifa kwa wananchi mkoani humo.
Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Shinyanga wakisikiliza kwa makini taarifa kuhusu maendeleo ya zoezi la Usajili vitambulisho vya Taifa kwa wananchi mkoani humo.
Viongozi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa NIDA wakiwa katika picha ya pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Shinyanga baada ya kumaliza kikao na kuweka mikakati ya pamoja ya kuwasajili wananchi na kumaliza zoezi kwa wakati.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu NIDA Ndg. ,Andrew W. Massawe akiweka saini kwenye kitabu cha wageni, mara alipowasili kwenye ofisi ya Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga. Pembeni ni Katibu Tawala huo Ndg Albert Msovela
Wananchi wa Kijiji cha Usanda Kata ya Tinde mkoani Shinyanga walivyokutwa kwenye foleni ya Usajili Vitambulisho vya Taifa kwenye zoezi linaloendelea mkoani humo wakati wa ziara ya Kaimu Mkurugenzi Mkuu aliyoifanya hivi karibuni.
Bi. Magdalena E. Ngosha mkazi wa kijiji cha Usanda Kata ya Tinde akichukuliwa alama za vidole na Afisa Usajili wa Mamlaka ya Vitambulisho wakati wa zoezi la Usajili linaloendelea kijijini hapo.

…………………………………………………………………………..

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida), Ndg. Andrew W. Msssawe amekutana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Shinyanga na kusisitiza umuhimu wa kukamilisha Usajili wananchi mkoani humo mwezi Mei mwaka huu ili NIDA kupata muda wa kutosha kufanya uhakiki na mapingamizi kwa wale wote waliosajiliwa; na kuwezesha Mamlaka kuzalisha vitambulisho kwa wakati.

Kauli hiyo ameitoa wakati wa ziara yake mkoani Shinyanga kukagua maendeleo ya zoezi la Usajii na Utambuzi wa Watu linaloendelea; akiwa ameambatana na Mkurugenzi Uzalishaji Vitambulisho Ndg. Alphonce Malibiche, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Bi.Rose Mdami na Ndg. Steven Kapesa Mkuu wa Kitengo cha Vihatarishi.

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa huo; Katibu Tawala wa Mkoa huo Ndg. Albert Msovela amesema mkoa wa Shinyanga una changamoto kubwa ya wahamiaji haramu hususani Wilaya ya Kahama na kwamba wamejipanga Usajili katika eneo hilo kufanyika kwa uangalifu mkubwa kwa kuhusisha vyombo vyote vya Ulinzi na Usalama.

Kwa upande wake Afisa Uhamiaji Mkoa Ndg.Bashiri Mang’enya amemhakikishia Mkurugenzi Mkuu wa NIDA; Idara yake imejipanga vizuri kuhakikisha maafisa Uhamiaji wa kutosha wanakuwepo wakati wote wa zoezi na kwa kushirikiana na NIDA watu wote wenye sifa kuwa wanasajiliwa kwa kusimamia misingi na taratibu zote za Usajili kwa mujibu wa sheria.

Aidha; Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NIDA Ndg. Andrew W. Massawe ameushukuru uongozi wa Mkoa wa Shinyanga kwa jitihada kubwa wanazozifanya kuhakikisha Usajili unafanyika pamoja na kuwepo changamoto nyingi; na kuahidi kuongeza vifaa kwa maana ya mashine za Usajili na watendaji ili kuongeza kasi ya Usajili.

Mkoa wa Shinyanga ni miongoni mwa mikoa iliyoanza usajili mwezi Septemba mwaka jana; na hadi sasa Wilaya ambazo ziko kwenye hatua ya kukamilisha Usajili ni Shinyanga na Kishapu huku Wilaya ya Kahama ikitegemea kuongezewa nguvu kubwa ili zoezi hilo kukamilika mwezi Mei mwaka huu.

No comments: