Tuesday, March 6, 2018

BASF YAANZISHA KIWANDA CHA UZALISHAJI WA KEMIKALI ZA UJENZI JIJINI DAR ES SALAAM

-Uzalishaji utapunguza kwa kiasi kikubwa muda wa usambazaji kwa wateja.
- Uzalishaji wa michanganyiko mbalimbali ya saruji utazingatia makubaliano ya ushuru.
- Kituo hicho kipya cha uzalishaji kitachochea huduma bora kwa wateja kwa kutumia teknolojia ya BASF yenye ufumbuzi wa bidhaa bora.

Kampuni inayoongoza kwa utengenezaji wa kemikali duniani vilevile kemikali za ujenzi , imeanza kuwekeza madhubuti kwenye uzalishaji wa ndani na hivi leo imekabidhi kituo cha uzalishaji nchini Tanzania. Kiwanda hicho ambacho kitazalisha mchanganyiko wa saruji, kitatumika kupitia makubaliano maalum ya ushuru na kitatoa ufumbuzi wa kibunifu ili kuiwezesha BASF kukidhi mahitaji ya wateja.

Kutokana na kiwanda hicho kipya, kitengo cha kemikali na ujenzi BASF kitajiimarisha katika wigo wa kuwafikia wateja wake wengi zaidi na kukidhi mahitaji ya soko huku ikitoa ufumbuzi wa hali ya juu katika sekta ya ujenzi. "Uwekezaji huu ni hatua nyingine muhimu kwa BASF Afrika.

Ushiriki wetu katika bara la Afrika unaongezeka na jukumu kubwa muhimu linalotekelezwa na kitengo hichi ni kutazama zaidi kwenye nchi zenye mipango mizuri na fursa kubwa, kama vile Tanzania "alisema Michael Gotsche, ambaye ni Makamu wa Rais wa BASF Afrika.

Christian Geierhaas ambaye ni Makamu wa Rais wa kitengo cha kemikali za ujenzi Upande wa Mashariki ya Kati, Asia Magharibi, CIS & Afrika, alisema kuwa "Kuwekeza nchini Tanzania, kutaiwezesha kitengo hicho kuleta bidhaa zenye teknolojia ya hali ya juu na ufumbuzi zaidi kwa wateja wetu katika soko hili muhimu."

Maarifa ya BASF katika kemia yatawanufaisha wadau wote katika sekta ya ujenzi kuwa endelevu kwa kukuza teknolojia zaidi nchini. Uwekezaji huu ni uthibitisho wa ahadi ya BASF ili kuonyesha uwepo wake Tanzania. "Kipaumbele chetu muhimu ni kuyafikia zaidi matarajio ya wateja. Huu ni wakati mzuri kwetu BASF katika biashara yetu nchini Tanzania na kuongeza nyayo zetu hapa nchini ni sehemu ya mkakati wetu wa ukuaji wa biashara," alisema Anand Sinha, Meneja Mauzo Ujenzi, kitengo cha kemikali na ujenzi BASF Tanzania Ltd.
***
Kuhusu BASF
BASF tunatengeneza kemikali kwa maendeleo endelevu ya baadaye. Tunaunganisha mafanikio ya kiuchumi na kulinda mazingira na uwajibikaji wa kijamii.
Kuna wafanyakazi zaidi ya 115,000 katika timu ya BASF na hufanya kazi katika kuchangia mafanikio ya wateja wetu katika kila sekta na karibu kila nchi duniani.

Kampuni yetu imegawanyika katika vitengo vitano: Kitengo cha Kemikali, Bidhaa za utendaji kazi, Vifaa vya utendaji kazi & Ufumbuzi, Ufumbuzi wa Masuala ya Kilimo pamoja na Mafuta na Gesi. Mauzo ya jumla ya BASF kwa mwaka 2017 ni Euro 64.5 bilioni. BASF inamiliki hisa Frankfurt (BAS), London (BFA) na Zurich (BAS). Tembelea tovuti yetu kwa maelezo zaidi www.master-builders-solutions.basf.co.tz

Kuhusu BASF Tanzania
BASF Tanzania Ltd ilianzishwa mwishoni mwa mwaka 2015 na ina ofisi zake Dar es Salaam. Ofisi inasimamia vitengo mbalimbali kwenye viwanda lakini imejielekeza zaidi kwenye kitengo cha kemikali za ujenzi na kilimo.

Tembelea tovuti yetu kwa maelezo zaidi www.master-builders-solutions.basf.co.tz

Kuhusu Kitengo cha Wataalamu wa Ujenzi na Ufumbuzi BASF
Kitengo hiki hushughulika zaidi kwenye kemikali kwa ajili ya ujenzi mpya, matengenezo, ukarabati wa miundo. Kitengo hiki kimejengwa kutokana na uzoefu uliopatikana kutoka zaidi ya miaka 100 katika sekta ya ujenzi.

Pia kitengo hiki hujumuisha kusimamia uchanganyaji wa saruji, virutubisho kwenye saruji, kemikali kwa ajili ya ujenzi wa chini ya ardhi, ufumbuzi wa maji na kukarabati. Kitengo hiki kinasimamiwa na jumuiya ya kimataifa ya wataalamu wa ujenzi wa BASF. Ili kutatua changamoto za ujenzi wa wateja wetu, tunachanganya ujuzi wetu tulioupata katika maeneo mengine katika miradi duniani kote.

Tunatumia teknolojia za kimataifa za BASF pamoja na ujuzi wetu wa kina ili kuendeleza ubunifu ambao husaidia wateja wetu kufanikiwa zaidi na kufanya ujenzi endelevu. Tembelea tovuti yetu kwa maelezo zaidi www.master-builders-solutions.basf.co.tz

Kuhusu kitengo cha Kemikali za Ujenzi
Kitengo cha Kemikali za ujenzi BASF, hujishughulisha na kemikali kwa ajili ya ujenzi mpya, matengenezo na ukarabati wa miundo: kazi zetu zinajumuisha mchanganyiko wa sarujii, vifaa vya kuziba, mfumo wa kukarabati na kulinda sakafu, mfumo wa kuweka vigae, mfumo wa kuhifadhi mbaovidonge vya saruji, ufumbuzi wa kemikali kwa ajili ya ujenzi wa chini ya ardhi, mifumo ya maji mifumo ya kudhibiti upanuzi. 

Kitengo cha Kemikali za ujenzi kina wafanyakazi 6,000 kukiwa na wataalamu kutoka mataifa mbalimbali ambao huhusika kutatua matatizo ya wateja ili kusaidia kukamilika kwa mradi. Tunaunganisha ujuzi wetu wa utaalamu kutokana na uzoefu uliopatikana katika miradi mingine duniani kote. 

Tunatumia teknolojia za kimataifa za BASF, pamoja na ujuzi wetu wa kina ili kuendeleza ubunifu ambao husaidia wateja wetu kufanikiwa zaidi na kuendesha ujenzi endelevu. Kitengo hicho hufanya uzalishaji katika vituo na vituo vya mauzo katika nchi zaidi ya 60 na kufikia mauzo ya dola bilioni 2.3 mwaka 2016.

No comments: