Tuesday, February 6, 2018

TANZANIA,CHINA KUSHIRIKIANA KUONGEZA WATALII.


Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

TANZANIA na China zimeamua kushirikiana kwa lengo la kukuza soko la utalii nchini.

Hivyo imeelezwa watu maarufu na mashuhuri wa nchi ya China akiwamo mwigizaji maarufu wa nchi hiyo Maododo atakuwa miongoni mwa watakaokuja kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo.Hatua inakuja kipindi ambacho kumekuwa na uchache wa watalii wa kutoka China kuja Tanzania,hivyo moja ya mkakati wa kuongeza watalii hao ni kuweka ushirikiano kwenye eneo la utalii.

Akizungumza katika mkutano ulioandaliwa na Ubalozi wa China kwa kushirikiana na Bodi ya Utalii Nchini (TTB) uliofanyika leo Dar es salaam, Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Jaji Mstaafu Thomas Mihayo amesema uhusiano wa China na Tanzania ni wa muhimu sana.

Amefafanua kuwa wana wanampango wa kubadilisha mfumo ili Wachina waingie kwa wingi nchini na kuboresha soko la utalii nchini China.Amesema fursa ya Wachina kushirikiana katika utalii i ni nzuri hasa  ikitumika ipasavyo."Kwani wamepata nafasi ya kuwatumia watu maarufu kutoka nchini China ili kusaidia kutangaza utalii wa Tanzania na moja ya watu maarufu watakaotumika kama mabalozi wa kutangaza Utalii ni muigizaji maarufu kutoka China.

" Anayejulikana kwa jina maarufu la 'Maudodo' pamoja na Mhifadhi wa Mazingira na Wanyamapori na Mtafiti wa Sokwe Mtu Sokwe wa Mkoa wa Kigoma ,Dk. Jane Goodal,"amesema.Amefafanua kuwa wameamua kutumia wazo hilo kwa sababu wana mvuto kwenye jamii.Jaji Mstaafu Mihayo ameongeza bodi ya utalii nchini iko tayari kushirikiana bega kwa bega na China ili kufikisha soko la utalii mbali na kuwa la kimataifa.Amesema Tanzania ina kila aina ya vivutio vya kipekee ilivyojaliwa na ni vya asili kabisa.

Kwa upande wa Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii, Meja Jenerali Gaudence Milanzi amesema wameamua kushirikiana na China kwa sababu China ni watu wanaosafiri sana duniani kote."Hivyo hivyo itasaidia kwa kiasi kikubwa kuutangaza na kutengeneza soko la utalii nchini," amesema.

Milanzi ameipongeza China kwa kupiga marufuku bidhaa zinazotengenezwa kwa kutumia malighafi ya meno ya Ndovu(Tembo) na faru kwani  ni jambo jema na itasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza ujangili."Tunaomba nchi nyingine nazo kuiga walichokifanya China kwa lengo la kukabiliana na ujangili," amesema.

Amesema Wachina wanatalii nchi mbalimbali lakini Tanzania wana asilimia moja katika kufanya utalii,hivyo ushirikiano huo lazima uendane na utalii.
 Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii, Meja Jenerali Gaudence Milanzi akizungumza wakati akifungua  mkutano wa ushirikiano kati ya Tanzania na China katika sekta ya Utalii jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii, Jaji Mstaafu Thomas Miyayo akizungumza kuhusiana na utalii nchini wakati wa mkutano wa ushirikiano kati ya Tanzania na China katika sekta ya Utalii uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
 Mhifadhi wa Mazingira na Wanyamapori  na Mtafiti wa Sokwe Mtu  Sokwe wa Mkoa wa Kigoma ,Dk. Jane Goodal akizungumza kuhusiana na Utalii nchini leo jijini Dar es Salaam.
 Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii, Meja Jenerali Gaudence Milanzi akiwa katika picha ya pamoja na wa vatendaji wa TTB wadau wa Utalii wa China.
 Msanii Maarufu nchini China, Nanping Liu akikabidhi zawadi Mhifadhi wa Mazingira na Wanyamapori  na Mtafiti wa Sokwe Mtu  Sokwe wa Mkoa wa Kigoma, Dk. Jane Goodal katika Mkutano wa Utalii jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wadau wakiwa katika mkutano wa wadau utalii kati ya Tanzania na China leo jijini Dar es Salaam.

No comments: