Monday, February 19, 2018

TAXIFY YAZINDUA HUDUMA MPYA YA ‘TAXIFY BAJAJ’JIJINI DAR ES SALAAM


Shivachi Muleji, Meneja Maendeleo wa Taxify, Kanda ya Afrika Mashariki akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa hafla ya uzinduzi wa huduma mpya ya 'Taxify Bajaji' mwishoni mwa juma. Application hiyo ni maalum kwa ajili ya kurahisisha usafiri wa Bajaj kwa wakazi wa jiji la Dar es salaam. Taxify sasa inapiga hatua nyingine katika kuleta suluhisho la usafiri hapa jijini, baada ya uzinduzi wa App yake kwa ajili ya magari miezi miwili iliyopita jijini Dar es salaam. Gharama za Taxify Bajaji kwa kipindi hiki zitakuwa kama ifuatavyo ya kuanzia TZS; Sh 750, TZS 350 kwa kila kilometa moja. TZS 75 kwa dakika huku bei ya kiwango cha chini ikiwa ni Shilingi 2000

Shivachi Muleji, Meneja Maendeleo wa Taxify, Kanda ya Afrika Mashariki akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa hafla ya uzinduzi wa huduma mpya ya 'Taxify Bajaji' mwishoni mwa juma. Application hiyo ni maalum kwa ajili ya kurahisisha usafiri wa Bajaj kwa wakazi wa jiji la Dar es salaam. Taxify sasa inapiga hatua nyingine katika kuleta suluhisho la usafiri hapa jijini, baada ya uzinduzi wa App yake kwa ajili ya magari miezi miwili iliyopita jijini Dar es salaam. Kushoto ni Meneja Uendeshaji wa Taxify Tanzania, Remmy Eseka.
Fenelisti Simon Metumba, Dereva wa Usafiri wa Bajaji jijini Dar es salaam akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) mwishoni mwa juma wakati wa hafla ya uzinduzi wa huduma mpya ya 'Taxify Bajaji'. App maalum iliyozinduliwa na kwa ajili ya kurahisisha usafiri wa Bajaj kwa wakazi wa jiji la Dar es salaam. Taxify sasa inapiga hatua nyingine katika kuleta suluhisho la usafiri jijini Dar es Salaam, baada ya uzinduzi wa App yake maalum kwa ajili ya magari miezi miwili iliyopita jijini Dar es salaam.
 
 

 Februari 2018, Dar es Salaam. Taxify, ambayo imejitanua katika utoaji wa huduma zake barani Ulaya na Afrika, leo imetambulisha huduma yake mpya ya ‘Taxify Bajaj’ ambayo ni App maalum kwa ajili ya Usafiri wa Bajaj huku wakiichagua Dar es salaam kuwa jiji la kwanza katika uzinduzi wa huduma hii.

Kupitia uzinduzi wa huduma hiyo, Taxify sasa imepiga hatua zaidi katika jitihada zake za kupunguza msongamamo jijini Dar es Salaam, mara baada ya uzinduzi wa App yake maalum kwa ajili ya usafiri wa teksi miezi miwili iliyopita.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo jijini Dar es Salaam, Meneja wa Maendeleo Taxify, Kanda ya Afrika Mashariki, Shivachi Muleji alisema, ‘Taxify Bajaj’ ni App mpya ya Taxify jijini Dar es Salaam ambayo inaunganisha watumiaji wa usafiri wa Bajaji na madereva ndani ya dakika chache.

"Tunafurahi sana kuanzisha huduma hii kwa mara ya kwanza kabisa jijini Dar es Salaam pia ni tumaini letu kuwa huduma hii itapokelewa vyema. Tunaamini kwamba huduma hii inaendana na utamaduni wa wakazi wa jiji hili na kwamba itatoa urahisi wa watu kuchagua usafiri anaoutaka kwa gharama nafuu pindi mtu anapotaka kufanya safari zake za mjini”

Bei ya Taxify Bajaj ni kama ifuatavyo: -Nauli halisi ni TZS 750, TZS 350 kwa Km, TZS 75 kwa dakika, wakati bei ya chini kabisa itakuwa ni TZS 2,000.

Programu ya Taxify inapatikana kwenye mifumo ya Android na iOS na ina sifa za kipekee kama kutumia ETA yako na rafiki au mpendwa wakati wa safari, ambapo itakuwezesha kufanya makadirio ya kukodisha kabla ya safari na pia kupata msaada wa huduma kwa wateja kutoka ndani ya programu.

Kwa upande wake, Meneja Mwendeshaji wa Teknolojia hiyo nchini Tanzania, Remmy Eseka alisema, programu yao ya teksi ambayo ilizinduliwa hivi karibuni jijini Dar es Salaam imepokelewa vizuri sana mpaka kufikia sasa, zaidi ya kampuni ilivyotarajia hivyo inawahakikishia watumiaji wa wake kuwa Taxify itaendelea kuwepo hapa nchini.

"Kama kampuni ya teknolojia, Taxify daima inaangalia njia ambazo inaweza kufanya ili kutoa ufumbuzi bora katika usafiri. Sisi daima tunaendelea kujibu haraka na kwa ufanisi mahitaji ya masoko mbalimbali ambako tunafanya kazi. Hivi ndivyo tunavyoweza kuwa mbele kwenye soko la ushindani na kuwa namba moja kuongoza katika masoko yetu yote, "alisema Eseka.

Usafiri wa Bajaj unekuwa maarufu sana katika miji mikubwa likiwemo jiji la Dar kwa sababu usafiri huu ni suluhisho kwenye njia zenye foleni zaidi kuliko magari.Kuongezeka kwa matumizi ya usafiri huu, unazifanya kampuni mbalimbali za Kiteknolojia kama Taxify kuja na suluhisho na kuboresha huduma hii ili kuwafikia watu wengi zaidi ambao wanapenda aina hii ya usafiri.

No comments: