Wednesday, February 28, 2018

VIONGOZI MTWARA FUATILIENI WATU WANAOTAKA KUHARIBU MASOKO YA KOROSHO-MAJALIWA

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa na mkewe Mary Majaliwa (kulia) wakimsikiliza Meneja Uzalishaji wa Kiwanda cha Korosho cha Tandahimba Cashew, Abdulrahman Sinani, wakati alipotembelea kiwanda hicho, kilichopo Wilayani Tandahimba, Mkoani Mtwara, kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Gelasius Gasper Byakanwa, Februari 28, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa na mkewe Mary Majaliwa (katikati) wakiangalia mashine ya kubangulia korosho katika Kiwanda cha Korosho cha Tandahimba Cashew, kilichopo Wilayani Tandahimba, Mkoani Mtwara, kushoto ni Meneja Uzalishaji wa kiwanda hicho, Abdulrahman Sinani, Februari 28, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na mbanguaji korosho Zuhura Abdallah, katika Kiwanda cha Korosho cha Tandahimba Cashew, kilichopo Wilayani Tandahimba, Mkoani Mtwara, katikati ni Mke wa Waziri Mkuu Mary Majaliwa na kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Gelasius Gasper, Februari 28, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akioneshwa mashine ya kuchambua korosho na Meneja Uzalishaji wa kiwanda hicho, Abdulrahman Sinani  katika Kiwanda cha Korosho cha Tandahimba Cashew, kilichopo Wilayani Tandahimba, Mkoani Mtwara, kulia ni Mke wa Waziri Mkuu Mary, Februari 28, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akioneshwa mashine ya kukaushia korosho na Meneja Uzalishaji wa kiwanda hicho, Abdulrahman Sinani  katika Kiwanda cha Korosho cha Tandahimba Cashew, kilichopo Wilayani Tandahimba, Mkoani Mtwara, kulia ni Mke wa Waziri Mkuu Mary, Februari 28, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiangalia ubora wa korosho, iliyo teyari kuliwa, wakati alipotembelea Kiwanda cha Korosho cha Tandahimba Cashew, kilichopo Wilayani Tandahimba, Mkoani Mtwara, kulia ni Mke wa Waziri Mkuu Mary, Februari 28, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)



WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka viongozi wa mkoa wa Mtwara kupambana na makundi ya watu yanayotaka kuharibu masoko ya korosho.

Hatua hiyo imekuja baada ya kuwepo kwa mnunuzi aliyekataa kununua korosho kutokana na kutoridhishwa na kiwango cha ubora wa korosho alichokikuta ghalani.Ametoa agizo hilo leo (Jumatano, Februari 28, 2018) wakati akizungumza na watumishi na madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Tandahimba.

“Tandahimba korosho zote ni daraja la kwanza sasa korosho chafu zinatoka wapi? Kuna kundi linataka kuharibu soko lazima tupambane nalo.”Waziri Mkuu ameongeza kuwa “lazima mshirikiane kuwabaini walioleta korosho chafu Tandahimba na wakipatikana wachukuliwe hatua kali za kisheria.”

Amesema haiwezekani mnunuzi amenunua korosho daraja la kwanza alafu anakuja anakuta korosho nyingine tena chafu, lazima waliozibadilisha wasakwe. Awali, Waziri Mkuu alitembelea kiwanda cha kubangua korosho cha Amama Farms, ambapo ametoa wito kwa walionunua viwanda vya korosho wafunge mashine mpya na kuanza uzalishaji.

Hata hivyo amewataka wamiliki wa viwanda vyote vya kubangulia korosho washirikiane na Serikali katika kufuata utaratibu wa kununua korosho.Pia Waziri Mkuu amezindua barabara yenye urefu kilomita tatu iliyojengwa kwa kiwango cha lami ambayo imegharimu sh. bilioni 1.38 zilizotokana na mapato ya ndani ya Halmashauri ya wilaya ya Tandahimba.

Kwa upande wake Meneja wa Kiwanda hicho Kwa Mahmoud Sinani alisema korosho zinazobanguliwa kiwandani hapo zinauzwa ndani na nje ya nchi.Amesema katika awamu ya kwanza ya uwekezaji huo umegharimu sh. bilioni 12 na wanatarajia kuendelea na awamu ya pili ambapo watawekeza dola milioni 20.

Amesema kwa sasa kiwanda hicho kimeajiri watumishi 250 na wanatarajia kuajiri watumishi 1,500 mara baada ya kumaliza awamu ya pili ya upanuzi wa kiwanda.Pia Waziri Mkuu amewapongeza watendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Tandahimba kwa kuweka kipaumbele katika ujenzi wa miundombini ya barabara kwa kiwango cha lami.


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMATANO, FEBRUARI 28, 2018.

No comments: