Sunday, March 11, 2018

Dkt.Abbas apongeza utafiti uliofanywa na Misatan kwa kushirikiana na CPESA

Na.Vero Ignatus Arusha.

MSEMAJI Mkuu wa Serikali Dkt.Hassan Abbas amesema Maafisa Mawasiliano serikalini bado wanakabiliwa na changamoto kutoka kwa mabosi wao, ikiwano wengine kutokutaka habari zao zisikike kwenye vyombo vya habari.

Dkt.Abbas aliyasema hayo jana mjini hapa wakati mapitio ya ripoti ya upatikanaji wa Taarifa Tanzania uliofanywa na Taasisi ya vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika(MISATAN) ikishirikiana na Taasisi ya CIPESA ya nchini Uganda.

Alisema kupitia ripoti hiyo aliyoiunga mkono na kuisoma vyema atahakikisha maofisa mawasiliano zaidi ya 300 wanaokutana mjini Arusha wanapata utafiti huo."Nimesoma utafiti huu, kurasa zote upo vizuri, niwaombe muendelee kufanya tafiti kama hizi kwani ni chakula kwetu," alisema Dkt. Abbas.

Akizungumzia utafiti uliofanywa katika mikoa 7 na MISATAN Wakili wa mahakama kuu James Marenga amesema ofisi za halmashauri ya mikoa ya Arusha na kigoma ,walau ndiyo zimeonekana ndiyo wanafanaya vizuri katika kuwa wazi katika utoaji wa taarifa kuliko ofisi za mikoa.

Dodoma manispaa,halmashauri ya Jiji la mbeya,Kigoma ofisi ya mkuu Arusha, ofisi ya mkuu wa mkoa Mwanza hakukuwa na ushirikiano,vilevile mkoa wa Mtwara hakukuwa na ushirikiano ,Dar ni katika halmashari ya Jiji,Kwahiyo Utafiti huo ulikuwa umegawanya utoaji  wa taarifa kwa ofisi za mkuu wa mikoa na ofisi za halmashauri au za Majiji katika mikoa iliyochaguliwa.

Moja ya mapendekezo yaliyotolewa baada ya utafiti huo vitengo vya watoa taarifa vinaimarishwa kama inavyotakiwa  katika sheria ya haki  kupata taarifa ya mwaka 2016.Vilevile utafiti huo unasisitiza kuwepo na uwazi katika utoaji wa taarifa haswa kwenye taasisi za serikali.


Msemaji mkuu wa Serikali Dkt.Hassan Abbas,akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano wa siku moja uliofanyika Jijini Arusha ,ulioandaliwa na MISATAN kwa kushorikiana na CIPESA.
Kaimu Mkurugenzi Gasirigwa Sengiyumva
Wakili wa Mahakama Kuu Janes Marenga akifafanua jambo katika mkutano wa siki moja uliaondalowa na Misatan na kufanyika Jiiini Arusha.
Mshiriki kutoka nchini Uganda akichangia jambo katika mkutano huo.
Baadhi ya wadau mbàlimbali pamoja na waandishi walioshiriki katika mkutano huo Jijini Arusha.
Mwandishi wa Gazeti la Habari leo Veronica Mheta akichangia mada katika mkutano huo
Mwenyekiti wa MISATAN Salome Kitomari akizungumza katika mkutano huo uliofanyika Jijini Arusha
Mmoja wa washiriki kutoka CIPESSA akitoa mada katika mkutano huo
Msemaji wa TANAPA Paschal Shelutete akichangia jambo katika mkitano huo.
Kaimu mkurugenzi wa MISATAN nchini Gasirigwa Sengiyumva (wa kwanza kushoto)akiwa na mmiliki wa Wazalendo Blog,Gadiola Emmanuel (mwenye skafu nyekundu shingoni)
 Mafunzo yakiendelea katika Hotel ya Impala Jijini Arusha.

No comments: