Sunday, February 4, 2018

TATUMZUKA YACHANGIA VIFAA VYA SHULE NA MATANKI YA MAJI WILAYA YA UBUNGO.

 Katibu Tawala wilaya ya Ubungo ,James Mkumbo akizungumza na Waandishi wa habari mwishoni mwa wiki kuhusu wilaya hiyo kupokea msaada wa baadhi ya vifaa Vya shule,kama vile Madawati 25,Vitabu 131 pamoja Matanki makubwa mawili  ya kuhifadhia maji kutoka kwa wachezeshaji wa Mchezo wa kubahatisha wa TatuMzuka.Kulia ni Mwakilishi wa TatuMzuka,Bi Patronela. Mkumbo alisema kuwa wamepewa msaada wa vifaa hivyo kutokana na mkazi wa wilaya hiyo ya Ubungo,aitwaye Catherine Tryphone kushinda kitita cha Milioni 60 kupitia mchezo huo wa TatuMzuka.
 Mwakilishi wa mchezo wa kubahatisha wa TatuMzuka,Bi.Patronela akikabidhi Vitabu 131 kwa ajili ya shule za Wilaya hiyo ya Ubungo kwa  Katibu Tawala wilaya ya Ubungo ,James Mkumbo,kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Wilaya ya hiyo,Ally Juma Ally akishuhudia tukio hilo.
 Mwakilishi wa mchezo wa kubahatisha wa TatuMzuka,Bi.Patronela akikabidhi madawati 25 kwa Kaimu Mkurugenzi wa Wilaya ya hiyo,Ally Juma Ally,pichani kati anaeshuhudia ni Katibu Tawala wilaya ya Ubungo ,James Mkumbo.Pichani nyuma kulia ni moja ya tanki lililokabidhiwa kwa viongozi hao wa Serikali.

No comments: