Saturday, March 17, 2018

KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA DKT. JUMA MALEWA AONGOZA KIKAO MAALUM CHA KUJADILI MIKAKATI YA JESHI LA MAGEREZA KUJITOSHELEZA KWA CHAKULA

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, Dkt. Juma Malewa, akisalimiana na Kamishna wa Utawala na Fedha wa Magereza, Gaston Sanga mara baada ya kuwasili kwenye viwanja vya Nanenane, Mkoani Mororogoro tayari kwa Kikao Maalum cha Maafisa Waandamizi wa Jeshi hilo. Kikao hicho kimefanyika kwa siku moja leo 17 Machi, 2018 Mkoani Morogoro.
Kamishna wa Fedha na Utawala wa Magereza, Gaston Sanga akitoa neno fupi kabla ya kumkaribisha Kamishna Jenerali wa Magereza kufungua rasmi kikao kazi hicho.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, Dkt. Juma Malewa akiongoza Kikao Maalum cha kujadili mikakati ya utekelezaji wa Jeshi la Magereza kujitosheleza kwa chakula.
Wajumbe wa Kikao hicho ambao ni Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza wakifuatilia kwa makini maelekezo kutoka kwa Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa(hayupo pichani).
Washiriki wa Kikao kazi ambao ni Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza wakifanya maadiliano mbalimbali katika vikundi kama inavyoonekana katika picha.
Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Magereza Mikoa yote Tanzania Bara(waliosimama mstari wa nyuma) mara baada ya ufunguzi rasmi wa kikao maalum cha kujadili mikakati ya utekelezaji wa Jeshi la Magereza kujitosheleza kwa chakula. Kikao hicho kimefanyika kwa siku moja leo 17 Machi, 2018 Mkoani Morogoro.Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza

No comments: