Monday, February 19, 2018

BINSLUM ATAKA MSHIKAMANO COASTAL UNION

Mkuu wa wilaya ya Tanga,Thobias Mwilapwa akizungumza katika hafla ya kuwapongeza wachezaji wa timu ya Coastal Union baada ya kupanda daraja kucheza Ligi kuu msimu ujao katika halfa iliyofanyika kwenye Hotel ya Tanga Beach Resort Mjini Tanga kushoto ni Mwenyekiti wa timu ya Coastal Union Steven Mguto na Mfadhili wa timu hiyo Nassoro Binslum 
Mfadhili wa timu hiyo Nassoro Binslum akizungumza katika halfa hiyo kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili Hemed Aurora
Mwenyekiti wa Klabu ya Coastal Union,Steven Mguto akizungumza katika halfa hiyo kushoto ni Mfadhili wa timu hiyo Nassoro Binslum kulia ni Mkuu wa wilaya ya Tanga,Thobias Mwilapwa 
Kocha Mkuu wa timu ya Coastal Union Juma Mgunda katika akiwa na Kocha wa Makipa Salim Waziri kushoto na kocha Msaidizi Joseph Lazaro kulia 
Mfadhili wa timu ya Coastal Union Nassoro Binslum kushoto akisalimiana na mchezaji wa timu hiyo,Athumani Iddi Chuji
Mfadhili wa timu ya Coastal Union Nassoro Binslum kushoto akiwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili Hemed Aurora 
Mkuu wa wilaya ya Tanga,Thobias Mwilapwa kulia akimkabidhi tuzo Mchezaji Athumani Iddi Chuji ambazo zimeandaliwa na mfadhili wa timu hiyo ,Nassoro Binslum kwa ajili ya kuwapongeza wachezaji wa timu hiyo baada ya kuipandishi timu hiyo kucheza Ligi kuu
Mkuu wa wilaya ya Tanga,Thobias Mwilapwa akimkabidhi tuzo Mlinda Mlango wa timu ya Coastal Union Sharifu Kasilasi kwa mchango wao wa kusaidia timu hiyo kupanda daraja
Kocha Msaidizi wa timu ya Coastal Union Joseph lazaro akipokea naye tuzo kutrokana na mchango wao waliuonyesha kwenye michuano ya Ligi Daraja la kwanza na kusaidia timu hiyo kupanda daraja(Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha) 
Mkuu wa wilaya ya Tanga,Thobias Mwilapwa kulia akimkabidhi tuzo Kocha Mkuu wa timu ya Coastal Union Juma Mgunda baada ya kufanikisha timu ya Coastal Union kupanda daraja
Mkuu wa wilaya ya Tanga,Thobias Mwilapwa akimkabidhi tuzo Kocha wa Makipa wa timu ya Coastal Union,Salim Waziri 
Mkuu wa wilaya ya Tanga,Thobias Mwilapwa kulia akimkabidhi tuzo beki wa timu ya Coastal Union Hamad Juma 
Sehemu ya wachezaji wa timu ya Coastal Union wakiwa na wake zao wakipata chakula kwenye halfa hiyo 
Mwenyekiti wa Kamat ya Usajili ya Coastal Union Hemed Aurora kushoto akiteta jambo na Mwandishi wa Gazeti la Majira mkoani Tanga Mashaka Mhando 
Meneja wa Hotel ya Tanga Beach Resort Joseph Ngoyo akiteta jambo na mdau wa michezo wakati wa hafla hiyo ya kuwapongeza wachezaji wa timu hiyo 
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Coastal Union Hemed Aurora katika akiwa na Mfadhili wa timu hiyo Nassoro Binslum kushoto ni Mwenyekiti wa Baraza la Wazee Salim Bawaziri


Mkuu wa Idara ya Mawasiliano ya Klabu ya Coastal Union,Hafidhi Kidoh kulia akisalimiana na mwandishi wa gazeti la Majira Tanga Mashaka Mhando kwenye halfa hiyo ya kupongeza wachezaji iliyofanyika kwenye ukumbi wa Hotel ya Tanga Beach Resort Mjini Tanga 


UONGOZI wa timu ya Coastal Union “Wagosi wa Kaya” umetakiwa kushikamana na kutoruhusu migogoro na makundi yasiyokuwa na tija kwani yanaweza kukwamisha ndoto zao za kupata mafanikio katika msimu ujao wa Ligi kuu soka Tanzania Bara. 
Lakini pia waaache vurugu na chokochoko iwapo wanataka kupata mafanikio huku wakitakiwa kuangalie wale wachache watakaopelekea hali hiyo wasiwaunge mkono kwa kuonyesheni mfano wamewachoka. 
Hayo yalibainishwa na Mfadhili wa timu hiyo,Nassoro Binslum wakati akizungumza kwenye ghafla ya kuwapongeza wachezaji wa timu hiyo sambamba na utolewaji wa zawadi baada ya kupanda daraja kucheza ligi kuu msimu ujao iliyofanyika kwenye ukumbi wa Hotel ya Tanga Beach Resort 
Alisema tatizo kubwa ambalo limekuwa likirudisha nyuma mafanikio ya timu hiyo ni majungu,fitina na makundi ndani na nje ya timi hiyo hivyo ni bora viongozi,wapenzi ,wanachama wakabadilika na kuongeza mshikamano . 
Binslum alisema umoja ulioonyeshwa na viongozi,wanachama na washabiki wakati timu ilipokuwa inatafuta nafasi ya kupanda ligi kuu unatakiwa uendelezwe ili uwe na tija kwa timu hiyo ili iweze kurudisha heshima yake ya miaka ya nyuma kuchukua ubingwa. 
Aidha alisema wakati timu zinapokuwa kwenye madaraja ya chini kunakuwa hakuna majungu wala makundi maana kipindi hicho hakuna udhamini wale fedha lakini inapopanda timu kila mtu anaweza kujitokeza kwa kueleza anaweza kuongoza. 
“Ndugu zangu niwaambie tuwaache viongozi,benchi la ufundi na wadhamini na sisi wengine tubaki tu kama wachezaji wa kumi na mbili kuisapoti timu na tukifanya hivyo tutafanikiwa sana kwani tutakuwa tumeweka msingi mzuri na imara “Alisema Binslum. 
Kwa upande wake Mwenyekiti kamati ya usajili Hemed Aurora alisema mbali na mafanikio hayo jambo kubwa litakalozingatiwa kuhakikisha makundi hayatakuwa na nafasi ili kuepusha yaliyoikuta timu hiyo na kupelekea kushuka daraja. 
Aurora alisema uwendeshaji wa timu unagharama kubwa itakayokuwepo si kutafuta ubingwa wa ligi kuu bali kuhakikisha kunajengwa umoja utakaoleta mafanikio na kupambana na wale wasiokuwa na nia njema na timu hasa baada ya timu hiyo kupanda. 
“Tunatambua sasa kazi ndio inaanza ni zaidi ya miaka 30 kihistoria tangu timu hiyo iliptwaa ubingwa lakini ubingwa si kazi kama tutashikamana na kuwapinga kwa pamoja wale maadui zetu wanaosubiri timu ipande waseme timu yao tutawashughulikia safari hii”Alisema. 
Awali akizungumza Mkuu wa Wilaya Tanga Thobias Mwilapwa alisema timu kurudi kucheza ligi kuu kunafaida kubwa sana kwa wanamichezo tu ikiwemo wakazi wa mkoa huo kwani itasaidia kuinua ukuaji wa uchumi ndani ya Halmashauri ya Jiji. 
Aidha alisema serikali iliahidi vitu vingi juu ya timu hiyo siku ya
mapokezi yake ilipokuwa ikitokea Morogoro na jukumu lililopo ni utekelezaji wake ambao unaweza kuleta tija zaidi na timu nyingine kupanda na kufikia idadi kama ya zamani. 
Hata hivyo alisema serikali imejitoa zaidi kuhakikisha inaisaidia timu hiyo iweze kuwa tishio na kwenye michuano ya Ligi kuu msimu ujao huku akizitaka zilizobakia nazo kuhakikisha zinaweka mipango imara ya kupanda ili kukuza vipaji vya vijana wetu na uchumu wa pato mkoa kwa kupitia michezo. 
Kwa upande wake,Mwenyekiti wa timu hiyo,Steven Mguto alisema wataendelea kushikamana ili kuhakikisha wanatimiza malengo yao ya kufanya vizuri kwenye michuano ya ligi kuu soka Tanzania Bara msimu ujao. 
Aliongeza kuwa mshikamano waliouonyesha wakati wa michuano hiyo ya Ligi Daraja la kwanza wataendelea nao ili kuhakikisha wanarudisha enzi za miaka 1988 walipotwaa ubingwa wa Ligi kuu Tanzania Bara.

No comments: