Thursday, February 15, 2018

WAZIRI KALEMANI ASHIRIKI MAKABIDHIANO YA SOKO LA SAMAKI, UTIAJI SAINI UJENZI WA BARABARA, CHATO

Waziri wa Nishati ambaye pia ni Mbunge wa Chato, Dkt. Medard Kalemani leo tarehe 14 Februari, 2018 ameshiriki makabidhiano ya Soko la Kimataifa la Samaki la Kasenda lililojengwa chini ya ufadhili wa Serikali ya Japan kwa gharama ya Dola za Marekani 148,146. Aidha, Waziri Kalemani ameshiriki utiaji saini wa mkataba kati ya Serikali ya Japan na Tanzania kwa ajili ya ukarabati wa barabara yenye urefu wa kilomita moja ya Muganza kwa gharama ya Dola za Marekani 90,645.
Balozi wa Japan Nchini, Masaharu Yoshida (kulia) akibadilishana nyaraka na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Chato, Joel Hari (kushoto) mara baada ya kusaini mkataba kati ya Serikali ya Tanzania na Japan kwa ajili ya ukarabati wa barabara ya Muganza kwenye uzinduzi huo. Katikati anayeshuhudia ni Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani.
Balozi wa Japan Nchini, Masaharu Yoshida akisoma hotuba katika uzinduzi huo.
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani akisisitiza jambo katika uzinduzi huo.

Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi Robert Gabriel akielezea mafanikio ya mkoa wake katika uzinduzi huo.
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (wa tatu kushoto, waliosimama mbele) Balozi wa Japan Nchini, Masaharu Yoshida ( wa n ne kushoto, waliosimama mbele) wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wa mkoa wa Geita mara baada ya uzinduzi wa Soko la Kimataifa la Samaki la Kasenda.
Sehemu ya wananchi wa Kitongoji cha Kasenda kilichopo wilayani Chato mkoani Geita wakisikiliza hotuba iliyokuwa inatolewa na Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (hayupo pichani) katika uzinduzi huo.

Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (katikati mbele) akicheza pamoja na kikundi cha Mwagazege katika uzinduzi huo.

No comments: