Mwenyekiti
wa Bodi ya Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF), Spika mstaafu,Anne Makinda
akizungumza na wanawake wa Mfuo huo leo jijin Dar es Salaam wakati
wakisheherekea siku ya wanawake duniani.
Imeelezwa
kuwa mashirika mengi yamekuwa yakianguka na kukosa mweelekeo kwa
sabababu ya washirika wake kuwa na mahusiano ya mapenzi wao kwa wao
wawapo kazini.
Kauli
hiyo imetolewa na Mwenyekiti Wa bodi Wa mfuko wa Taifa Wa bima ya afya
NHIF Spika wa bunge mstaafu Anne Makinda wakati Wa sherehe za
kuadhimisha siku ya wanawake iliyofanywa na shirika hilo ofsini kwao
jijini Dar es salaam.
Akizungumza na watumishi Wa NHIF Makinda amesema kuwa na mahusiano kazini yanakufanya usijiamini uwapo kazini.
"Ukiwa
na mahusiano na bosi wako hata kama utafanya Kazi kwa juhudi na
kupandishwa cheo itaonekana kama umepanda kwa sababu mahusiano mliyokuwa
nayo,"alisema Makinda.
Makinda amewaasa wafanyakazi wa NHIF wafanye Kazi kwa uaminifu na waache makandokando.
Kwa
upande wake Mkurungenzi Mkuu wa NHIFA Bernard Konga amesema shirika lao
linasimamia suala zima la usawa wa kijinsia na watahakikisha wanawake
wenye sifa wanapanda cheo.
Aidha
Rose Gabriel ambae ni Mwenyekiti wa akina mama NHIF ametoa rai kwa
wanawake kusherekea siku ya wanawake kwa kudumisha Umoja na mshikikamano
Amesema unapokuwa kazini masuala ya mahusiano uachane nayo na kufanya kazi kwa waminifu pamoja na kujituma kwa bidii.
Mkurugenzi
Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Bernard Konga
akizungumza machache katika leo jijin Dar es Salaam wakati
wakisheherekea siku ya wanawake duniani.
Mwenyekiti
wa Bodi ya Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF), Spika mstaafu, Anne Makinda
akikata keki leo wakati wakisheherekea siku ya wanawake duniani.
Mwenyekiti
wa Bodi ya Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF), Spika mstaafu, Mhe,Anne
Makinda akimlisha keki Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya
(NHIF), Bernard Konga.
Mwenyekiti
wa Bodi ya Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF), Spika mstaafu Anne Makinda
akipokea zawadi kutoka kwa Mwenyekiti wa wanawake wa (NHIF)Rose Gabriel.
Mwenyekiti
wa Bodi ya Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF), Spika mstaafu, Anne Makinda
akimkabidhi zawadi wa kikombe Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima
ya Afya (NHIF), Bernard Konga.
Mwenyekiti
wa Bodi ya Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF), Spika mstaafu, Anne Makinda
akilishwa keki na Mwenyekiti wa wanawake wa (NHIF)Rose Gabriel.
Baadhi
ya wanawake wakiwa katika makoo makuu ya (NHIF) jijini Dar es Salaam
wakisheherekea siku ya wanawake duniani ambayo hufanyika kila Machi 8
kila mwaka kwaajili ya kujua mchango wa mwanamke katika nafasi
mbalimbali za ajira pamoja na kujua dhamani ya Mwanamke katika jamii.
No comments:
Post a Comment