Sunday, February 4, 2018

WAZIRI JENISTA MHAGAMA : WCF KUFUNGUA OFISI KWA AWAMU MIKOANI KURAHISISHA UTOAJI HUDUMA ZAKE

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama (MB), akizungumza kwenye warsha ya siku moja ya kuwajengea uelewa wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhusu majukumu ya Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), kwenye ukumbi wa Msekwa, Bungeni mjini Dodoma Februari 3, 2018. Kulia ni Mwenyekiti Mwenza wa Bunge, Mhe. Andrew Chenge, na katikati ni Mwenyekiti wa Warsha hiyo, ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Kamatui ya Bunge ya Katiba na Sheria na Mwenyekiti Mwenza wa Bunge, Mhe. Najma Giga.

NA K-VIS BLOG/Khalfan Said, DODOMA

KUANZISHWA kwa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi ni hatua muafaka katika mazingira ya sasa ambapo kuna ongezeko la maeneo ya uzalishaji hususan viwanda kunakokwenda sambamba na ongezeko la matukio ya athari zinazotokana na ajali, magonjwa ama vifo kutokana na kazi, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama amewaambia wabunge wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wakati wa warsha ya kujenga uelewa kwa wabunge kuhusu majukumu ya Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), mjini Dodoma Februari 3, 2018.

Mhe. Mhagama alisema warsha hiyo ni utekelezaji wa ombi lililotolewa na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria  kutaka wabunge wajengewe uelewa wa shughuli za Mfuko huo.
Akifafanua zaidi Mhe. Waziri alisema Mfuko uliundwa Julai 2015 chini ya kifungu cha 5 cha Sheria ya Fidia kwa wafanyakazi, sura 263 marejeo ya mwaka 2015 ili kulipa Fidia stahiki kwa mfanyakazi aliyeumia, kupata maradhi au kifo wakati akitekeleza majukumu yake ya kikazi kwa mujibu wa mkataba.
Alisema, Serikali ilianzisha Mfuko huo  kwa lengo la kuhakikisha kuwa wafanyakazi wanapata Mafao bora ya Fidia tofauti na Sheria ya zamani ya Fidia kwa Wafanyakazi ambayo viwango vyake vya Mafao ya Fidia vilikuwa vya chini mno.
“Mathalan viwango vya juu vya Fidia kwa Mfanyakazi aliyepata ajali kazini ilikuwa ni shilingi 108,000/= huku Mfanyakazi aliyefariki katika ajali ama ugonjwa kutokana na kazi anayofanya kwa mujibu wa Mkataba wa ajira yake ilikuwa ni shilingi 83,000.” Alibainisha Mhe. Waziri.
Alisema tangu kuanzishwa kwa Mfuko huo, mafanikio mbalimbali yamefikiwa ikiwa  ni pamoja na kupata hati safi kwa hesabu za mwaka 2015/2016 na 2016/2017 zilizokaguliwa na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), usajili wa waajiri 12,546 hadi kufikia Januari 31, 2018, na kulipa Fidia kiasi cha shilingi bilioni 1.6 kwa wafanyakazi 1,144.
"Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2016/17) na Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 ambavyo vinatekelezwa kwa kasi kubwa na Serikali ya awamu ya tano chini ya uongozi mahiri wa Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, vinalenga kukuza uchumi wa viwanda na kuboresha maisha ya Watanzania na hatimaye kuifanya Tanzania kuwa nchi yenye kipato cha kati ifikapo mwaka 2025." Alisema Mhe. Waziri.
"Katika kuhakikisha Mfuko unaendelea kuboresha huduma zake na kuhakikisha wadau wanapata huduma kwa urahisi zaidi na katika ufanisi wa hali ya juu, Mfuko utafungua ofisi mikoani kwa awamu." alisema.
Kwa sasa Mfuko unatekeleza majukumu yake mikoani kwa kutumia Maafisa Kazi wa Mikoa.  
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba alisema, katika mazingira yab sasa ambapo serikali ya awamu ya tano chini ya uongozi wake Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli ya kujenga uchumi wa viwanda, jukumu la Mfuko halitakuwa kulipa Fidia pekee bali pia kubuni, kukuza na kuendeleza mbinu za kupunguza ama kuzuia kabisa ajali katika maeneo ya kazi.
“Ili kuwezesha kufanikisha hilo, Waheshimiwa wabunge mnao umuhimu wa kipekee katika kutoa uelewa sahihi wa madhumuni, majukumu na uendeshaji wa Mfuko.”
Matarajio ya Mfuko ni kupata ushirikiano wa kutosha kutoka kwa wadau wote, (Waajiri, wafanyakazi, Mashirika mbalimbali ya Kimataifa, mashirika yasiyo ya kiserikali, hospitali na vyombo vya habari, alifafanua  Bw. Mshomba.
Akizungumzia majukumu muhimu ya Mfuko, Bw. Mshomba alitaja kuwa ni pamoja na kusajili waajiri na wafanyaakzi, kukusanya michango kutoka kwa waajiri, kulipa fidia stahiki kwa mfanyakazi na wategemezi na kuwekeza ili kujenga uwezo wa kulipa fidia.
Katika warsha hiyo ya siku moja, waheshimiwa wabunge walipata fursa ya kuelimishwa juu ya utaratibu unaotumika kufanya tathmini ya Mfanyakazi aliyeumia, kupata maradhi au kifo wakati akitekeleza wajibu wake wa kazi aliyoajiriwa kwa mujibu wa mkataba ili hatimaye Mfuko utoe Fidia stahiki.
Lakini pai wabunge walielezwa muundo wa Mfuko huo ambapo umezingatia mfumo jumuishi, kwa maana ya kuwa na bodi ya uwakilishi wa makundi mbalimbali ili kukidhi malengo ya kuanzishwa kwa Mfuko.

  Mhe. Najma Giga(katikati), akizungumza wakati wa ufunguzi wa warsha hiyo. Kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria, iliishauri serikali juu ya umuhimu wa waheshimiwa wabunge kukutana nna wataalamu kutoka WCF ili kuwajengea uelewa wa shughuli za Mfuko. 
 Mhe. Andrew Chenge, akizunhgumza kwenye warsha hiyo.
 Baadhi ya waheshimiwa wabunge na viongozi wa WCF wakifuatilia warsha hiyo.
 Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Bw. Masha Mshomba, akitoa mada juu ya  uelewa wa jumla kuhusu utekelezaji wa Matakwa ya kifungu cha 5 cha Sheria ya Fidia kwa wafanyakazi, sura 263 marejeo ya mwaka 2015 mjini Dodoma leo Februari 3, 2018.

 Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Bw. Masha Mshomba, akitoa mada juu ya  uelewa wa jumla kuhusu utekelezaji wa Matakwa ya kifungu cha 5 cha Sheria ya Fidia kwa wafanyakazi, sura 263 marejeo ya mwaka 2015 mjini Dodoma leo Februari 3, 2018.

 Mbunge wa Kuteuliwa na Rais, Mhe.Mama Salma Kikwete, akisikiliza kwa makini mada iliyokuwa ikitolewa na Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba wakati wa warsha hiyo.
Mkurugenzi wa Uendeshaji wa WCF, Bw. Anslem Peter akitoa mada juu ya muundo wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, ikiwa ni pamoja na uongozi na bodi ya wadhamini ambayo ni shirikishi.
Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini, Dkt. Abdulsalam Omar, akitoa mada kuhusu utaratibu unaotumika kufanya tathmini ya Mfanyakazi aliyeumia, kupata maradhi au kifo wakati akitekeleza wajibu wake wa kazi aliyoajiriwa kwa mujibu wa mkataba kabla ya Mfuko kutoa Fidia.
Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala, Wizara ya Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Bw.Peter Kalonga, akimwakilisha Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, akizungumza.

Baadhi ya waheshimiwa wabunge kwa shauku kubwa wakifuatilia mada zilizokuwa zikitolewa na wataalamu wa WCF.

Kutpka kushoto, Mhe. Jenista Mhagama, Mhe. Andrew Chenge na Mhe. Najma Giga, wakifuatilia maelezo yaliyokuwa yakitolewa na Mkurugenzi Mkuu wa WCF.
Timu ya wataalamu wa WCF, kutoka kushoto ikiongozwa na Mkurugenzi Mkuu, Bw. Masha Mshomba,  Mkurugenzi wa Uendeshaji wa WCF, Bw. Anslem Peter, Mkurugenzi wa Huduma za Fedha na Utawala, Bw.Bezil Kwala, Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini, Dkt. Abdulsalam Omar na Mkuu wa Huduma za Sheria Bw. Abraham Siyovelwa.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makzi, Mhe. William Lukuvi, (katikati), akibadilishana mawazo na  Meneja Madai (Claims), wa WCF, Bi. Rehema Kabongo, (kushoto na Meneja Matekelezo, (Compliance), Bw.Bw.Victor Luvena mwishomi mwa warsha hiyo.
Wabunge juu na chini wakipitia vipeperushi vyenye maswali na majibu kuhusu shughuli za Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, 9WCF), wakati wa warsha ya kuwajengea uelewa kuhusu Mfuko huo.





Mbunge wa Nkasi, Mhe. Ali Kesy(kulia) na mbunge mwenzake wakiwa kwenye warshan hiyo.
Mkurugenzi wa Huduma za Fedha na Utawala, Bw.Bezil Kwala, akizungumza mbele ya waheshimiwa wabunge.
Meneja Madai (Claims), wa WCF, Bi. Rehema Kabongo, akizunguzma kwenye warsha hiyo ya wabunge.

Mbunge  wa jimbo la Mafinga Mjini Mhe.Ndugu Cosato David Chumi, akizungumza kwenye warsha hiyo.

Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Medard Kalemani, (Kusbhoto), akiteta jambo na Mbunge wa Mtwara vijijini Mhe. Hawa Ghasia, (katkati) na Mhe. Mbunge ambaye jina lake halikupatikana wakati wa warsha hiyo.
Mhe. Waziri na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge, wakiwa katika picvha ya pamoja na uongozi wa WCF.
Mhe. Waziri Jenista Mhagama, Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Angelina Mabula, (wapili kulia), Mwenyekiti Mwenza wa Bunge, Mhe. Andrew Chenge, (wapili kushoto), Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba, wabunge na viongozi wengine wa Mfuko, wakiwa katika picha ya pamoja
Mheshimiwa Waziri Jenista Mhagama, akipeana mikono na Mkuu wa Mkuu wa Huduma za Sheria Bw. Abraham Siyovelwa. 

Mheshimiwa Waziri Jenista Mhagama akiagana na Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Mshomba na viongozi wengine wa Mfuko huo. 

No comments: